Peter Salasya amuomba Andrew Kibe msamaha kwa kutofuata ushauri wake

“Lakini mimi nilikuwa nataka kubadilisha maisha ya huyu msichana mdogo. Hata nilikuwa nimejitolea ku’market bidhaa zake. Tukasema niende ninunue hata kwa wingi ili nije nigawe kwa wasichana wengine"

Muhtasari

• Hata hivyo, Salasya alinyoosha maelezo kuhusu nia yake kwa Huddah, akisema kuwa hakuwa anamtaka kimapenzi bali alikuwa anataka kuunga mkono biashara yake.

SALASYA NA KIBE
SALASYA NA KIBE
Image: HISANI

Mbunge Peter Salasya amenyenyekea na kuomba msamaha kwa YouTuber Andrew Kibe kwa kile alichokitaja kama ni kutosikiliza ushauri wake wakati alianza kuonyesha nia ya kumfukuzia mwanasosholaiti Huddah Monroe kimapenzi.

Kupitia ukurasa wake wa YouTube, Salasya alimuita Kibe kama mkubwa wake na kusikitika kuhusu kupuuza ushauri wake kumhusu mwanasosholaiti Huddah Monroe, siku moja baada ya mbio zake za kumfukizia mrembo huyo kufika ukingoni.

“Mzee Kibe, nakuheshimu Andrew Kibe. Ninaomba msamaha na sasa kuanzia leo, mzee Andrew Kibe nakuheshimu zaidi ya maelezo na wewe sasa ni mkubwa wangu,” Salasya alisema.

Hata hivyo, Salasya alinyoosha maelezo kuhusu nia yake kwa Huddah, akisema kuwa hakuwa anamtaka kimapenzi bali alikuwa anataka kuunga mkono biashara yake.

“Lakini mimi nilikuwa nataka kubadilisha maisha ya huyu msichana mdogo. Hata nilikuwa nimejitolea ku’market bidhaa zake. Tukasema niende ninunue hata kwa wingi ili nije nigawe kwa wasichana wengine. Kwa sababu napenda sana kubadilisha maisha ya watu,” Salasya alieleza.

Salasya alijipiga kifua kwamba yeye ndiye kiongozi ambaye anahisi ana utofauti mkubwa kutoka kwa viongozi wengine, kwani hachagui wala kubagua mtu anayetangamana naye.

“Mimi hapa Kenya ndiye kiongozi ambaye ako tofauti na wengine, kiongozi anayetaka kutangamana na kila mtu. Mimi nimewahi kuwa pasta kwa watoto wa mitaani mjini Nakuru. Mimi nimezungukwa na watu wengi, lakini najua kwa sababu sisi wote ni binadamu, nilifungia macho mambo mengi ili kumleta kwenye uwepo wa mitandaoni,” Salasya alisema.

“Mimi nilikuwa naweka airtime na tunazungumza kwa hata zaidi ya saa nzima nikimpa ushauri rudi nyumbani kwa sababu hakuna kitu anafanya huko nje,’ aliongeza.