Davido amjibu shabiki aliyemwambia amebadilika tangu afunge ndoa

Itakumbukwa kuwa Davido na mkewe, Chioma walifanya harusi yao tarehe 25 mwezi wa Juni na hafla hiyo ilihudhuriwa na mastaa wakubwa.

Muhtasari

• Kupitia jukwaa la X, Davido alichapisha ujumbe kwamba anaipenda sana familia yake kwa maana ya mkewe Chioma Rowland

Mkali wa Afrobeats, Davido amemjibu kwa upendo shabiki yake mmoja aliyemwandikia kupitia mtandaoni kwamba amegundua msanii huyo amekuwa na mabadiliko makubwa tangu afunge ndoa rasmi na mkewe.

Kupitia jukwaa la X, Davido alichapisha ujumbe kwamba anaipenda sana familia yake kwa maana ya mkewe Chioma Rowland.

Shabiki huyo, kama wengi tu alifika na kuweka wazi yaliyo moyoni mwake akisema kwamba Davido amebadilika sana tangu afunge harusi miezi michache iliyopita.

Kwenye jukwaa la microblogging X, mwimbaji alionyesha upendo mkubwa kwa familia yake. Aliandika: “Naipenda familia yangu ….❤️”

@Magik_jay_ aliandika: “Tunaona , tangu uoe rasmi unakuja kwa njia tofauti”

Davido alijibu: "Tunajaribu kufanya vizuri zaidi .... ❤️”

Itakumbukwa kuwa Davido na mkewe, Chioma walifanya harusi yao tarehe 25 mwezi wa Juni na hafla hiyo ilihudhuriwa na mastaa wakubwa.

Wageni wengi walikuwa wamemzawadia mamilioni ya pesa ttaslimu kwa sarafu ya naira na fedha za kigeni.

Video ambayo inavuma iliyotumwa na mwanablogu Tunde Ednut inaonyesha wakati Davido alionekana aaktupiwa usoni burunguti la noti za dola wakati akitumbuiza kwenye harusi yake.

Davido alienda kwenye sehemu ya maoni katika video hiyo na kutoa maoni hayo akisema kuwa pesa alizonyunyiziwa kwenye video za harusi hazilingani na kiasi walichopeleka nyumbani