Kenyan Prince ahusisha ajali za barabarani na uchawi

Mfanyabiashara wa Forex Kenyan Prince ameelezea sababu za kuwa akipata ajali za barabarani kila mara

Muhtasari

• Prince,amevunja kimya baada ya yeye kupata ajali za barabara , akisema chuki, wivu na uchawi ndiyo sababu kuu.

•Kenyan prince amekuwa akipata ajali za barabarani, si mara moja tu,  akini amekuwa akiponea na kutokea salama.

KENYAN PRINCE.
KENYAN PRINCE.
Image: Instagram

Mfanyibiashara wa Forex Kenyan Prince amejitokeza kuelezea bayana sababu za yeye kuwa akipata ajali mara kadha wa kadha. Prince hivi maajuzi alipata ajali iyosababisha gari lake kuharibika na yeye kupata majeraha madogo.

Akizungumza na kikao cha wanahabari, alidai kuwa sababu kubwa ya yeye kuwa akipata ajali za barabarani ni kuwa watu wanamwonea  wivu na wamejawa na chuki, aidha akisema kikubwa zaidi ni uchawi.

'Nyinyi wote ni wachawi,people are bad out here;there's nothing else,there's external forces acting ,thats why niko na taabu mingi,but on God,everything will be okay' kenyan Prince alisema.

Kenyan prince amekuwa akipata ajali za barabarani, si mara moja tu,  akini amekuwa akiponea na kutokea salama licha ya magari yake kuharibika vibaya.

Prince, amekuwa akivuma hasa kutokana ba ufanyabiashara wa Forex , kupitia video katika mtandao wa tiktok huku akionyesha posho analotengeza kupitia biashara hiyo.

Ikumbukwe kuwa ni hivi maajuzi mfanyabiashara mwenza kwa jina Sammy Boy, pia aliponea ajali ya barabara na ambapo kwa sasa anazidi kuuguza majeraha katika hosipitali ya Agha Khan, na ambapo afya yake inazidi kufanya vyema licha ya kuratibiwa upasuaji na akiwashukuru wafuasi kwa sapoti yao kwake.