Pesa maua! Bridget Achieng afichua kitita alichotumia kubadili rangi

Kidosho huyu Bridget Achieng alisema kuwa tangu aanze kuchibua ngozi yake ametumia shilingi milioni 10.

Zaidi ya hayo, alisema kuwa hakuwa na pesa lakini alipopata pesa akaamua kuzitumia vizuri.

“I didn’t have money and when I got it, I said I will buy Kenya, I’ll buy the world. If I had more money, right now I’d have used 50 million,” she said on her YouTube channel.

Nilifungwa miaka kumi kwa kupachika mtoto mimba,’ Jamaa afichua

Achieng, aliyejifungua mtoto wake juzi bado anatarajia kupata watoto wengine zaidi.

 “My stomach was just cut the other day, I haven’t healed. I’m not pregnant but I want a house full of babies. A football camp or a rugby team,” alisema.
Hata hivyo, pasi na Bridget kutaka kuwa na watoto wengi hawezi kwa sababu alifanyiwa upasuaji hivyo basi hawezi jifungua watoto zaidi ya watatu.

“Unfortunately, I can only get four babies, and the fourth one is by God’s grace. But because I gave birth through CS, I can only get three babies straight. So trust me, I’m gonna give you three babies.”

Licha ya hayo, alisema kuwa mtoto wake Sekani aliacha kunyonya pindi tu baada ya kumpoteza mama yake.

“Sekani stopped breastfeeding when he was three months. I think due to my mum’s death and stress, it made me lose milk. So my milk dried. So for the last few months, he does feed on breastmilk. Happy baby, happy mother.”

Toboa Siri! Mashabiki wamtaka Kate Actress afichue baba ya mtoto wake

Amini usaimini, Achieng alisema kuwa mpenzi wake ni mrembo zaidi kiasi ambacho hawezi weka picha yake waziwazi kwenye mtandao wa kijamii.

“He is one fine something. I call him Alejandro. I will post his picture once he accepts to be public,” she said.

“He is too fine that I’m not about to handle the thunder you women want to bring my way. I’m not ready to show him to the world, but we will revisit.”

Wacha tungoje kwa hamu na ghamu kwa ile siku ambayo Achieng atafichua sura ya mpenzi wake.

Wabunge 23 wataka naibu rais Ruto kujiuzulu

Jumla ya wabunge 23 wamemshtumu Naibu Rais William Ruto kwa kumdharau Rais Uhuru Kenyatta na kumtaka ajiuzulu.
Walisema naibu rais amekuwa akishambulia maafisa wa serikali na kufanya kila jitihada kusambaratisha maafikiano baina ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na kuvuruga ripoti ya BBI.

Alichokibeba Paul Manyasi katika ‘safari’ ya ndege, jina lake la msimbo

Wanasiasa hao kutoka vyama vya Jubilee, ODM, Ford Kenya, Wiper na Kanu – wengine wao ambao wamekuwa wakimuunga mkono naibu rais – walimshtumu kwa kupiga vita serikali akiwa ndani na kumtaka aondoke.
“Kama hujaridhishwa na uongozi wa rais Uhuru Kenyatta, nakudhubutu ujiuzulu,” Mbunge wa Tiaty William Kamket alisema.

Uhuru na Raila

Wabunge hao walikuwa wanajibu mashambulizi ya wanachama wa mrengo wa Tangatanga siku ya Jumanne, dhidi ya waziri wa usalama Fred Matiang’i, katibu wa kudumu wa maswala ya ndani Karanja Kibichu na Inspekta mkuu wa Police Hillary Mutyambai.

PATANISHO: Mume wangu huwapa wanawake simu wanitusi

Wanasiasa wa mrengo wa Tangatanga walikuwa wamedai kuwa watatu hao walipanga ghasia zilizoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya Kibra wakati wa uchaguzi mdogo wiki iliyopita. Ruto pia amekuwa akimshambulia Raila na wafuasi wake wa ODM akidai kwamba walichochea hali tete ili kushinda uchaguzi huo mdongo au kuvuruga maridhiano baina ra raila na Uhuru.
Lakini wabunge wanaowaunga mkono Uhuru na Raila walisema kwamba mashambulizi dhidi ya maafisa wa serikali ni madharua kwa rais – ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuteua maafisa hao. “Wacha kushtumu wafanyikazi wa umma. Wacha kushtumu waziri, katibu wa kudumu na Inspekta mkuu wa polisi. Jitokeze peupe na kusema tu kwamba ni rais unashtumu,” Kamket alisema.

uhuru.birthday
Waliohudhuria mkutano huo katika majengo ya bunge ni Jimmy Angwenyi (Kitut Chache North), Gathoni Wamuchomba (Mwakilishi wa wanawake Kiambu), Ben Momanyi (Borabu), Fatuma Gedi (Mwakilishi wa wanawake Wajir), Peter Mwathi (Limuru), Mishi Mboko (Likoni) and Raphael Wanjala (Budalang’i).

