Muigizaji maarufu Wema ISepetu ameonesha kukerwa na baadhi ya waislamu wenzake hasa wale wanaotumia mitandao ya kijamii ambao hawakufurahishwa na kitendo chake cha kumutakia mpenziwe heri njema ya kuzaliwa.
Wema Sepetu ambaye aliwajibu kupitia njia ya Vdeo amesisitiza kwamba hajawahi kuona kwamba kumutakia mtu heri njema ya kuzaliwa ni kosa wakati wa mfungo wa Ramadhani.
"Yote tisa waislamu wa mitandaoni tutashindwa kuishi maisha yetu walahi. Kwa hivyo hata mtu akimutakia mwingine heri njema ya kuzaliwa ni makosa. Tunaambiwa Ramadhani iko, kwani Ramadhani ikiwa Hakuna kuwishi mtu Happy Birthday. Mbona maajabu. Mimi sijawahi kuona au labda mimi ndio sijui. Msifanye ivyo mnakosea,"alisema muigizaji Wema Sepetu.
Mwanadada huyo pia amefunguka kwamba hangependa mtu kuingilia mapenzi yake na mpenziwe hii ni baada ya fununu kuenea kwamba mama yake mzazi hampendi kabisa mpeniziwe Whozu ambaye ni mwanamziki kutoka katika taifa hilo la Tanzania.
Amesisitiza kwamba mahusiano hayo hayafai kuingiliwa na mtu yeyote maana ni yake na hakuna mtu ambaye anafaa kumchagulia mtu wa kupenda.
'"Mimi nasema kwamba maisha yangu mimi ya mapenzi hayamuhusu mtu yeyote hata wewe. Yananihusu mimi na mpenzi wangu. Hayatakiwi kumuhusu mtu yeyote mwingine hata kama hapendi, bora mimi na mpenzi wangu tuko sawa. sijui kama niko sahihi au hapana. Ninachojua ni kwamba mama hana shida, yuko sawa lakini hili linakwenda kwa mutu yeyote huko inje," aliweka wazi Sepetu.
Muigizaji huyo maarufu na mshindi wa tuzo ya miss Tanzania pia amefunguka kwamba yeye anamzidi Mpenziwe Whozu kwa umri wa miaka sita na wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka minne kufikia sasa.
'Namuzidi na mika sita, nimemzidi Whozu na miaka sita na mimi naona siyo mibaya sana, hata kama ingekuwa 10 kwani shda iko wapi, kuna watu wanashindaniana miaka 20 sembuse mimi miaka sita. Huu mwaka wa nne wa 'mapenzi' na tupo.," alikiri.
Mwanadada huyo pia alifichua kwamba hana hamu sana na ndoa. "Ndoa sio kitu ambacho mimi nakiona au nakiota, na sio kitu ambacho labda nakitamani. Nadhani imeniharibu kimawazo hasa kutokana na watu wangu wa karibu," aliweka wazi.