Bradley Mtall anatafuta walinzi wawili wa kike

“Ninatazamia kuajiri walinzi wawili wa kike wenye ujuzi na uzoefu kwa ajili ya usalama wa kibinafsi," alisema.

Muhtasari

•Bradley Mtall amesema kuwa anataka kuajiri walinzi wawili wa kike ambao wana ujuzi kwa ajili ya usalama wake wa kibinafsi.

•Bradley kwa sasa yuko jijini Mombasa siku chache baada ya kumtembelea mamake.

Bradley Mtall
Bradley Mtall
Image: Bradley Mtall Genz Goliath//Facebook

Bradley Mtall amesema kuwa anataka kuajiri walinzi wawili wa kike ambao wana ujuzi kwa ajili ya usalama wake wa kibinafsi.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, amechapisha kuwa anataka kuajiri walinzi wawili wa kike na ambao wana ujuzi kwa ajili ya usalama wa kibinafsi.

“Ninatazamia kuajiri walinzi wawili wa kike wenye ujuzi na uzoefu kwa ajili ya usalama wa kibinafsi.”

Pia ameongeza  ikiwa  kuna kampuni ambayo inatoa huduma hizo, wamfikie na maelezo.

Ikiwa kampuni yako hutoa huduma hizo, tafadhali tufikie na maelezo. Asante,” aliandika.

Bradley kwa sasa yuko jijini Mombasa siku chache baada ya kumtembelea mamake.

Jumamosi Bradley alimtembelea mama yake eneo la Chavakali kaunti ya Vihiga pamoja na wasimamizi wake kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.

Bradley alionekana kuwa na furaha kuungana na mama yake kwa mara ya kwanza tangu apate umaarufu.

Kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, alichapisha video iliyoonyesha akimkumbatia mamake kwa furaha baada ya kuwasili nyumbani. Mamake alionekana kujawa na furaha na kumkaribisha mwanawe nyumbani.

"Nilisafiri zaidi ya kilomita 378 kukutana na mama yangu," aliandika.

Ziara ya Bradley kuenda Vihiga ilijiri wiki chache baada ya mamake kulalamika kuwa hajakuwa akienda nyumbani wala kushika simu zake baada ya yeye kuwa maarufu.