Nilikuwa napata Sh200 kwa siku kabla ya umaarufu- Stevo Simple Boy afichua kazi ya awali

“Kwa usanii inategemea lakini kwa siku nawezapata Ksh. 20,000 na pengine utapata ni mara moja kwa mwezi,” Simple Boy alisema.

Muhtasari

•Msanii Stevo Simple Boy asema kuwa alikuwa akipata Ksh.200 katika eneo la ujenzi (mjengo) kabla ya kupata umaarufu

•Kwa sasa analipwa Ksh.20,000 kutoka kwa muziki ambayo huwa ni mara moja kwa siku ama mwezi

Stevo Simple Boy
Stevo Simple Boy
Image: Stevo Simple Boy8//Facebook

Msanii Stevo Simple Boy amesema kuwa alikuwa akipata Ksh.200 katika eneo la ujenzi (mjengo) kabla ya kupata umaarufu.

Katika mahojiano na YouTuber 2mbili, Simple Boy alisema alikuwa akifanya kazi katika eneo la ujenzi kwa sababu maisha hayakuwa rahisi kwake.

Nilikuwa nalipwa Ksh.200 kwa siku,"alisema. Lakini sahii watu wa mjengo wanalipwa Ksh.650 kwa siku.

Hata hivyo alisema kuwa ijapo usanii ikakataa, yeye  hataki kurudi kufanya mjengo na atatafuta kitu kingine cha kufanya.

Vile sahii mimi ni msanii mkubwa na vile watu wangu wa Kenya wananipenda, wakenya wanatumaini kwangu sana kwa hivyo mjengo siwezi rudi,” Stevo alisema.

Simple Boy alisema kuwa alifanya kazi huko kwa mwaka moja  ambapo alikuwa akisafirisha vifaa vya ujenzi kama vile simiti na alikuwa mtu wa mkono.

Pia alifichua kuwa sasa anatengeneza Ksh.20,000 kwa siku au zaidi kutoka kwa usanii.

“Inategemea, kwa siku nawezapata Ksh. 20,000 na hiyo ni mara moja na pia kwa mwezi. Inategemea na event,”

Anawashauri wale ambao wanachagua kazi kuwa wafanye kazi yoyote na wasichague bora tu wasiibe.

Kazi si kazi bora unapata maokoto (pesa) yako kidogo kuliko kuiba. Kazi ni kazi,usibague kazi si lazima uandikwe kazi kwa ofisi ndio upate maokoto. Unaweza andikwa kazi ama ufanye biashara yako wewe mwenyewe,”

Simple Boy alisema kuwa  hakuwa anapenda kubeba simiti alipokuwa akifanya kazi kwa mjengo.

Alikiri kuwa hali ngumu ya maisha ndiyo ilimfanya akaingia kufanya kazi ya mjengo.