Harmonize aachia kibao cha bangi na Konshens baada ya kutangaza ada ya 5M kwa collabo (+video)

Harmonize alitangaza kuwa ataanza kutoza Tsh100M ili kufanya collabo.

Muhtasari

•Mastaa hao wanazungumzia bangi na kuangazia majina tofauti ambayo mataifa mbalimbali yanaita dawa hiyo ambayo ni haramu Afrika Mashariki.

•"Naanza kutoza kwa collabo, TZS 100M. Sharti ngoma iwe kali. Siwezi kusubiri kumtoza mtu fulani TZS 500," Harmonize alisema.

Staa wa Bongo Harmonize ameachia kibao kipya 'Weed Language' ambacho amemshirikisha mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamaica, Konshens.

Katika wimbo huo mpya ambao ulitolewa Alhamisi usiku, mastaa hao wawili wa muziki wanazungumzia bangi na kuangazia majina tofauti ambayo mataifa mbalimbali yanaita dawa hiyo ambayo ni haramu Afrika Mashariki.

“Unaitaje bangi kwa lugha yako,” anasema Harmonize kwenye ubeti wake wa wimbo huo.

Katika ubeti wake, Konshens anaimba kuhusu jinsi wanavyoita bangi katika nchi yake ya Jamaica na kuhusu mapenzi yake kwa mihadarati hiyo.

Kibao hicho kiliachiwa masaa machache baada ya  Konde Boy kuahidi kuachia wimbo unaohusu bangi kabla ya mwisho wa mwezi wa Disemba.

"Disemba hii, nisipotengeneza wimbo kuhusu bangi .. nipigeni risasi," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na emoji ya kikohozi, ambacho huwa anatumia kama utambulisho wake katika nyimbo zake nyingi. Kikohozi pia huhusishwa na matumizi ya bangi kwani watumizi wengi hujipata wakikohoa baada ya kuvuta.

Harmonize kwa kawaida huwa hafichi kwamba yeye ni mtumizi wa mihadarati hiyo. Katika video za nyimbo zake nyingi ameonekana akivuta kinachoaminika kuwa bangi. Pia amewahi kurekodi video zingine nyingi akivuta.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide pia alitangaza kuwa ataanza kutoza Tsh 100M (Ksh 5M) ili kufanya  collabo na wasanii wengine.

Harmonize alitangaza kuwa ataanza kutoza Tsh100M ili kufanya  collabo na wasanii wengine.

Mapema mwaka huu, Harmonize alidokeza kuhusu mpango wa kuanzisha Brand ya sigara. Staa huyo aliwaomba mabwenyenye wa Tanzania kujitolea kushirikiana naye kufanikisha ndoto ya kuanzisha kampuni ya kutengeneza bidhaa hiyo.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alifichua kuwa bidhaa yake itatambulika kama sigara ya Tembo.