Hisia nzuri Winnie Odinga akikutana na kufanya wimbo na rapa 'pacha' wake, Breeder LW anayefanana naye sana (+video)

Wawili hao walipata kutengeneza wimbo wa freestyle pamoja wakiwa wamekaa kwenye gari..

Muhtasari

•Wawili hao walikutana siku ya Ijumaa na wakaonyesha baadhi ya picha na video za mkutano wao ambao ulionekana kuwa mzuri sana.

•Wawili hao walisikika wakitema mistari ya mashairi kiubunifu na ustadi wao ulionekana kuwashangazai wengi.

Image: TWITTER// BREEDER LW

Binti wa kinara wa ODM Raila Odinga, Winnie Odinga alifurahi sana kukutana na rapa wa Kenya Paul Baraka almaarufu Breeder LW ambaye mara nyingi imesemekana anafanana naye.

Wawili hao walikutana siku ya Ijumaa na wakaonyesha baadhi ya picha na video za mkutano wao ambao ulionekana kuwa mzuri sana.

Pia walipata kutengeneza wimbo wa freestyle pamoja wakiwa wamekaa kwenye gari.

“Freestlye Friday na pacha wangu #bigbabafridays,” Winnie Odinga aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha na video yake na rapa huyo mzaliwa wa jiji la Nairobi wakishiriki wakati mzuri pamoja.

Breeder pia alielezea furaha yake baada ya kukutana na binti huyo wa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga. Pia alionekana kupenda ujuzi wa Winnie wa kurap ulioonyeshwa katika wimbo wa freestyle ambao walitengeneza pamoja wakati wa mkutano wao.

“Wangwan Mhesh @realwinnieodinga #bigbaba. BIG BABA X WINNIE ODINGA FREESTYLE. Hii ni Bonasi ya Ijumaa hii! Mmeskia vile Winnie anatema? Noma sana,” Breeder aliandika..

Katika video waliyoshiriki, wawili hao walisikika wakitema mistari ya mashairi kiubunifu na ustadi wao ulionekana kuwashangaza watumiaji wengi wa mtandao.

Wanamitandao wengi waliojibu machapisho yao pia hawakukosa kutambua kufanana kwao huku baadhi yao wakidai kuwa wanafanana na mapacha.

Tazama baadhi ya maoni chini ya chapisho la Breeder:

@mulamwah big baba.. you look again.

@Kaysparks Wewe ni mgani? Next time mark  yourself tukujue wewe ndio mgano, ama hata uchukue mkono juu.

@Lema Bro yako anakufanana siet.

@Ngafocus Which is which?

@Iconic_Kemboi Haha.. haungekuwa umevaa hiyo Tshirt ya white I swear ningekuconfuse na Winnie.

Kwa muda mrefu, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakimliwafananisha rapa Breeder LW na Winnie Odinga na kudai kuwa wanafanana sana. Baadhi yao mara nyingi wamesema kwamba wanaonekana kama mapacha.