I QUIT !- Sababu Unazofaa kuzitegemea kuacha ndoa/Uhusiano Mbaya

  Ndoa ama uhusiano kati ya watu wawili wanaopendana na kitu cha kipekee . Ni uhusiano ambao kila mmoja anafaa kumtegemea mwenzake kwa hali na mali na baada ya kuwekeza muda na hisia ili kuhakikisha kwamba mambo yanasonga mbele vyama ,huwa vigumu sana mtu kuamua kusalimu amri na kuondoka uhusiano au ndoa yake .

Lakini kwa sababu ya changamoto nyingi za mahusiano kama vile kutokuwpo mawasiliano yafaayo, ukosefu wa tendo la ndoa , na msaada wa kihisia-kuna sababu ambazo hukufanya useme ‘enough is Enough’ na uondoke .Hizi hapa sababu zinazofaa kukufanya kuacha ndoa au uhusiano wako

 

  1. Kukataa kuwasiliana .

  Kadri unavyojaribu kuwasilisha ujumbe wako au kuzungumza na mwenzio hataki au hawezi kukuelewa . umejaribu kuzungumza kwa sauti ya chini ,umetoa vitisho  umejaribu kunyamaza lakini hakuna kinachobadiliska .Hii ni ishara kwamba huenda mtindo huo wa malumbano na kutowasiliana ifaavyo ndio utakaokuwa ada . Ishara hii ni mojawapo za kuanza kukutayarisha uzingatie kuondoka.

Must Read:Bibi Wa Pili? Mbivu na Mbichi kuhusu ndoa za Polygamy

 2.Kila kitu ni kibaya .

  Hakuna kizuri kinachotoka katika  mdomo wake . unachofanya,unachosema ,unachovalia –vyote havimpendezi! Kama wanandoa au walio katika uhusiano ,panafaa kuwa na njia nzuri ya upedo ya kumwambia mwenzako chochote bila kumkwaza .lakini inafaa kuzua hofu endapo kila anachpofanya au kusema mwenzako kina kuja na  ubaya . tatizo hili linakufanya unakuwa na woga wa kufanya uamuzi wowote ukohofia kwamba majibu ya mwenzako hayayakupendeza na   dhana inayozuka mara nyingi itakuwa ya kudhalilishwa .

 3.Unahisi katika moyo wako kwamba uhusiano huo sio mzuri

  Umefanya kila uwezalo kuboresha uhusiano wako . umezungumza na rafiki zako  na kusoma vitabu viingi kuhusu mahusiano  .katika moyo wako umeshahamu kwamba tayari umebeba mzigo mzito na unakuumiza na huwezi kuendelea hivi .  Msisimko wa kale kati yenu wawili haupo tena . Hali ya uhusiano wenu inazidi kudorora au imesalia pale pale .Hii ni ishara kwamba wakati umewadia kujifungilia mlango na kuchukua basi lijalo .

Stacy 4

 4. Kukataa kubadilika/kuboreka

    Hakuna mtu halisi asiye na dosari  .lakini iwapo kuna udhaifu katika mmoja wenu au nyote  basi mnafaa kuchukua hatua za kubadilika ili kuwa watu bora .Chukueni  hatua za kuhakikisha kwamba mnabadilisha mambo ndani yenu ambayo yanavuruga uhusiano wenu .Ila iwapo mwenzio hana nia au ari ya kutaka kubadilika basi itakuwa vigumu kupiga hatua ya kuimarisha uhusiano wenu .

Waluhya Waliwakosea nani? Vijembe 10 vya utani ambavyo vimetupatia Ucheshi

  5. Hataki kupata usaidizi .

Umemrai mwenzako kutafuta  usaidizi wa mshauri ili kumaliza  matatizo ya uhusiano wenu . Labda hata umekuwa wa kwanza kufika kwa mshauri zaidi ya mara moja ukifikiria atategwa na chambo kasha akubali kuja lakini wapi! Kwa ufupi unahisi kuna  hali kubwa  kwa upande wake kukataa kabisa kuja ili kuyaweka wazi masuala ambayo yanavuruga ndoa ama uhusiano wenu .Yeye haoni tatizo lolote ilhali wewe na watu walio nje  wanashuhudia kila kilicho kibaya katika uhusiano huo.