‘Nilifungwa miaka kumi kwa kupachika mtoto mimba,’ Jamaa afichua

Wengine walikuwa Ken Chonga (Kilifi Kusini), Jerusha Momanyi ( Mwakilishi wa wanawake Nyamira), Abdikarim Osman (Fafi) na Samuel Arama (Nakuru Mjini).
Momanyi ambaye amekuwa mwandani wa Naibu Rais, alibadili msimamo na

 

kusema wataunga mkono mapendekezo ya BBI kufanyia katiba mabadiliko ili kumpa rais mamlaka kumtimua naibu wake ambaye ni mtovu.“Uhuru anafaa kupewa mamlaka kumfuta naibu wake. Tunataka mabadiliko ya katiba rais akipata naibu rais mwenye utovu wa nidhamu,anaweza kumfuta kazi.

 

Huezi jifanya wewe ni naibu wa rais na huku unadhalilisha urais,” Momanyi alisema.
Angwenyi, ambaye pia ni naibu kiongozi wa wengi bungeni, pia alikashifu mrengo Tangatanga kwa kutaja jamii gusii kijiji pamoja na kumshambulia waziri Matiang’i.

Upekuzi: Paul Manyasi aliyedondoka kwenye KQ na Cedric Shiunja ni mmoja

Kisa cha mwanaume aliyedondoka katika ndege ya KQ Julai kimekuwa cha kukanganya sana hususan baada ya familia inayokisiwa kuwa ya jamaa huyo kukana madai hayo huku wakisema mwanao ni Cedric Shiunja.

Mwili wa Paul Manyasi ulioganda kutokana na kupigwa na upepo mkali uliangukia bustani moja nchini Uingereza wakati ndege ya KQ ilipofungua magurudumu yake ikijiandaa kutua.

Hata hivyo haijabainika wazi iwapo Manyasi aliaga dunia katika safari hiyo iliyochukua masaa manane na nusu au alifariki alipoangukia ardhi mkavu.

Kulingana na upekuzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Sky News, inaonesha kwamba Manyasi alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya Colent iliopewa kandarasi ya usafi katika uwanja wa ndege wa Nairobi.

+ Picha ) Alichokibeba Paul Manyasi Katika ‘Safari’ Ya Ndege, Jina Lake La Msimbo

Hata hivyo, kampuni ya Colnet ambayo ilipinga madai hayo huku ikikana kuwepo kwa mfanyakazi kwa jina la Paul Manyasi.

Jamaa huyo anaaminika kujificha katika gurudumu la ndege katika angatua ya JKIA Nairobi.

Babake Isaac Manyasi katika mahojiano na kituo cha KTN alisema kwamba mwanawe yupo katika rumande na hakuwa amefariki jinsi ilivyoripotiwa.

“Si mwanangu, niliwaambia walionionesha kwenye picha sio kijana wangu, mwanangu hajakuwa nyumbani tangu 2016 alipoenda Nairobi,” Isaac alisema.

Awali, familia ilisema kuwa mwana wao ni Cedric Shiunja wala sio Paul Manyasi.

Aidha, iliongezea kuwa hawajui mwanao alipo na wamekataa taarifa za kuhusishwa na mwili wake Paul.

+ Picha ) Familia Ya Paul Manyasi Yamgeuka, Yasema Kijana Wao Ni Cedric

 

Hata hivyo, upekuzi wetu unatudhihirishia kwamba Cedrick na Paul ni mamoja.

Kakake mkubwa Paul pamoja na mke wake Janet wanasema hawajapata kumsikia kutoka kwake Paul tangu Julai.

Ikumbukwe kwamba Paul Manyasi alidondoka kutoka ndege ya KQ mnamo Julai 2, 2019.

