
Mcheshi na mwanaharakati maarufu Erick Omondi amemnunulia bi Faith Kathambi kipande cha aridhi mjini Nairobi na kuanzisha ujenzi wa nyumba ya kisasa katika ploti hiyo
Erick Omondi amedokeza kuwa atajitosa katika uanaharakati kama njiamojawapo ya kupigania haki za wanyonge na wasiojiweza,akitembea sako kwa bako na Kathambi wakizuru nyumba aliojengewa bi kathambi ambayo i karibu kutamatika.
Erick akielezea hisia zake jinsi alivyo muona bi Kathambi ambaye licha ya kuwa kabwela pia ni kiziwi kwa kuzingatia hali hiyo tata ya kimaumbile ya bi Kathambi alimuonea huruma na kuhisi kama binadamu yeyote yule kilikuwa ni kitendo cha uhayawani na mateso bila huruma kwa binadamu.
Jambo kama hilo lilimfanya mwanamitindo Erick kuguswa na kushikwa na hisia za utu na kuamua kuwarai mashabiki wake mtandaoni wamusaidie kuchanga hela kwa minajili ya kumuauni mwanadada huyo kufikia januari 18,2025 walikuwa wamechanga kitita cha shilingi 87,6000.
Akielezea maazimio ya bi Kathambi Erick alisema kwa sasa ana mpango mpana wa kuhakikisha kuwa Bi Kathambi anaanzisha biashara ya dukakuu yaani supermarket,amnunulie na amfae kwa boma zuri na ahakikishe kuwa bi Thambi anarejelea masomo yake baada ya kuyakatiza kwa muda.
Kulingana na azima ya Erick Omondi analenga kuchangisha shilingi milioni tatu 3m kwa manufaa na faida ya bi Kathambi,akilenga kutimiza hayo, mwanamke mmoja kutoka nairobi kwa jina Cate alitoa msaada wa vyombo vya samani kwa ajili ya nyumba ya Kathambi.
Itakumbukwa wazi kuwa bi Kathambi alipigwa kitutu akiwa nyumbani kwao maeneo ya Kisii kwa kukosa pesa za kulipia unga wa pakiti ya ugali jambo ambalo lilimsababishia majeraha mengi mwilini huku akirekodi taarifa katika kituo cha polisi kilichokuwa karibu naye.
Hicho kitendo cha unyama kilikemewa vikali na wakenya wa matabaka mbalimbali wakiwemo watumizi wa mitandao ya kijamii kwa kulaani tukio hilo la kinyama,vilevile wito ulitolewa kwa wananchi kuwa na moyo wa utu kila mara na kutochukua sheria mikononi mwao kuwapo na hali ya sintofahamu bali wafuate sheria na kuwa na nyoyo za utu kila uchao na kuimarisha umoja na utangamano.