Be careful… Diamond atawapa tu machozi,you will never be happy-Tanasha atoa tahadhari

Tanasha Donna  sasa anazungumza na kuandika kila kitu kuhusu uhusiano na anaweza kutumika kama mtaalam wa kuwapa himizo waliosalitiwa na mapenzi .

Hii ni baada ya mrembo huyo wa Kenya kuchana na msanii wa Bongo  Diamond Platnumz. Tanasha amekuwa akiwatahadharisha wanawake mtandaoni kupitia posti zake  kuhusu masuala ya mahusiano  na katika mojawapo ya posti zake amesema hayuko  tayari kujipata katika uhusiano na macelebs wa kiume tena.

Ameonekana kumpiga  moja Diamond  akidai kwamba nyota huyo wa Bongo hajui jinsi ya kuwafurahisha wanawake ,aliandika

@BONFIRE, YOU SURE KNOW HOW TO MAKE A WOMAN FEEL LIKE A QUEEN. HAPPY WOMEN’S DAY TO ALL THE STRONG FEARLESS POWERFUL WOMEN IN THE WORLD. 🌊❤️; SHE POSTED.

Katika posti nyingine aliwaonya wanawake dhidi ya kuhadaiwa na muonekano wa wanaume kabla ya kutumbukia katika  mapenzi nao.

PAY ATTENTION. EVEN SALT LOOKS LIKE SUGAR,’ Aliandika

Tanasha    alitengana na  Diamond  wiki moja iliyopita  baada ya staa huyo kudaiwa kuhusika kimapenzi na  mwanadensi aliyeshirikishwa  kwenye video  ya wimbo Jeje . Katika ujumbe mwingine alioandika  katika instagram  Tanasha alisema .

WHEN PEOPLE WRONG YOU NEVER WRONG THEM BACK. YOU CAN ONLY FIGHT EVIL WITH GOOD. YOU WILL SLEEP BETTER AT NIGHT KNOWING ALL ALONG YOU WERE REAL, GENUINE, LOYAL AND NOT FAKE, AS YOU SIT BACK AND RELAX FOR THEIR KARMA TO HIT THEM.