Kwa Nini Ripoti Ya BBI Imecheleweshwa Kukabidhiwa Uhuru Na Raila?

Kulingana na mitandao yao kijamii, tulibaini haya:

(i) Alisomea chuo kikuu cha Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT).
(ii) Alienda shule ya upili Tande.

(iii)Anaishi Naiorbi South, Nairobi Area, Kenya.

(iv)Anatoka Kakamega.

Picha zilizotumiwa na Sky News zilimtambulisha Paul Manyasi kuwa sawa na picha za Cedrick zilizokuwa kwenye mtandao wa kijamii.

Hizi ni baadhi picha zake:

 

cedrick 1

cedrick 3

 

‘Nilifungwa Miaka Kumi Kwa Kupachika Mtoto Mimba,’ Jamaa Afichua

 

 

Jamaa ambaye aliyepita na shemeji yake alalamika kuchezwa pia 

Kuna msemo husema dunia duara. Msemo huu huashiria shepu ya dunia lakini maana yake ni kuwa hata uende wapi bado utarudi nyumbani.

Hata hivyo katika muktadha huu, natumia msemo huu kuashiria kuwa chochote umfanyiacho mwenzako siku moja kitarejea kwako kama adhabu.

Msemo huu autambuaye vyema ni jamaa kwa jina Sylvester, ambaye sasa amebakia na uchungu na machozi tele akilipia makosa au dhambi alizotekeleza siku za nyuma.

Akizungumza na Massawe Japanni kwenye kipindi cha Bustani la Massawe, jamaa huyu alifichua kuwa walitengana na mkewe baada ya kupatikana akimnyemelea dadake (shemeji yake).

Patanisho:Bwana akosana na shemeji!Je nani atamsaidia kuremjesha mke wake 

Alidai kuwa mkewe alimtenga naye akaamua kumuoa dadake na huku akidhani ameangukia dili nono hakujua kilichomngoja siku za usoni.

Sylvester ambaye ni dereva wa masafa marefu alipewa fununu kuwa mkewe huleta wanaume kwake kila anapoondoka. Siku moja alifunga safari na kurudi nyumbani na amini usiamini alimfumania mkewe na jamaa mwingine kwake.

Skiza usimulizi wake,

Nilioa dada ya mke wangu haki najuta sana, mke wangu alimleta kwa boma na tulikuwa tunaishi pamoja na ile tamaa ya mwanaume ikaniskuma.

Mke wangu alipojua aliniacha na nikamuoa dadake, sasa siku hizi nikiwa kazi zangu niliskia fununu kuwa kuna jamaa huja kwangu. Siku moja baada ya kurudi nilipata mwanaume kwa nyumba.

Mjue staa wako: Je, Tammy Abraham ni Nani?

Irene afunguka A-Z, usiri uliowekwa kwa kutoweka kwa Paul Manyasi

Aliyekuwa mpenzi wa Paul Manyasi amefunguka A-Z kumhusu.

Irene amesema kuwa Paul alipotea kazini na kuambiwa na msimamizi kuwa ibaki siri hadi arudi.

Irene anadaiwa kuwa mpenzi wake Paul.

Haya yanajiri huku shirika la ndege la Kenya Airways likikana taarifa za kuwa alikuwa akihudumu katika shirika hilo.

(+ Picha) Paul Manyasi aliyeanguka kutoka kwa ndege anga za London

‘Babake’ Isaac anakana kuwa kijana huyo ni mwanawe.

Kizungumkuti kinazingira swala nzima huku wazazi’ wakikataa ombi la kuendea mabaki ya mwili wa kijana huyo.

Kisa cha mwili wa Paul Manyasi kuanguka kutoka kwa ndege la shirika la KQ kiliwatia wengi hofu kubwa.

Kijana huyu anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kusafisha katika kampuni ya Colnet.

Mpenzi wake kwa jina Irene amefunguka kuhusu usuhuba wao.

Sio Citizen TV tena, Liondeh sasa anaotea nafasi ya katibu mkuu serikalini

“Nilimpenda tu jinsi alivyokuwa. Tulikuwa katika makubaliano kuwa itafika siku tuoane. Nahisi kuwa nilipoteza kipenzi cha roho…”

Kampuni hii ya Colnet ilikuwa katika kandarasi ya kudumisha usafi katika uwanja wa ndege wa KAA.

