• Shabiki huyo wa Liverpool alikuwa ameweka ujumbe wa kushangilia baada ya timu yake kuichabanga Man United Jumapili jioni.
Msemaji wa ikulu Hussein Moammed amelalamika kupitia ukurasa wa X kwamba mashabiki wanamkebehi hata kwenye mzaha wa soka.
Shabiki huyo wa Liverpool alikuwa ameweka ujumbe wa kushangilia baada ya timu yake kuichabanga Man United Jumapili jioni.
Hata hivyo, mashabiki wa Man Utd walifurika katika ukurasa huyo na kumpa mipasho wengine wakivuta siasa ndani ya utani huo wa so0ka.
Mohamed ambaye katikac siku za hivi karibuni amekuwa akipata wakati mgumu kutetea sera za rais William Ruto alichapisha ujumbe mwingine akishangaa mbona hadi kwenye utani wa soka bado anaburuzwa tu.
Hata hivyo, alisisitza kwamba anawakubali wote wanaomfuata kwenye mtandao wa kijamii na kuwatania zaidi mashabiki wa Man Utd kwamba wasipojipanga tena katika mkutano ujao bado watapigwa tu.
“Eh, Jameni! Hata banter ya soka mnanilima tu? Lakini bado nawapenda wote! Anyway, pongezi kwa marafiki zangu wazuri wa Man United. Ushindi ulikuwa wa kutisha. Mjipange next time! Habari za asubuhi!” Hussein Mohamed alisema.
Liverpool iliichabanga Manchester United Jumapili jioni katika uga wa OLD Trafford mabao 3-0.