Thomas Müller azungumzia suala la mkataba mpya Bayern

Mshambulizi huyo amesema yuko imara na anaweza akaongeza mkataba mpya katika kikosi cha Bayern Munich.

Muhtasari

•"Tusubiri tuone chenye kitatokea,mwili tuu ndio unazeeka lakini ni jambo ambalo nazidi kupambana nalo," alisema.

THOMAS MULLER
Image: HISANI

Mchezaji matata anayechezea klabu ya Bayern Munich inayoshiriki katika ligi kuu ya Ujerumani almaarufu Bundesliga, amesema kwamba yuko imara zaidi na ana uwezo mkubwa wa kuwa katika kikosi cha kwanza katika timu hiyo.

Müller ambaye amaekuwa akionyesha ubabe na kutumikia timu hiyo ya Bayern kwa miaka mingi, amesema kuwa anataka kujitangaza kwa kuwa anauwezo mkubwa licha ya umri wake kusonga.'tusubiri tuone chenye kitatokea,mwili tuu ndio unazeeka lakini ni jambo ambalo nazidi kupambana nalo'.

Müller ambaye ana umri wa miaka 34 ,amekuwa nguzo muhimu katika timu hiyo na kuisaidia kunyakua mataji likiwemo la ligi.

Müller ana uzoefu kutokana na kujumuishwa katika mechi nyingi ambapo ameonyesha kiwango cha juu cha mchezo na kuwa na tajriba ya kutosha.

Müller,amecheka na nyavu mara si haba akichezea timu ya taifa pamoja na klabu ya Bayern Munich.

Bayern Munich ambao msimu jana walishindwa kutetea taji lao,baada ya timu ya Bayern Leverkusen kutwaa ushindi pasina kupoteza mechi hata moja chini ya ukufunzi wake xhabi Alonso.

Klabu hiyo yake ya Bayern Munich,itakuwa na mageuzi baada ya kupata kocha mpya na aliyekuwa mchezaji wa mapema wa Manchester City,Vincent Kompany na kuridhi mikoba yake Julian Nagelsman.