Mwanadada huyu kwa jina Irene alisimulia jinsi alivyojaribu kumpigia simu bila yeye kuipokea.

“Niliipiga simu yake ila sikumpata na ilikuwa imezimwa. Msimamizi wetu kazini alimuulizia akamkosa…” Alisimulia Irene

 

Ni mwisho wa Nasa, Raila Odinga awinda marafiki wapya

Muungano mpya unaandaliwa huku chama cha ODM kikitengana na vyama tanzu vya awali vilivyounda NASA.

Kinara wa chama cha ODM anatumia maafikio ya uchaguzi mdogo wa Kibra kusanifisha siasa zake za 2022, huku akitumai kwamba kufaulu kwa BBI kutaleta taswira mpya katika uchaguzi mkuu ujao.

Je Wajua Waweza Ishi Kwa Mda Mrefu Kwa Kuwa Mkarimu?

Waziri mkuu wa zamani akiongoza sherehe za kutoa shukran kwa wana Kibra alisema kwamba ushindi huo ni wa taifa nzima.

“Uchaguzi wa Kibra ni mfano kwa taifa nzima kuwa wakenya wana kiu ya mabadiliko,” Raila alisema.

Aliongeza kuwa,” Imetudhihirishia kuwa wakenya wamechoka na siasa potovu na ufisadi. Pia, imetufafanulia kwamba pesa hazitanunua kura.”

Kwa kile kinaonekana kuwa mkondo mpya katika siasa za nchi, kiongozi wa ODM aliwaorodhesha marafiki wapya, baadhi yao wakiwa mahasimu wake wa kitambo.

Kikundi chake kipya kinajumuisha wanachama kutoka Mlima Kenya, Ukambani na maeneo ya Bonde la Ufa.

Mojawapo ya windo kuu la Raila ni naibu wa gavana wa Kiambu James Nyoro ambaye wakati moja alikuwa mshauri katika ofisi ya Ruto kabla ya kuacha kazi hiyo 2015 na kuingia siasa.

Baadhi ya wanachama kutoka timu ya Kieleweke walionaswa kwenye kikosi kipya cha Raila ni mbunge Maina Kamanda, mbunge wa  Cherang’any Joshua Kuttuny na wabunge za zamani Dennis Waweru Dagoretti kusini na Kilemi Mwiria wa Tigania magharibi.

Itakuaje? Idah Odinga Na Lwam Bekele Wapewa Wiki Mbili Kusuluhisha Kesi

Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru, Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi, Beatrice Elachi, mwakilishi wa wanawake wa Wajir Fatuma Gedi miongoni mwa wengine.

Wote hao walishirikiana na chama cha ODM kwa kumpigia debe Imran Okoth huku wakimpuuza McDonald Mariga ambaye alikuwa akigombea kwa chama cha Jubilee.

Mbunge wa Chereng’any Joshua Kutuny anaibuka kuwa mfuasi mkubwa wa Raila katika Bonde la Ufa, eneo linaloaminika kuwa na uungwaji mkubwa wa naibu wa Rais Ruto.

Kutuny alikuwa miongoni mwa walioambatana na Raila Jumapili.

Kutoka eneo la magharibi mwa Kenya, Raila amenasa wabunge wawili kutoka chama cha ANC cha Musalia Mudavadi. Wawili hao ni mbunge mteule Godfrey Osotsi na seneta wa Kakamega Cleophas Malala.

Wawili hao walikuwa wakimuunga mkono mgombeaji wa chama cha ODM Imran Okoth huku wakimpuuza Eliud Owalo wa chama chao cha ANC.

Pia, juhudi za Raila zimemnasa viongozi wa Ukambani ambao ni Kalonzo, pamoja na magavana watatu-  Charity Ngilu, Kivutha Kibwana na Aflred Mutua.

Soma Jinsi Serikali Ya Misri Ilivyowaokoa Harambee Stars Mjini Cairo

 

 

 

Kwa nini ripoti ya BBI imecheleweshwa kukabidhiwa Uhuru na Raila?

Shajara ya rais Uhuru Kenyatta juma hili inaonesha kwamba shughuli chungu nzima imeratibiwa na nafasi ya kukabidhiwa ripoti ya BBI ni finyu.

Kumekuwa na wingu la matarajio kwamba rais pamoja na kinara wa ODM Raila Odinga wangekabidhiwa ripoti ya BBI juma hili baada ya kukamilika kwa uchaguzi mdogo wa Kibra Ijumaa iliyopita.