6.Mateso ya kifikra na kupigwa

  Zamani  ilikuwa kawaida wanaume kwa wanawake  kuvumilia ndoa na mahusiano yenye    tatizo kubwa la kusumbuliwa fikra na mwenzako bila kulichukulia kama jambo kubwa .lakini sasa imegundulika kuna uhusiano mkubwa kati ya mtu anayetatizwa fikra na maamuzi anayofanya .Ndoa isiokuwa na kujali ,huzaa maamuzi ambyo huleta kilio . Pia kuna wanandoa –hasa wanawake ambao huvumilia ndoa  licha ya kupigwa na waume zao .Hili halifai kukubalika kwa vyovyote vile na unafaa kufanya uamuzi wa kuondoka uhusiano ama ndoa kama hiyo .

Must Read: Still Single?Sababu 8 zinazokufanya usiwe na Mpenzi

7 .Usinzi/Uzinifu

  Hili halihitaji  maelezo . Ingawaje kuna nyakati mmoja wenu katika uhusiano anaweza kuteleza na kujipata nje ya ndoa , haifai kuwa mtindo wa kumsamhe mwenzako ambaye anahatarisha hali ya uhusiano au ndoa yenu kwa kufanya msururu wa mahusiano ya kimapenzi  na watu wan je ya ndoa .

  Ingawaje  kuna sababu nyingi kuu ambazo zinaweza kukufanya kuondoka katika uhusiano au ndoa ,hizi ni baadhi  tu ya sababu hizo wala sio  msingi wa kuacha ndoa au uhusiano wako . wakati mwingine ,yaweza kuwa sababu moja au mseto wa sababu hizo na nyingine zaidi .  Kwa vyovyote vile ,tumia juhudi zote kuwa na ndoa au uhusiano mzuri lakini usijivunje mgongo  kupasua kuni zisizoweza kushika moto .

Patanisho: Bi Terry amfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike 

 

Kiprono, 28, aliwasilisha tatizo linalomsumbua na kumfanya kutatizika maishani kutoka mwaka jana mwezi wa Oktoba.

Baba huyu wa watoto wawili alikosana na bibiye Terry  na akatoroka na kuenda kwao. Mzozo huu ulianza kutokota na kurindima moto kipindi bwana huyu alipoanza kumshuku kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na wateja aliokuwa anawauzia chakula katika kibanda chake.

Soma mengine hapa.

Man begs Martha Karua for daughters hand in marriage

Wateja wake walikuwa mafundi wa mjengo uliokuwepo karibu na kibanda chake  na habari zilienea na kumfikia Kiprono huenda mkewe akawa anachepuka na mafundi hao. Wivu mwingi ukamwingia na akaanza kumshuku sana na kuanza kudadisi tetesi hizi ili aweze kuufahamu ukweli wa mambo.

Alifika nyumbani kwake saa mbili za usiku na kumkosa chumbani huku watoto wao wawili wakiwa katika hali ya upweke.

Hapa hakusita na akaamua kumpigia simu mkewe ili kujua aliko. Mama Derrick hakuchukua simu ila aliikata. Alikuwa na mafundi wake kwenye mjengo akiwauzia chakula na alihofia kuenda nyumbani kama amechelewa kwani bwanake angemchapa.

Jombi atumia gundi kumfunga mkewe sehemu za siri

Kwenye laini ya simu na kituo cha Redio Jambo kipindi kinachoruka kila asubuhi patanisho alionekana mwenye masimango na kusononeka kwani alikuja kupata ulikuwa udaku wa majirani uliofanya amshuku mkewe. Hadithi hizi za udaku wa majirani zilitia shubiri ndoa yake ya miaka 5.

Baada ya kutoroka na kwenda kwao, mama Derrick alirudi anapofanyia kazi na kumfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike ambaye walijuana kipindi na ambapo alikuwa anawatembelea nyumbani kwao. Kiprono aliichukua namba yake ya simu  na kuanza kumtongoza.

Man accused of beating wife over sukuma wiki turns anger on investigating officer

“Alinipata naye kwa chumba cha kukodisha na akaanza kulia. Hata hakumpiga cousin yake.”

