• Vera Sidika waliweka wazi mahuisiano yao ya kimapenzi na Brown Mauzo mapema mwaka 2021 na kuachana mwaka 2023.
• Katika kipindi kifupi cha mapenzi yao, wawili hao walibarikiwa na watoto wawili.
Mwanasosholaiti na mfanyibiashara Vera Sidika amelaumu ujio wa janga la Covid-19 kwa kuolewa kwake.
Sidika anasisitiza kwamba halikuwa lengo lake kuingia kwenye ndoa hata kwa siku moja lakini ujiuo wa Covid-19 mapema mwaka 2020 lilimsababishia kukubali kuingia kwenye ndoa na msanii Brown Mauzo.
Covid-19 ilifanya shughuli nyingi zikiwemo za kusafiri hapa na pale kusitishwa na wengi wakalazimika kutulia nyumbani, hivyo Sidika naye alijipata ametulia Kenya bila kusafiri nje mara kwa mara na hilo likampelekea kuingia na kutulia kwenye ndoa.
Alisema kwamba miaka 8 kabla, alikuwa amekiri tena kwenye kipindi kimoja cha runinga humu nchini kwamba ndoa ni utapeli na hajui kilimsibu kipi mpaka kukubali kuingia katika ndoa haswa.
“Huyu ni mimi miaka 8 nyuma. Kila mara nilikuwa nasema nisingekubali kuingia katika ndoa. Sijui nini kilinitokea wakati wa Covid-19, lakini nimeshakuwa pale na niamini mimi ninaposema ndoa ni utapeli. Siwezi tena,” Mama huyo wa watoto wawili alisema.
Vera Sidika waliweka wazi mahuisiano yao ya kimapenzi na Brown Mauzo mapema mwaka 2021 na kuachana mwaka 2023.
Katika kipindi kifupi cha mapenzi yao, wawili hao walibarikiwa na watoto wawili.