Bwanangu alitishia kujiua nikamletea kamba ajinyonge - Maggie

Kama wadhani ushawahi patana na watu wenye roho ngumu humu duniani, basi hujapatana na mwanadada kwa jina Maggie.

Mwanadada huyu aliwashangaza waskizaji wengi wa Redio Jambo ikiwemo mtangazaji Massawe Japanni. Kisa na maana? Alidai kuwa wakati mumewe alitishia kujiua alikimbia sokoni na kununua kamba kisha kumpa na kuondoka ili ampe nafasi ajitie kitanzi.

Kulingana na Maggie, mumewe alimtishia kuwa ile siku atamuacha atajimaliza na kumhakikishia kuwa hatapata mume mwingine.

Alisimulia kuwa baada ya kumnunulia kamba, hadi wa leo hajawahi jitia kitanzi na kuwa bado yeye hungoja.

Huku Massawe akishangazwa na usimulizi wake, Maggie naye alidai kuwa vitu vingine kama vile unapaswa kuwa kichwa ngumu.

Mimi nilikuwa naambiwa eti nikimuacha niende hakuna mwanaume nitapatana naye, halafu kuna wakati aliniambia kuwa atajinyonge ile siku nitamuacha.

Nikamwambia sasa badala ya kwenda kununua kamba ujinyonge mwenyewe nikanunua kamba nikampea, nikamwambia haya hiyo hapo. Sasa badala aende anunue kamba afadhali mimi mwenyewe ninunue.

Nikampea kamba nikajiondoa hajawahi kufa, mimi hungoja afe na hajawahi kufa. Massawe vitu zingine unafaa kuwa kichwa ngumu.