logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Shetani alitaka kuniua!” Size 8 akumbuka alivyoponea kifo baada ya kuugua ugonjwa wa kutishia maisha

Mwanamuziki huyo amekuwa akipambana na ugonjwa wa shinikizo la damu tangu mwaka wa 2015.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani15 August 2023 - 08:19

Muhtasari


  • •Siku ya Jumanne, mwanamuziki huyo alishiriki video ya mkusanyiko wa picha ambazo zilipigwa alipokuwa amelazwa hospitalini.
  • •Pia alionyesha picha zake za sasa ambapo alionekana mwenye afya na akihubiri neno la Mungu kanisani na kwenye mikutano.

Mhubiri maarufu na mwimbaji wa nyimbo za injili Linet Munyali almaarufu Size 8 amekumbuka kwa hisia kipindi ambacho alipambana na ugonjwa wa kutishia maisha.

Katika chapisho la Jumanne, mama huyo wa watoto wawili alishiriki video ya mkusanyiko wa picha zilizopigwa wakati alipokuwa amelazwa hospitalini.

Katika maelezo ya video hiyo iliyochapishwa kwenye Instagram, Size 8 alimshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yake huku akibainisha madai shetani alikusudia kumuua.

“Shetani alitaka kuniua. Lakini Yesu alisema Hapana. Sasa maisha yangu ni ya Yesu, popote anaponiongoza nafuata,” Size 8 alisema Jumanne.

Katika picha hizo za kumbukumbu zilizokusanywa kwenye video ambayo alichapisha, mke huyo wa DJ Mo alionekana hospitalini ambako alionekana kutokuwa vizuri kiafya. Kwa kutazama picha hizo, mtu anaweza kusema kwa urahisi kwamba alikuwa akipitia maumivu mengi katika kipindi hicho.

Ili kuthibitisha jinsi Mungu alivyomtendea miujiza, mwimbaji huyo pia alionyesha picha zake za sasa ambapo alionekana mwenye afya njema na akihubiri neno la Mungu kanisani na kwenye mikutano.

 "Maisha yangu ni yako Yesu Kristo, nafuata njia yako," alisema.

Mwaka uliopita, mwanamuziki huyo alifichua kuwa amekuwa akipambana na tatizo la shinikizo la damu zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Kupitia YouTube channel ya 'The Murayas', alisema aligunduliwa kuwa na ugonjwa huo mnamo Januari 31, mwaka wa 2015.

Ugonjwa huo ulitambulika baada yake kuzirai mtaani wakati alipokuwa anaelekea nyumbani baada ya kutumbuiza katika tamasha ambayo alikuwa amehudhuria pamoja na mume wake Samuel Muraya almaarufu DJ Moh.

"Nilizirai nikiwa mjini nikapelekwa katika hospitali moja iliyokuwa pale. Hapo ndipo nikaambiwa shinikizo la damu yangu ni kubwa mno. Nilikuwa siko sawa. Kutoka siku hiyo nilianza kuchukua dawa za shinikizo la damu," alisimulia.

Mama huyo wa watoto wawili alisema ugonjwa huo umekuwa ukimzidia mara kwa mara na kumfanya alazwe hospitali mara kadhaa tangu ulipogunduliwa.

Alisema amekuwa akipambana nao kwa ujasiri. Hata hivyo alikiri kwamba hivi majuzi ugonjwa huo ulikuwa umemwathiri kiasi cha kupatwa na msongo wa mawazo na kutaka kukata matumaini ya maisha.

"Mara hii haikuwa rahisi kwangu. Nilihisi nilikuwa nazama kwenye msongi wa mawazo.Kama sio neema ya Mungu nadhani ningekufa moyo kabisa.. Nilihisi kama kwamba nimechoka kupambana, nimechoka kuendelea, nimechoka kusubiri, nimechoka kusubiri muujiza. Mara nyingi sikuwa nahisi vizuri. Kuna wakati Moh alikuja katika chumba cha malazi na nikamwambia sihisi poa na nahisi kukata tamaa. Hiyo ni baada ya kutoka hospitali. Tulishiriki naye mazungumzo marefu," Alisema.

Mwanamuziki huyo alisema DJ Moh amekuwa guzo muhimu sana katika mapambano yake na shinikizo la damu na amekuwa akimtia moyo na kumsihi asikate tamaa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved