Jackie Matubia afurahia baada ya bintiye wa pili kuanza shule

“Nilihisi kana kwamba sehemu ya roho yangu imebaki, nilijawa na hisia, kumlea mtoto peke yako mpaka kufikia hatua hii ya kuenda shule ni ushindi wa kipekee.,"Matubia alisema.

Muhtasari

• Matubia akuweza kuzuia furaha yake kupitia mtandao wa Instagram ambapo alichapisha msururu wa picha na video za siku ya kwanza kwa Zendaya shuleni.

JACKIE MATUBIA NA ZENDAYA.
JACKIE MATUBIA NA ZENDAYA.
Image: INSTaGRAM

Muigizaji Jackie Matubia ni mama mwenye furaha baada ya binti yake mzaliwa wa pili, Zendaya kuanza maisha mapya kama mwanafunzi.

Matubia akuweza kuzuia furaha yake kupitia mtandao wa Instagram ambapo alichapisha msururu wa picha na video za siku ya kwanza kwa Zendaya shuleni.

“Zendaya alikuwa na furaha kusema kweli, hakuna kulia, na hajali chochote kama kawaida na kuweza kuangalia nyuma pia, hivyo ndivyo tuliondoka tukamuacha shuleni,” Matubia aqlisimulia.

Baada ya kumuacha shuleni kwa mara ya kwanza, Matubia alisema kwamba alikuwa na hisia mseto, kwa wakati Fulani akihisi kwamba sehemu ya moyo wake imebaki mbali naye.

“Nilihisi kana kwamba sehemu ya roho yangu imebaki, nilijawa na hisia, kumlea mtoto peke yako mpaka kufikia hatua hii ya kuenda shule ni ushindi wa kipekee. Yote ambayo ninaweza sema ni kwamba Mungu alifanikisha na atazidi kufanikisha,” aliongeza huku akionekana kutupa dongo kwa aliyekuwa mpenzi wake, Blessing Lung’aho.

Itakumbukwa Matubia na Blessing Lung’aho waliingia kwenye mapenzi baada ya kukutana kwenye kipindi maarufu cha Zora kwenye runinga ya Citizen.

Baada ya kipindi hicho kukamilika, wapenzi hao walioana na kubarikiwa na binti Zendaya.

Hata hivyo, mapenzi yao yaliisha kimya kimya miezi kadhaa baadae, huku Matubia akionekana kumlenga kwa mishale Lung’aho kwamba hajawahi kumsaidia katika malezi ya binti yake.

Kwa upande wake, Lung’aho hajawahi zungumzia suala hilo na ameonekana kujikita katika mambo yake.