“Nakupenda juu wewe ni mchapakazi, njoo tuchape kazi pamoja” Simple Boy kwa Charlene Ruto

Sasa inasubiriwa kuonekana kama binti wa kwanza wa taifa ataitikia ombi laq Stevo na kufanya kaiz pamoja, japo msanii huyo hakuweza wazi ni kazi gani anataka wachape pamoja na Charlene.

Muhtasari

• Rapa huyo mcheshi aliendelea kumtaka Charlene kuutangaza wimbo wake mpya unaoitwa ‘Mafi Mafi Mushkila’ neno la Kiarabu ambalo linamaanisha hakuna tatizo.

 
• “Niko na ngoma mpya inaitwa mafi mafi mushkila hebu support na ushare iyo ngoma alafu tutaongea,” aliongeza.

 

STEVO NA CHARLENE
STEVO NA CHARLENE
Image: HISANI

Rapa mzawa wa Kibera Stephen Otieno Adera almaarufu Stevo Simple Boy ametoa wito kwa binti wa kwanza wa taifa, Charlene Ruto akimuomba kukubali kufanya kazi na yeye.

Kijana huyo anayejiita ‘Sauti ya wanyonge’ alichapisha video kwenye Instagram akikiri kwamba anampenda Charlene Ruto kutokana na jitihada zake katika kuchapa kazi, akifichua kuwa naha aliweka nywele kama yeye.

Alimuomba Charlene Ruto kukubali ombi lake kwa kuwa pia yeye ni mchapakazi, hivyo pamoja wataunganisha nguvu katika kuchapa kazi hadi kieleweke.

“Charlene Ruto ni mwanadada ambaye anachapa kazi. Charlene Ruto hata mimi ni mwanamume wa kuchapa kazi njoo madam tufanye kazi pamoja,” Stevo Simple alisema.

Rapa huyo mcheshi aliendelea kumtaka Charlene kuutangaza wimbo wake mpya unaoitwa ‘Mafi Mafi Mushkila’ neno la Kiarabu ambalo linamaanisha hakuna tatizo.

“Niko na ngoma mpya inaitwa mafi mafi mushkila hebu support na ushare iyo ngoma alafu tutaongea,” aliongeza.

Alhamisi, Stevo Simple Boy alichapisha wimbo huo kupitia YouTube yake akifafanua zaidi kuhusu maana halisi na kauli hiyo ya Kiarabu.

Awali, alikuwa amekiri kwamba kauli hiyo ilimshindia ziara ya kikazi kuelekea nchini Saudi Arabia mwezi ujao ambapo atakuwa anatumbuiza.

“Kwa nini mimi kila mara ninabadilisha muonekano wa nywele, mavazi na pia misamiati? Unajua mimi ni msanii si Kenya peke yake, ni Afrika Mashariki nzima lakini sasa nataka kutanua mbawa zaidi niende kimataifa,” Stevo alifafanua.

Sasa inasubiriwa kuonekana kama binti wa kwanza wa taifa ataitikia ombi laq Stevo na kufanya kaiz pamoja, japo msanii huyo hakuweza wazi ni kazi gani anataka wachape pamoja na Charlene.