Samidoh, Karen Nyamu wamsherehekea mtoto wao wa kwanza kwa njia ya maalum

Sam Muchoki Jr ni mtoto wa kwanza wa Karen Nyamu na Samidoh na kuzaliwa kwake mnamo 2020 kulifichua mahusiano yao.

Muhtasari

•Sam Muchoki Jr aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa Jumatano na wazazi wake walichukua fursa hiyo kueleza upendo wao kwake.

•Kwa upande wake, Samidoh alisherehekea ukuaji wa haraka wa mtoto huyo wake na kumtakia baraka zaidi maishani.

wamemsherehekea mtoto wao Samuel Muchoki Jr.
Samidoh na Karen Nyamu wamemsherehekea mtoto wao Samuel Muchoki Jr.
Image: HISANI

Siku ya Jumatano, Novemba 15, wapenzi Karen Nyamu na Samidoh walimsherehekea mtoto wao wa kwanza pamoja katika siku yake maalum.

Samuel Muchoki Jr, ambaye ni mtoto wa pili wa seneta huyo, aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya tatu Jumatano na wazazi wake walichukua fursa hiyo kueleza upendo wao kwake.

Katika ujumbe wake kwa mvulana huyo mdogo, seneta Nyamu alizungumzia jinsi anavyojivunia yeye na kuahidi kumuunga mkono kila mara.

“Siku zote nitakushangilia kwa sauti kubwa mwanangu. Hutawahi kuwa na shaka kuhusu shabiki wako mkubwa ni nani,” Karen Nyamu aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Aliambatanisha ujumbe wake na video ya mvulana huyo akicheza densi ndani ya hoteli huku wimbo wa Samidoh na Joyce Wa Mamaa ‘Wendo wi Cama’ ukichezwa.

"Heri ya kuzaliwa ya miaka mitatu Tami Tami. Prince of good vibes, "aliandika.

Kwa upande wake, Samidoh alisherehekea ukuaji wa haraka wa mtoto huyo wake na kumtakia baraka zaidi maishani.

"Wakati unaenda na unakua kuwa mtu mdogo wa kushangaza. Kila tabasamu, Kila hatua muhimu ni hazina. Hapa kwa vicheko zaidi, upendo, na matukio mengi. Heri ya siku ya kuzaliwa mwanangu,” aliandika Samidoh kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Samuel Muchoki Jr ni mtoto wa kwanza wa Karen Nyamu na Samidoh wakiwa pamoja na kuzaliwa kwake mnamo 2020 kulifichua mahusiano yao ambayo yalikuwa ya siri kwa muda mrefu.

Mwaka jana, wawili hao walijaliwa mtoto wao wa pili pamoja, Wairimu ambaye alizaliwa Februari mwaka jana. Wairimu amepewa jina la mamake marehemu Samidoh, na kuwafanya wawili hao kuwa na uhusiano mkubwa.

Mapema mwaka huu, wote wawili walisherehekea msichana wao mrembo Wairimu kwa jumbe tamu. Nyamu alishiriki picha za kupendeza kutoka kwa sherehe ya kuzaliwa ya bintiye na kummiminia upendo.

Mwanasiasa huyo ambaye alijifungua katikati ya kampeni, alimtaja bintiye kuwa mwenye akili na mwenye furaha..

"Mtoto wangu wa kutoka chini hadi juu ametimiza mwaka mmoja! Naam, binti mfalme, utawala wako juu ya ufalme wa mioyo yetu umefikia mwaka mzima, na ulionekana malaika kabisa leo kwenye sherehe zako za kuzaliwa. Una akili, wewe ni mjuvi, na umeandikiwa ukuu, mtoto,” Nyamu alisema.

Kwa upande mwingine, Samidoh alishiriki picha ya bintiye kwenye Instastories zake na kisha akaandika nukuu "Heri ya kuzaliwa, mdogo wangu."