Ringtone aeleza kwa nini Diana Marua anamfaa Bahati

“Mimi siku nitapata dem kama Diana kwa Maisha yangu, nitampenda kabisa ju mimi kupenda sio rahisi,” Ringtone alisema

Muhtasari

•Ringtone alisema ikiwa atakutana na mwanamke kama Diana Marua, basi atamthamini sana mwanamke huyo na kufanikiwa zaidi maishani.

•Kulingana na Ringtone, Bahati alifanikiwa kuwa na Diana kwa sababu anamsaidia Bahati kuwa kwenye ubora wake.

Ringtone, Bahati na Daina
Image: instagram

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ameangazia sababu iliyomfanya msanii wa Kenya Bahati kuwa na rapa Diana Maruakama mke wake.

Kulingana na Ringtone, Bahati alifanikiwa kuwa na Diana kwa sababu anamsaidia Bahati kuwa kwenye ubora wake.

Ringtone alisema ikiwa Diana angeondolewa kwenye maisha ya Bahati, Bahati hangekuwa mahali alipo akisema hata wasanii wa chini kabisa wangemzidi.

“The biggest blessing, Bahati, alishai kupata maishani si kupata mali ya dunia, ni kupata Diana juu wa kiachana hata Stevo Simple Boy atapita Bahati.” Ringtone alisema.

Ringtone aliendelea kukiri kwamba wawili hao ni wanandoa wenye nguvu sana ambao wanaweza kufikia chochote ikiwa wataweka akili zao kwa pamoja.

 "Wakiwa hivyo tu collabo pamoja wako top," alisema.

 Ringtone aliongezea ikiwa pia atapata kukutana na mwanamke kama Diana Marua, basi atamthamini sana mwanamke huyo na kufanikiwa zaidi maishani.

 Pia aliongezea kuwa ndoa ya Bahati na Diana humfanya kuwa na wivu wakati mwingine.

“Mimi siku nitapata dem kama Diana kwa Maisha yangu, nitampenda kabisa ju mimi kupenda sio rahisi, Ringtone alisema

Wanamuziki Kevin Bahati na Diana Marua ni miongoni mwa wanandoa wachache waliosherehekewa zaidi nchini na kwa sababu ya jinsi wanavyofanya mengi pamoja, kuanzia kuimba pamoja hadi kufanya maudhui pamoja.

Hivi majuzi walitangaza onyesho lao la kwanza ‘The Bahati’s empire’ kwenye mtandao wa Netflix.