logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Njugush apanda laana uwanjani Emirates ili Man United kuipiga Arsenal Jumapili (+video)

Mkewe, Celestine Ndinda alisema kwa sasa hata amechanganyikiwa kuhusu timu gani ya EPL ambayo mumewe anashabikia sana.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani29 August 2023 - 10:34

Muhtasari


  • •Njugush alitania kuwa alipanda bahati mbaya uwanjani huo kabla ya mechi kubwa ya Arsenal na Manchester United siku ya Jumapili.
  • •Katika sehemu ya maelezo ya video hiyo, alisema kwamba alikuwa akisafisha uwanja huo kabla ya mchezo mkubwa wa Jumapili.
kwenye uwanja wa Emirates.

Mchekeshaji Timothy Kimani almaarufu Njugush na mkewe Celestine Ndinda wamekuwa wakifurahia likizo nchini Uingereza, bara Ulaya na wamekuwa wakishiriki baadhi ya matukio yao ya kustaajabisha na mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya Jumatatu, wanandoa hao walifichua kwamba walitembelea uwanja wa Arsenal wa Emirates na wakaonyesha baadhi ya picha na video zilizochukuliwa wakati wa ziara yao.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Njugush alichapisha video iliyomuonyesha akikimbia kwenye korido za uwanja huo huku akiwa amevalia jezi ya Wanabunduki iliyoandikwa ‘Wa Tugi 12’ nyuma. Chini ya video hiyo, alitania kwamba alikuwa amepanda bahati mbaya uwanjani huo kabla ya mechi kubwa ya Arsenal na Manchester United siku ya Jumapili.

"Masaa ni ya kuchoma .Ndio kuleta maswara huku...mimi hii mwaka staki ma ulcers mimi naenda na ile team inakaa iko serious na maisha," Njugush alisema.

Katika video nyingine aliyoichapisha, mchekeshaji huyo alionekana akipeperusha kofia yake uwanjani kana kwamba anaondoa kitu hewani.

Katika sehemu ya maelezo ya video hiyo, alisema kwamba alikuwa akisafisha uwanja huo kabla ya mchezo mkubwa wa Jumapili.

"Jumapili kiwanja kimesafishwa," alisema.

Mke wake Celestine Ndinda pia alichapisha picha na video zao wakiwa ndani na nje ya uwanja wa Emirates.

Wakati huo, alidokeza kuwa kwa sasa hata amechanganyikiwa kuhusu timu gani ya EPL ambayo mumewe anashabikia sana.

"Kwa wakati huu sijui Kimani ni wa timu gani," alisema.

Pia alionyesha video nyingine iliyowanasa wakitafuta bendera ya Kenya kwenye bango kubwa lililo nje ya uwanja wa Emirates na hatimaye kuipata.

Siku ya Jumapili, Arsenal watakuwa wakiikaribisha Manchester United katika uwanja wa Emirates kwa mechi yao ya kwanza dhidi ya kila mmoja wao msimu huu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved