Njugush afichua kwanini alimpa mkewe jina la utani 'Wakavinye'

Kulingana na Njugush, mkewe alikuwa akimiliki Vitz, katika siku za nyuma.

Muhtasari

•Njugush kwa mara ya kwanza amefichua mahali ambapo mkewe Celestine Ndinda alipata jina la utani la Wakavinye.

•Njugush pia alimsifu mke wake kwa mafanikio yake na kuongeza kuwa hataacha kufanya kazi na yeye.

Njugush na mkewe Wakavinye
Image: INSTAGRAM// CELESTINE NDINDA

Mchekeshaji wa Kenya Timothy Kimani almaarufu Njugush kwa mara ya kwanza amefichua mahali ambapo mkewe Celestine Ndinda alipata jina la utani la Wakavinye.

Kulingana na Njugush, mkewe alikuwa akimiliki Vitz, katika siku za nyuma.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Mwende Macharia aliema;

"Cele alikuwa anamiliki Vitz kwa hiyo ningeiita Kavinye, Ndivyo nilivyoishia kumuita Wakavinye (Mmiliki wa kavinye {Vitz})"

Njugush pia alimsifu mke wake kwa mafanikio yake na kuongeza kuwa hataacha kufanya kazi na yeye licha ya baadhi ya watu kumshauri dhidi ya hilo.

Alisema mara kwa mara huwa anapata ushauri ambao haujaombwa kufanya kazi na wengine badala yake.

Akikiri haya kwenye chaneli ya YouTube ya mkewe Ijumaa, Mei 12, Njugush aliwakosoa watu wanaomchukia akisema hatawahi kumfukuza mkewe.

"Ana nia yangu nzuri moyoni" alisisitiza.

Alisema aliweka msingi ambao umewaweka kwenye njia ya mafanikio.

Baba huyo wa watoto wawili alikuwa akijibu swali kutoka kwa Celestine kwake na Abel kuhusu jinsi inavyokuwa kufanya kazi na wake zao.

“Wakati naanza kazi Cele alikuwa anasimamia ATM yangu, kutokana na kuelewana huko, kusonga mbele inakuwa mnatoka kwenye hatua ya nyinyi ni mabeste.

Mtu pekee,na mimi huendelea kusema mtapanda, mtateremka, lakini sitaacha kufanya kazi na Cele.

Maana ni mtu pekee aliyeniamini wakati hakuna hata hawa wanapiga makelele hawakuonekana na sasa ghafla ...usifanye kazi na mkeo!!” alifoka kwa mshangao.

"Kama nani??/Ni mtu wa kwanza kuniamini, hata wasanii wenzangu naambia msee waje tuchape clip, saa hii wanataka kuuliza tunakupendaje?" aliongeza

Akimnyooshea kidole Cele, Njugush aliweka wazi kuwa mkewe ndiye sababu yake ya kufaulu.

"Aliniamini, tunachofanya sio kitu ambacho tulifundishwa shuleni kama daktari.

Lazima uwe na uzoefu huo, na amekuwa nami tangu wakati huo.

Yeye pia ni mama wa watoto wangu. She makes me better as Njugush kuna job naweza pata, but as Wakavinye akiingia kwa mix kuna job ingine inaweza kuja wenye mnasema niwache kuwork na bibi yangu hawezi kunipea.

Kwa hivyo ikiwa inanifanya bora, nitaiweka karibu nami. Anyone who say otherwise ni mtu ako na shida, na zinaonekana"

Wanandoa hao wanajitayarisha kwa msimu wao wa nne wa TNT utakaofanyika KICC mnamo Mei 27.