Sina muda wake, sasa ni wakati wa kazi – Salasya kuhusu msamaha wa Huddah

“Ni wakati wa kazi sasa. Mimi ni mwendawazimu mwenye napenda utata na huwa sijali sana zaidi yangu na eneo bunge langu mengine ni hekaya za abunuwasi," Salasya asema.

Muhtasari

•Mbunge wa Mumias mashariki Peter Salasya anamwambia mwanasosholaiti Huddah Monroe aende akaimbe na kudensi na wasanii na yeye mwenyewe aende apige siasa.

HUDDAH NA SALASYA
HUDDAH NA SALASYA
Image: HISANI

Mbunge wa Mumias mashariki Peter Salasya anamwambia mwanasosholaiti Huddah Monroe aende akaimbe na kudensi na wasanii na yeye mwenyewe aende apige siasa.

"Mtu amfikishie taarifa huyo mwanamke mimi sina muda kwa upuzi wake, sasa aende aimbe wimbo na kudance na wasanii na kuchukuwa pesa kwa watu wenye wana pesa yenye haina kazi mimi nipige siasa hiyo ndio kazi ninayoweza,” Salasya aliandika.

Pia aliongeza kuwa yeye hajali mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe na eneo bunge yake.

“Ni wakati wa kazi sasa. Mimi ni mwendawazimu mwenye napenda utata na huwa sijali sana zaidi yangu na eneo bunge langu mengine ni hekaya za abunuwasi," Mbunge huyo mcheshi aliongeza.

Majibu haya ya Salasya alijiri baada ya Huddah kuandika kwa insatory zake kuwa bado anamheshimu mbunge huyo na kwamba akubali kukataliwa kwani ni hali ya maisha.

“Sina nia mbaya dhidi yako. Bado nina heshima kubwa kwako na upendo mwingi. Wewe ni mwanamume mzuri. Jitunze." Huddah aliandika.

Hata hivyo, Salasya katika video kupitia chaneli yake ya YouTube alibadili nia na kusema lengo lake kwa Huddah halikulenga mapenzi bali kuipa biashara yake ya bidhaa za urembo sapoti.

“Lakini mimi nilikuwa nataka kubadilisha maisha ya huyu msichana mdogo. Hata nilikuwa nimejitolea ku’market bidhaa zake. Tukasema niende ninunue hata kwa wingi ili nije nigawe kwa wasichana wengine. Kwa sababu napenda sana kubadilisha maisha ya watu,” Salasya alieleza.

Salasya alijipiga kifua kwamba yeye ndiye kiongozi ambaye anahisi ana utofauti mkubwa kutoka kwa viongozi wengine, kwani hachagui wala kubagua mtu anayetangamana naye.

Mimi hapa Kenya ndiye kiongozi ambaye ako tofauti na wengine, kiongozi anayetaka kutangamana na kila mtu. Mimi nimewahi kuwa pasta kwa watoto wa mitaani mjini Nakuru. Mimi nimezungukwa na watu wengi, lakini najua kwa sababu sisi wote ni binadamu, nilifungia macho mambo mengi ili kumleta kwenye uwepo wa mitandaoni,” Salasya alisema.

"Mimi nilikuwa naweka airtime na tunazungumza kwa hata zaidi ya saa nzima nikimpa ushauri rudi nyumbani kwa sababu hakuna kitu anafanya huko nje,’ aliongeza.