• “Bado niko katika maabara ya mkate, ninaokwa nikijishughulisha na nitakapomaliza mtaipenda zaidi,” Vishy alisema.
Pritty Vishy ameonesha muonekano wake mpya baada ya kimya cha muda katika mtandao wa instagram.
Vishy, alionyesha picha akiwa amerembeshwa na kufichua kwamba huo ni mwanzo tu wa kushughulikia urembo wake kwani bado yuko jikoni anashughulikiwa.
Mrembo huyo aliahidi kwamba kufikia wakati atakapokamilisha kushughulikia urembo wake, mashabiki wake wataupenda zaidi muonekano wake.
“Bado niko katika maabara ya mkate, ninaokwa nikijishughulisha na nitakapomaliza mtaipenda zaidi,” Vishy alisema.
Akizungumzia kimya cha muda katika mitandao ya kijamii, mrembo huyo alifichua kwamba katika kipindi cha miezi michache iliyopita, alikula yamini ya kujipenda, kujikubali na kuweka maslahi yake binafsi mbele katika kila uamuzi.
“Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, nilijiahidi kwamba nitajifunza jinsi ya kujipenda na katika kila mapunguzu. Lakini pindi ninapojaribu ndivyo ninavyopotelea katikati. Natamani nyinyi wote mngejua jinsi ninavyojaribu lakini inaonekana kwamba hii itakuwa safari ngumu zaidi katika maisha yangu,” Vishy alisema.
“Nahisi macho yangu yameanza kuwa mazito kusema kweli,” aliongeza.
Vishy amekuwa mmoja wa warembo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifanyiwa utani usiofurahisha wakinyanyapaliwa na kukejeliwa kuhusu mionekano ya miili yao.,
Hata hivyo, amekuwa akisimama tisti kwa ukakamavu na kuonekana kutojali wanachosema watu, huku akiwema furaha ya nafsi yake katika mstari wa mbele.