Huddah Monroe amwomba radhi Peter Salasya

MP Peter Salasya amekuwa akimchumbia mwanashoshalaiti huyo kwa muda sasa.

Muhtasari

• MP Peter Salasya amekuwa akimchumbia mwanashoshalaiti Huddah Monroe kabla ya mwanasiasa huyo kusema kuwa amechoka katika kuendelea kumchumbia Huddah.

• Licha ya ugomvi huo Huddah amekiri  bado anampenda Salasya na kuwa ana heshima sana kwake.

HUDDAH NA SALASYA
HUDDAH NA SALASYA
Image: HISANI

Mwanashoshalaiti Huddah Monroe ameomba radhi kwa mbunge wa Mumias mashariki Peter Salasya baada ya majibizano makali katika mtandao wa Instagram,

Huddah amesema kuwa bado ana heshima na mapenzi ya dhati kwa mheshimiwa huyo anayehudumu muhula wake wa kwanza katika bunge la kitaifa.

"Nakuheshimu sana Peter Salasya na naomba radhi kwa kukushambulia . Tuonane hapo juu, Ubarikiwe."  Aliandika Huddah Monroe.

Awali mbunge Salasya alikuwa amemjibu mwanashoshalaiti huyo kutokana na mashambulizi yake kwake.

Salasya alijitetea kuwa Huddah alihariri ujumbe wa mpesa kuonyesha kuwa alipokea shilingi milioni 2 ilhali nchini Kenya kiwango cha juu zaidi cha hela zinazotumwa kupitia njia ya mpesa ni laki tano.

Kulingana na Salasya, Huddah hana hela na alikuwa anamwomba kila siku kupitia jumbe za Whatsapp hadi atakmtumia (Salasya) namba yake ya Kenya.

Aidha Huddah Monroe amesema kuwa hajawai kutana na Peter Salasya na kuwa walijuana kupitia mtandao wa Instagram na hapo ndipo itakamilikia.

Hata hivyo, Huddah Monroe ameonyesha kumjali sana Peter Salasya kupitia ujumbe alioandika kwenye matukio ya Instagram.

"Sina kinyongo nawe, bado nina heshima kubwa na upendo mwingi  kwako.Wewe ni mtu mkubwa. Jitunze."  Aliandika Huddah.