"Wewe ni baraka kubwa zaidi maishani mwangu" Diana akiri upendo kwa mwanawe wa kulea, Morgan Bahati

Rapa huyo alikiri upendo wake mkubwa kwa Morgan na kueleza jinsi anavyojivunia yeye.

Muhtasari

•Diana alionyesha maendeleo makubwa katika maisha ya Morgan tangu kadri miaka inavyoendelea kusonga.

•Bahati alimchukua Morgan kuwa mtoto wake mwaka wa 2014 wakati alipoenda kutumbuiza katika nyumba ya  watoto yatima ya ABC.

Diana Marua na Morgan Bahati
Image: HISANI

Mwanavlogu na rapa mashuhuri wa Kenya Diana Marua amemsherehea mtoto wake wa kulea Morgan Bahati.

Siku ya Jumatano, mke huyo wa mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati kupitia ukurasa wake wa Instagram alionyesha maendeleo makubwa katika maisha ya Morgan tangu kadri miaka inavyoendelea kusonga.

"Jinsi ilivyoanza vs jinsi inavyoendelea," Diana Marua alisema chini ya picha  za hatua tofauti za mvulana huyo wa miaka 13.

Mama huyo wa watoto watatu aliendelea kukiri upendo wake mkubwa kwa Morgan na kueleza jinsi anavyojivunia yeye.

"Wewe ni baraka kubwa maishani mwangu. Nakupenda @morgan_bahati," Diana alisema.

Mamia ya wanamitandao walimiminika chini ya chapisho hilo kutoa hisia zao kuhusu ujumbe wa Diana kwa mwanawe huyo wa kulea huku wengi wakionekana kumpongeza kwa jinsi alivyoboresha maisha yake.

millywajesus:You have done a very good job.

caroxheal:Your the best and blessing to Morgan

kibunja.lucy: Thankyou for taking care of him, be blessed.

_y.thera: Enyewe always trust the process, keep it locked @diana_marua

Mapema mwaka huu, Diana alisema ameona maendeleo na mabadiliko mengi kwa mwanawe na kumtakia mwongozo wa Mungu maishani.

"Nimekuona ukibadilika na kuwa Muungwana uliye leo na kitu ninachoweza kusema ni kwamba Mungu aendelee kukulinda na aniongoze mimi na Baba yako siku zote tuweze kukulea ili uwe toleo bora kwako," alisema Januari.

Mama huyo wa watoto watatu pia alionyesha fahari yake kubwa kwa kumpa Morgan alichotaka kwa siku yake ya kuzaliwa.

Diana alikuwa mama mwenye fahari baada ya mwanawe huyo wa kulea kuhitimu kutoka shule ya msingi hadi Sekondari ya Chini mwishoni mwa mwaka jana. 

Huku akimsherehekea Morgan kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana Marua alisema kuwa anajivunia mafanikio hayo makubwa ya mwanawe na akamhakikishia kuhusu upendo wake kwake.

"Ninajivunia kuitwa mama yako. Imekuwa ni safari na kukuona ukihitimu siku ya leo, nimeshangazwa na uaminifu wa Mungu. Nakupenda Morgan Bahati," Diana aliandika mwezi Desemba.

Mama huyo wa watoto watatu alisema hayo baada ya kuhudhuria hafla ya kuhitimu kwa watahiniwa wa darasa la sita katika Juja Preparatory School ambapo Morgan amekuwa akisomea.

Bahati alimchukua Morgan kuwa mtoto wake mwaka wa 2014 wakati alipoenda kutumbuiza katika nyumba ya  watoto yatima ya ABC ambapo alikulia pia baada ya mama yake kuaga dunia.