Stevo Simple Boy afafanua kauli yake kumtaka Diamond kumlipa Sh20m kabla ya kolabo

“Media za Tanzania zilinipigia, wakisema stevo umefanya jambo la maana sababu tunaona kazi yako huko Kenya, pia wakasema Diamond ana kila haki ya kutoa sh20m ndio nimpe kolabo,” alifafanua.

Muhtasari

• “Media za Tanzania zilinipigia, wakisema stevo umefanya jambo la maana sababu tunaona kazi yako huko Kenya, pia wakasema Diamond ana kila haki ya kutoa sh20m ndio nimpe kolabo,” alifafanua.

DIAMOND NA SIMPLE BOY
DIAMOND NA SIMPLE BOY
Image: HISANI

Msanii Stevo Simple Boy kwa mara ya kwanza amejibu maswali kuhusu ni kwa nini alimtaka gwiji wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kumlipa shilingi milioni 20 pesa za Kenya ili kufanya kolabo na yeye.

Akizungumza kwenye runinga ya K24, mkali wa Freshi Barida alifafanua kauli hiyo akisema kwamba alikuwa anamtaka Diamond kurudisha mkono vkwa Wakenya.

Kwa mujibu wa Simple Boy, Wakenya wamchangia pakubwa mafanikio ya Diamond kimuziki hivyo ni wakati wake kurudisha shukrani kwa kumlipa sh20m kama mwakilishi wa Wakenya kwa ajili ya kolabo.

“Ni kweli nilisema hivyo kwa sababu ukiangalia sisi kama Wakenya, tumesapoti Diamond mpaka mahali amefika. Kwa nini yeye asirudishe mkono afanye kolabo na msanii wa Kenya?” Stevo alisema.

Msanii huyo pia alikwenda hatua zaidi na kufichua kwamba kauli hiyo iliwatia kiwewe sana watanzania kiasi kwamba vyombo vingi vya habari kutoka nchini humo walimfikia kwa njia ya simu wakimtaka kufafanua zaidi.

“Media za Tanzania zilinipigia, wakisema stevo umefanya jambo la maana sababu tunaona kazi yako huko Kenya, pia wakasema Diamond ana kila haki ya kutoa sh20m ndio nimpe kolabo,” alifafanua.

Wiki mbili zilizopita, Stevo alisema bila kupepesa jicho kwamba bila sh20m kwake hapati kolabo.

"Diamond, ulinitumia meseji kwenye Instagram ukisema unataka collabo, lakini usipokohoa Sh20 milioni, hakuna dili," Stevo Simple Boy alisema.