Tume ya maridhiano na uwiano ilikamilisha kuandika mapendekezo majuma matatu yaliyopita, huku wakisema kwamba ‘ripoti itakabdihiwa nafasi itakapopatikana.’

“Tayari tumewasiliana na afisi ya rais kwamba mapendekezo ya BBI yako tayati kukabidhiwa rais,” ujumbe uliotiwa saini na Paul Mwangi na mwenzake Martin Kimani ulisoma.

Kucheleweshwa kwa ripoti hiyo kukabidhiwa viongozi hao wawili kumewadia kipindi ambacho kuna tetezi kwamba baadhi ya mapendekezo kwenye ripoti hiyo ‘yanafaa kufutiliwa mbali.’

Kulingana na taarifa kutoka baadhi ya waliochangia ripoti hiyo, inasema kwamba baadhi ya mapendekezo yanatathminiwa kwa kuwa yataleta mgawanyiko zaidi kwenye serikali.

Nilifungwa Miaka Kumi Kwa Kupachika Mtoto Mimba,’ Jamaa Afichua

Tayari viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya wameonya kupinga mapendekezo hayo iwapo yatapendekeza rais kuchaguliwa bungeni kinyume na ilivyo sasa ambapo rais huchaguliwa na wakenya kwa njia ya kura.

Kulingana na hali ilivyo sasa, rais anamsururu wa makongamano na warsha kadhaa ikiwemo kukutana na wajumbe waliohudhuria kongamano la ICPD25 linaloendelea.

Alhamisi asubuhi, rais Uhuru anatarajiwa kukutana na waziri wa masuala ya kigeni wa Jamhuri ya Czech Thomes Petrricek.

Mnamo Ijumaa, rais anatarajiwa katika uzinduzi wa mkutano wa kanda kuhusu ajira kwa vijana.

‘Nilifungwa Miaka Kumi Kwa Kupachika Mtoto Mimba,’ Jamaa Afichua

+ Picha ) Alichokibeba Paul Manyasi katika ‘safari’ ya ndege, jina lake la msimbo

Paul Manyasi alikuwa amejihami na vitu kama chupa ya soda, maji ya kukata kiu na mfuko ambao aliubeba katika ‘safari’ yake ya kuzuru Uingereza.

Mwili wa kijana huyu wa Kakamega ulianguka katika shamba la maua ndege ilipochomoa magurudumu kutua Juni 30 nchini Uingereza.

(+ Picha) Paul Manyasi aliyeanguka kutoka kwa ndege anga za London

_109639193_b696922f-fb6e-4ebd-a633-341cabd63409

Marafiki wamesema kuwa jina la utani la Paul Manyasi lilikuwa MCA (Member of County Assembly).

Je, huenda ikawa Paul Manyasi alikuwa na nia ya kuwa mwakilishi wodi?

Tukio la jana la aliyekisiwa kuwa babake kijana huyu Mzee Isaac Munyasi kumkataa limefanya swala hili kuwa ngumu zaidi.

Shirika la habari la Sky News linachunguza kwa makini kubaini wazazi wake Paul.

Sio Citizen TV tena, Liondeh sasa anaotea nafasi ya katibu mkuu serikalini

‘Baba’ huyu alisema kuwa huyo sio mtoto wake.

_109639194_b4131492-33c4-4135-a4f9-5de852891870

Anahisi kuwa mwanawe bado yupo hai.

Alisema kuwa mwanawe anaitwa Cedric Shivonje na atazamia jiji la Nairobi kumtafuta.

Iwapo atamkosa mwanawe basi itabidi DNA au vinasaba kufanyika ili kubaini ukweli.

Kisa cha mwili wa Paul Manyasi kuanguka kutoka kwa ndege la shirika la KQ Juni 30 kiliwatia wengi hofu kubwa.

 Kijana huyu anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kusafisha katika kampuni ya Colnet.

Kampuni hii ya Colnet ilikuwa katika kandarasi ya kudumisha usafi katika uwanja wa ndege wa JKIA taarifa na ambazo shirika hili limekataa.

 

 

 

Soma jinsi serikali ya Misri ilivyowaokoa Harambee Stars mjini Cairo

Serikali ya Misri iliwaokoa Harambee Stars waliokua nusura wafurushwe kutoka kwa hoteli yao jijini Cairo kutokana na kutolipwa kwa ada.

