"Mmeona chochote?" Mammito aaibika baada ya zipu ya suruali kuwa wazi akiwa jukwaani

"Poleni jamani. Wah! mmeona. Je, mmeona chochote?," aliwauliza wasikilizaji.

Muhtasari

•Mammito alipatwa na kipindi cha aibu jukwaani wakati wa moja ya shoo za vichekesho siku chache zilizopita.

•"Hiyo ilikuwa aibu. Nini? Ni vizuri umeniambia (Wanda) nimefanya hivyo," alisema.

Image: INSTAGRAM// MAMMITO

Mchekeshaji Eunice Mammito alipatwa na kipindi cha aibu jukwaani wakati wa moja ya shoo za vichekesho siku chache zilizopita.

Mamitto alikuwa akitumbuiza kwenye jukwaa wakati mmoja wa wachekeshaji wenzake, Justice Wanda, alipogundua kuwa zipu ya suruali yake ilikuwa chini na akapanda hadi pale  jukwaani kumjulisha mbele ya hadhira yake.

Wanda alionekana akinong'ona maneno yasiyosikika kwenye sikio la mchekeshaji huyo wa Churchill Show ambaye mara moja aliinama kidogo ili kuvuta zipu yake juu huku aibu kubwa ikiwa imeandikwa usoni mwake.

"Poleni jamani. Wah! mmeona. Je, mmeona chochote?," aliwauliza wasikilizaji wake ambao walisikika wakicheka kwa nguvu.

Baadaye  alionekana kufarijika na akajiunga na mashabiki kwa kicheko baada ya kushawishika kuwa hawakuona chochote.

"Hiyo ilikuwa aibu. Nini? Ni vizuri umeniambia (Wanda) nimefanya hivyo," alisema.

Mchekeshaji huyo alitania kwamba wanaume walikuwa wakimtazama sana kwa sababu zipu yake ilikuwa chini.

"Jamani mlifurahi sana. Ndio maana wanaume walikuwa wakinitazama hivyo, nilikuwa najiuliza kuna nini? Nyote hamwezi kuwa mnatabasamu hivyo," alisema.

Zaidi, alifanya utani kwamba alikuwa ametoka kwenye kipindi kifupi cha mapenzi.

Tazama video:-