Wasanii wa Nigeria wametuteka hadi vijijini! Omondi alalamika kuhusu shoo ya Ruger huko Meru

Ruger anatarajiwa kutumbuiza Meru wikendi hii

Muhtasari

• Omondi ameweka hisia zake mtandaoni Instagram na kusema kuwa wanamuziki wa nchi nyingine wameteka wananchi wa Kenya kuliko wasanii wa Kenya.

• "Unadhani mwanamuziki wa Kenya anaweza kuenda Nigeria na kuwa na hafla vijijini? Yaani sasa wanawatumbuiza Wakenya hadi vijijini? " alisema.

Eric Omondi// Ruger

Mchekeshaji Eric Omondi amewakashifu wasanii Wakenya kwa mara nyingine kwa kudorora kwenye sekta ya muziki.

Akizungumza kupitia Instagram, Omondi alisema kuwa wasanii wa nchi zingine wameteka wananchi wa Kenya kuliko wale wa Kenya. Alisema kuwa wanamuziki wa mataifa mengine  haswa wale kutoka Nigeria wamekuja nchini na kupafanya kwao kwa kuwatumbuiza Wakenya wanavyotaka.

Hii ni baada ya msanii wa Nigeria, Ruger, kuja Kenya kwa ajili ya tamasha la Walker Festival ambalo limeratibiwa kufanyika Jumamosi katika uwanja wa Kinoru, kaunti ya Meru.

"Unadhani mwanamuziki wa Kenya anaweza kuenda Nigeria na kuwa na hafla vijijini? Yaani sasa wanawatumbuiza Wakenya hadi vijijini? " alihoji.

Omondi amesema kuwa wasanii wa Kenya wamezoea kuwakaribisha wasanii wa mataifa mengine na hata kuwafungulia shoo.

"Na sisi bado tutacurtain raise tu, hivi karibuni utasikia Konshens ako Budalangi akiwatumbuiza Wakenya," alisema.

Mtunzi huyo wa kibao  'girlfriend' aliwasili nchini Kenya Jumanne ili kufanya matayarisho ya hafla yake itakayokuwa  Meru .

Omondi amekuwa akiwapa wasanii Wakenya msomo huku akiwaambia kuwa wanamfanyisha kazi ya punda na baadae kumpiga mateke.

Katika orodha ya nyimbo bora 100 ya Appple Music,  nyimbo mbili pekee za Kenya zilihitimu huku Nigeria ikitoa nyimbo 80.

Omondi aliwahimiza wanamuziki kusikiliza ushauri wake ili waweze kufika kiwango cha juu na kutambulika kwenye nchi nyingine.