Alipopigiwa simu na Gidi, mama Derrick alifunguka mwanzo mwisho kuhusu jinsi bwanake alisaliti penzi lao.

“Huyo alinikosea sana. Yaani ananiacha amenimalizia na kuenda kwa cousin kufanya naye sex. The same day !” alishangaa Terry.

“Si hata wewe uanweza mpatia miaka 10?” aliuliza Terry.

Akionekana kusimama kidete na msimamo wake Bi Terry alisema atarudi baada ya muda alioutaja mbeleni.

Nilipigwa na mke wangu mja mzito na akuniuma mgongo

“Nishamsamehe lakini hiyo miaka 10 kwanza iishe…yaani nikapata macd kwa nyumba. Sijui alikuwa ameniwekea nikuje kuona ama?”

Kiprono alimsingizia shetani kwa majaribu ya kutoka na binamu wa Terry kimapenzi

“Gidi hiyo ni shetani tu ata mimi sikuelewa vile kitu yenyewe ilihappen mwongeleshe apunguze miaka Gidi .” aliomba Kiprono.

Zari Hassan apata kipenzi kipya

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Zari ameweza kutokea katika mitandao ya kijamii na mwanaume ambaye amtamrithi msanii na mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz. Katika chapisho siku ya ijumaa, mrembo huyu na mama wa watoto watano amesema kuwa mwanamume aliyempata kwa sasa ni baraka kubwa kwake.

Zari na Diamond waliachana mwaka uliopita tarehe 14 Februari siku ya wapendanao kwa kuchapisha ua jeusi lililoambatana na ujumbe mzito wa kuonyesha hawapo tena katika mahusiano.

zariposeswithdiamond
Zari na mpenzi wa zamani Diamond

Mama Tiffah alionekana kukasirishwa na tendo la mzazi mwenzake kukiri katika runinga na redio kubwa nchini Tanzania kuwa aliweza kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Zari The Bosslady ametupia picha ya mpenzi wake mpya katika mtandao wake maridhawa wa Instagram. Katika chapisho  hilo, mama Tiffah ameonekana kummiminia sifa kedekede mume huyu mpya na kubana jina lake kabisa na kumwita Bwana M.

Mrembo huyu ambaye ni msanii kutoka nchi jirani ya Uganda baada ya kumtema staa wa muziki Chibu Dangote alionekana kusononeka sana kwa kumpoteza mpenzi aliyempenda kwa dhati.

From Verona to Venice! Check out how Massawe Japanni is slaying in Italy

Katika mitandao ya kijamii, anadokeza kwamba mshikaji wake mpya amemkubali pamoja na watoto wake watano. Zari amezaa watoto wawili na Diamond platnumz na watatu na aliyekuwa mmewe marehemu Ivan Ssemwanga.

Zari amefunguka sana maneno matamu kwa mpenzi wake.

“Nimebarikiwa sana kukupata wewe. Nakupenda sana Bwana M… Sio kwa vitu unazoninunulia wewe kwa kuwa nimeona tena kubwa na nzuri maishani mwangu ila naupenda moyo wako na jinsi unavyonifanya nijihisi vizuri pamoja na watoto wangu.” Anasema mrembo huyu.

Akionekana kuwa amepitia katika mahusiano ya mateso,  mrembo huyu amesema kuwa yeye huwajenga wanaume na wala sio sampuli ya wanawake wanaotegemea kupewa na wanaume.

“Mimi sio sampuli ya wanawake wanaochukua kutoka kwa wanaume ila nawajenga.”

zari with teddy bear
Zari Hassan

Anasema Bwana M ni tofauti na wapenzi wa jadi na kwamba ana upole na utulivu mwingi ambao unafanya ampende zaidi. Mzazi mwenza Simba  anaonekana kuzama katika mahaba mazito na mtangazaji wa redio Tanasha Donna kutoka hapa nchini.

Penzi lake diamond na Tanasha linaonekana kunoga zaidi baada ya mkali huyu kumpeleka Donna nyumbani Madale na kumtambulisha kwa  familia. Dadake Platnumz anapenda sana mahusiano haya na anajuta kuwa wawili hawa wangekutana zamani.