• Nadia alielezea jinsi walikutana na kufichua kwamba Arrow Bwoy ndiye aliyemkaribia na kumsalimia akimtambua kwa jina lake.
Msanii Nadia Mukami kwa mara nyingine amefichua jinsi walipokutana na kuanza safari ya mapenzi na baba mwanawe, Arrow Bwoy.
Akizungumza na Obinna wakati wa ziara yake ya kutangaza albamu yake mpya, Queen of the East, alifichua kwamba walikutana kwa klabu kwenye sherehe lakini Arrow Bwoya mara kwa mara hupinga hilo.
Nadia alielezea jinsi walikutana na kufichua kwamba Arrow Bwoy ndiye aliyemkaribia na kumsalimia akimtambua kwa jina lake.
“Sisi tulikutana kwenye klabu lakini Arrow Bwoy hajawahi kukubali kwamba tulikutana kwenye klabu. Huo wakati nilikuwa na meneja wangu wa zamani tulikuwa tumefilisika hatuna chochote tumeketi tu hapo mbele tunaitisha soda pekee bila pombe. Arrow Bwoy alikuwa anatesa siku hizo na walikuwa kwenye safu ya juu na kina KRG,” Nadia alikumbuka.
“Ilikuwa ni Club 64, lakini kalba ya hapo, tulikuwa kwenye group moja ya WhatsApp alikuwa ananiona najituma narusha ngoma zangu pale. Mimi nilikuwa nimeshatumbuiza ngoma yangu na staa Arrow Bwoy ndiye alikuwa anakuja kufunga.”
“Wakati akitumbuiza, alikuja kwenye meza yetu na kusema ‘mambo Nadia’ na akarudi jukwaani, lakini leo hii ukimuuliza hawezi kubali aliniita kwa jina langu. Infact sasa anasema alikuw hanijui na hivyo ndivyo tulikutana,” Mukami alisimulia.
Baadae, meneja wake alimtaka kuwasiliana na Arrow Bwoy na hivyo ndivyo walikutana kwenye studio wakarekodi ngoma na baadae penzi lao likaota.