Capitol Hill ya Raila Odinga na Ikulu ya Uhuru ni nguzo kuu Kenya, asema Orengo

bbi
bbi
Seneta wa Siaya wakili James Orengo ametoa taarifa kwamba kuna nguzo mbili kuu za mamlaka nchini.

Katika mahojiano na kituo cha utangazaji jana Jumapili usiku, Orengo alisisitiza kuwa Kenya ina miimili miwili mikuu.

Nguzo ya kwanza aliitaja kuwa ipo katika ofisi ya kinara wa ODM ,Capitol Hill na nyingine katika Ikulu anapoishi Rais Uhuru Kenyatta.

"Hebu tazama uone idadi kubwa ya watu wanaomiminika Capitol Hill wakiwepo makatibu wa wizara, makatibu wa kudumu, wanasiasa na wengineo."

Soma hadithi nyingine:

"Tunapozidi kuelekea katika safari ya 2022, tutashuhudia ugawaji wa mamlaka. Kama sio kupitia mabadiliko ya taasisi basi kisiasa."

Seneta huyu alisema kuwa mabadiliko ya taasisi yatakuwepo kupitia mpango wa BBI.

Mkataba na makubaliano ya BBI yalitimia kupitia "Handshake" ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.

Orengo amesema kuwa Handshake ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta haihusu kamwe maswala ya kugawana mamlaka.

Soma hadithi nyingine:

Seneta huyu aidha amehoji kuwa jinsi serikali inavyoendesha mamlaka ni ishara kuwa kuna nguzo mbili za mamlaka nchini.

"...Inapokuja maswala ya kisiasa yanayohitaji uamuzi viongozi hawa wawili hushauriana. Katika utekelezaji wa uamuzi huo, Rais Kenyatta hutoa agizo kwa mawaziri na viongozi serikalini." Alisema Orengo.

Seneta huyu aidha alitoa ubashiri kuwa kuna uwezekano kwa kura za kugeuza katiba Juni mwaka ujao.

Orengo aidha alimshauri Miguna Miguna asife moyo katika juhudi zake za kurejea nchini.

"Miguna hana kila haki ya kukubaliwa arejee Kenya...azidishe juhudi za kurudi Kenya...anafaa arudi."

Soma hadithi nyingine:

Kiongozi huyu aidha alikana taarifa kuwa upinzani ulimtema wakili Miguna.

Miguna alifurushwa nchini baada ya tukio la kumwapisha kinara wa upinzani Raila Odinga mwaka wa 2018.

"Mawakili wa Nasa walimwakilisha vyema katika mahama ya rufaa na wakapewa maagizo ya kumrejesha..." Aliendela Orengo.

Mwezi wa Agosti, Miguna aliwaburuza mahakamani maafisa 25 wakuu serikalini.

Kulingana na Miguna, maafisa hawa walimnyima uraia.

Miguna alisimama kidete kuwa hakuna siku aliwahi ukana uraia wa Kenya.