Andrew Kibe amkashifu Peter Salasya kwa kulishwa keki na mwanaume mwenzake

“Eti rafiki yako ndio anakulisha keki? Kwani hakukuwa na msichana wa kuhudumia wateja katika mgahawa huu? Wanaume pia nyinyi mnafanya mzaha sana, hizi ndio picha zinatrend?” aliongeza.

PETER SALASYA AKILISHWA KEKI
PETER SALASYA AKILISHWA KEKI
Image: FACEBOOK

YouTuber Andrew Kibe ameonesha kutofurahishwa kwake baada ya picha ya mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya akilishwa keki na mwanamumec mwenzake klabuni kuibuka.

Picha hiyo ya Salasya ni ya kutoka Agosti 22 ambapo alihudhuria hafla katika klabu moja jijini Nairobi ambapo alikaribishwa kwa kulisgwa keki.

“It was nice meeting @brianmwenda_ and @kenya_prince01 vijana ya town ....mlinipigia story mpaka nikacheka yangu yote nikaisha yote waaah .You people you are amazing and thank you @alfakheer.tr for hosting me for the first time...hakuna kitu napenda mtu kunipigia story za jaba 😄 🤣 😂 😆 wananifanya niwe wazimu kwa kucheka,” Salasya aliandika kwenye picha hizo alizochapisha kwenye kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, picha hiyo ilimkera Andrew Kibe ambaye alitoa dhana kwamba hakuna kitu chochote kinachoweza kumpa ruhusa mwanamume kukubali kulishwa keki na mwanamume mwenzake.

Kulingana na Kibe, kama mwanamume, hata baba yako mzazi hafai kukulisha keki mdomoni.

“Kama utanipata nimelewa na kitu ambacho unataka kufanya ni kunilisha mdomoni, heri uniachilie niende. Inawezekanaje unamlisha mwanamumke mwenzako keki ukiwa umemuangalia mdomoni? Sioni kuna wakati utafika nijipate kwa hali kama hii na marafiki zangu, haiwezi kutokea,” Kibe alisema.

“Eti rafiki yako ndio anakulisha keki? Kwani hakukuwa na msichana wa kuhudumia wateja katika mgahawa huu? Wanaume pia nyinyi mnafanya mzaha sana, hizi ndio picha zinatrend?” aliongeza.

Salasya katika picha hiyo alikuwa analishwa keki na Brian Mwenda, mwanamume aliyejipata katika mikono ya sheria kwa kutuhumiwa kuhudumu kama mwanasheria bila vibali maalum.