Stars wako jijini humo kwa mechi yao ya kufuzu kwa AFCON ya kundi G dhidi ya the Pharaohs leo usiku. Rais wa FKF Nick Mwendwa ameilaumu serikali kwa hali hio ambayo anasema inatishia kusambaratisha mechi yao dhidi ya Misri.

Serikali hata hivyo kupitia kwa katibu wa michezo Kirimi Kaberia ilirushia lawama FKF huku Kaberia akisema hawakuipa serikali taarifa muhimu na kuwa walitaka kupewa pesa taslim.

Harambee Starlets wamewasili salama nchini Tanzania kabla ya kipute cha ubingwa wa kinadada cha CECAFA mwaka 2019 kinachopangiwa kuanza jumamosi.

Hii ni siku moja tu baada ya kinadada hao kuwasili nchini kutoka Zambia ambapo walibanduliwa nje ya michuano ya kufuzu kwa olimpiki ya bara mwaka 2020 na She Polopolo.

Starlets wanatumai kushinda taji hilo ambalo limekua likiwaponyoka katika miaka ya hivi majuzi, watakapoanza kampeni yao dhidi ya Ethiopia jumapili tarehe 17.

Meneja wa Uingereza Gareth Southgate anasema hatasita kumchagua kiungo Raheem Sterling kwa mechi ya jumapili ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 huko Kosovo.

Sterling alichujwa kutoka kwa mechi ya leo baada ya kulumbana na mwenzake Joe Gomez. Uingereza inahitaji alama moja tu dhidi ya Montenegro ili kufuzu. Sterling anayechezea Manchester City Sterling atacheza mechi ya jumapili huko Kosovo.

Wing’a wa Chelsea Callum Hudson-Odoi anasema aliongea na meneja Frank Lampard kumshawishi asalie Stamford Bridge. Kinda huyo wa miaka 19 aliwasilisha ombi la kutaka kuhama mwezi Januari baada ya Chelsea kukataa ofa ya pauni milioni 35 kutoka kwa Bayern Munich.

Hata hivyo Odoi amemfurahisha Lampard aliyechukua uskani msimu wa joto. Odoi atakosa mechi za msimu huu baada ya kupata jeraha la mguu alipokua akicheza katika mechi yao dhidi ya Burnley mwezi Aprili.

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaregea katika ulingo wa soka baada ya kukubali kuwa mkuu wa ukuzaji soka duniani wa FIFA. Hatua hii inamaliza uvumi uliomhusisha mfaransa huyo na kurudi kama meneja wa Bayern Munich.

Wenger aliondoka Gunners Mei mwaka 2018, baada ya miaka 22 mamlakani. Wadhfa wake mpya utasaidia kukuza soka ya kinadada na wanaume na vilevile masuala ya kiufundi.

 

PATANISHO: Mume wangu hupea wanawake simu wanitusi

Mercy, mwenye umri wa miaka 26, ndiye aliyeomba kupatanishwa na mumewe bwana Kevo akidai ameshindwa na ndoa yake na anafikiria kujitia kitanzi.

Alipoulizwa mbona kapata mawazo yale, Mercy alisema,

PATANISHO: Nimebaki nikichekwa na Jamaa aliyeninyang’anya mke

“Yaani nimefika mwisho kwani hadi mume wamgu hupea mama mwingine simu anitusi. Mimi nilikuwa nimekubali kuishi ushago huku yeye akiwa Eldoret. Na nikizungumza naye ananiambia kuwa ni mwanadada alichukua simu yake bila yeye kufahamu.
Kulingana na Mercy, cha kushtua ni kuwa yule mama ambaye humtusi anajua siri zao zote ikiwa mipango yake ya ujenzi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka saba na wamejaliwa watoto wawili ambao wanaishi na mama yao.

Nimevumilia Sana Kwani hata mwaka wa 2015 kuna mama ambaye amezaa naye alinitusi kuwa sijasoma na sipaswi kuwa naye.” Aliongeza Mercy.

PATANISHO: Nilikuwa nalala na kisu kitandani kwa raha zangu

Anasema licha yao kukosana, Kevo alikuwa anashughulikia watoto.

Hata hivyo, hatukuweza kuwapatanisha wawili hawa kwani bwana Kevo hakujibu simu yetu.