logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vybz Kartel amnunulia mamake gari la kifahari baada ya kushinda rufaa dhidi ya hatia ya mauaji

Msanii huyo wa Jamaika amekuwa gerezani tangu mwaka wa 2011 alipokamatwa kwa mauaji ya Clive "Lizard" Williams.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani05 April 2024 - 13:08

Muhtasari


  • •Mwimbaji huyo ambaye alikuwa amefungwa jela miaka 32 alimnunulia mzazi wake gari aina ya BMW kama zawadi kwa siku yake ya kuzaliwa.
  • •Msanii huyo wa Jamaika amekuwa gerezani tangu mwaka wa 2011 alipokamatwa kwa mauaji ya Clive "Lizard" Williams.
alimnunulia mama yake grai la kifahari kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Bi Teresa Palmer, mama ya staa wa dancehall wa Jamaika Adidja Azim Palmer almaarufu Vybz Kartel, ni mmiliki mpya wa gari.

Mwimbaji huyo ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 32 jela alimnunulia mzazi wake gari aina ya BMW kama zawadi kwa siku yake ya kuzaliwa.

Kartel alifichua habari hizo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo alishiriki picha za mzazi huyo akiwa amesimama kando ya gari hilo jeupe.

“Heri ya Siku ya Kuzaliwa Bosi wangu, Malkia wangu, Malaika Mlezi wangu #MAMAYANGU,” Vybz Kartel aliandika chini ya picha za mama yake na gari alizoshiriki kwenye Instagram.

Mwimbaji huyo wa dancehall amekuwa gerezani tangu mwaka wa 2011 alipokamatwa kwa mauaji ya Clive "Lizard" Williams.

Mnamo 2014, alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kiwango cha chini cha miaka 35, baadaye kikapunguzwa kwa rufaa hadi miaka 32 na nusu.

Katikati mwa mwezi uliopita, mwanamuziki huyo alindolewa mashtaka ya mauaji na mahakama ya London.

Mahakama ilisema kwamba majaribio ya kuwahonga majaji wakati wa kesi yake yalifanya uamuzi huo kutokuwa salama.

Kartel, alifungwa nchini Jamaica tangu 2011. Kesi hiyo ilihusisha kutoweka kwa mshirika wake Clive "Lizard" Williams mnamo 2011. Mwili wa Williams haukupatikana.

Kufuatia kesi ya muda mrefu mwaka wa  2014, Kartel na wengine watatu walipatikana na hatia na kupewa kifungo cha maisha jela kwa muda usiopungua miaka 35, na baadaye kupunguzwa hadi miaka 32.5 baada ya kukata rufaa.

Mnamo Februari 2024, Kartel alikata rufaa ya mwisho kwa Baraza la Privy huko London, mahakama ya juu zaidi ya Jamaika na mataifa fulani ya Jumuiya ya Madola. Mawakili wake walidai kuwa hakimu anayesimamia kesi ya awali alishughulikia vibaya madai ya kutoa hongo kwa majaji.

Siku ya Alhamisi Machi 14 2024, Baraza la Privy lilikubaliana na utetezi. Waliamua kwamba uamuzi wa hakimu wa kumruhusu mshtakiwa aliyeshtakiwa kwa hongo kubaki kwenye baraza la mahakama ulihatarisha haki ya kesi hiyo.

Baraza la Faragha limerejesha kesi hiyo kwa Mahakama ya Rufaa ya Jamaica. Mahakama hii itaamua iwapo Kartel na washtakiwa wenzake watakabiliwa na kesi mpya.

Ingawa amefungwa tangu 2011, Kartel alirekodi nyimbo nyingi mpya kutoka kwa seli yake kwa kutumia simu mahiri na aliandika pia kitabu kinachomhusu yeye kilichoitwa "The Voice of the Jamaica Ghetto".


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved