'Bwanangu aliuza nguo za mtoto ili akalewe,' Asimulia mwanadada

Watu wengi hutumia mda wao kunywa pombe kama njia moja ya kujistaarabisha baada ya siku refu kazini au kila baada ya wiki.

Lakini kuna wale ambao hawawezi hata fanya kazi kidogo bila kunywa pombe, kwani imefika mahali ulevi umegeuka kuwa ugonjwa.

Kulingana na mwanadada mmoja, mumewe ameadhirika na pombe na hata kuna siku alimuacha kinywa wazi baada ya kuanza kuuza nguo za mtoto wake ili akabugie angalau pombe kiasi.

Akizungumza na Massawe Japanni katika kipindi cha Bustani la Massawe, mwanadada huyo alisema kuwa yule jamaa hata hakuwa anamshughulikia mkewe tangu alipompachika mimba.

Alipopata mtoto na kudhani kuwa atabadilika, yule jamaa alianza kumuonesha madharau na kuuza nguo na taulo za mtoto zile ambazo mkewe ndiye aliyenunua na jasho lake.

Soma usimulizi wake,

Wakati nilikuwa na mimba bwanagu hakuwa ananishughulikia. Mpaka wakati nilipata mtoto bwanangu alifika mahali kazi yake ni kunywa, mpaka ilifika mahali akaanza kuuza nguo za mtoto.

Aki Massawe mimi nilikuwa nashtuka, eti juu amekosa pesa watu mpaka hawakuwa wanampa kazi, anaona hakuna kitu amebakisha mimi naingia kwa bag za mtoto napata nguo zake, towel zote ameenda akauza.