Ilikuwaje: Mamangu mzazi alinitekeleza na kumpendelea dadangu

Mama mmoja ameelezea jinsi mamaye mzazi alivyomtekeleza maishani mwake akiwa katika shule ya msingi huku kisa na maana ikiwa ni kushindwa kufanya vyema shuleni. Doreen kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja na anaishi mjini Nairobi kwenye harakati za kumtaftia mwanawe riziki.

“Tulizaliwa tukiwa wasichana wawili. Mamangu alikuwa anapenda dadangu mdogo kuniliko kwa sababu alikuwa mwerevu darasani. Mama aliakuwa ananidharau sana hadi kiasi kwamba aliacha kunilipia karo shuleni.”

Doreen amelezea Masawe Japani kuwa mamaye alikataa kumlipia karo ya shule jambo lilompea mawazo mengi maishani. Baba yake doreen na mama yake walitalikiana akiwa mdogo hivyo mamake ndio alikuwa mlezi wa kipekee.

“Niliamua kumwitisha baba karo baada ya mama kukataa kunilipia ila baba alinituma kwa mama nimuulize kama anakubali baba anilipie karo. Nilimbebeleza mama akubali nilipiwe karo ila alikataa na kusema kuwa haina haja kuharibu pesa kwa watoto wajinga shuleni.”

Ukali wake mamaye ulimpelekea Doreen kumuuliza mamaye mzazi iwapo yeye alikuwa mmoja wa watoto wake.” Baba na mama walirudiana na nilipowauliza kuhusu hatma yangu shuleni walikata hadi mama akaniambia mimi ni wale watoto hufanya mapenzi na baba zao jambo lililoniudhi sana moyoni mwangu.”

Kutokana na matatizo haya, Doreen alianza kufanya kazi ya vibarua ili aweze kupata pesa za karo yake huku dadake mdogo alikuwa analipiwa karo na wazazi wao. Doreen alimaliza darasa la nane akiwa na umri wa miaka kumi na minane huku dadaye alikuwa tayari amekamilisha masomo ya shule ya msingi na alikuwa katika shule ya upili.

” Baada ya miaka kadha ilinibidi niolewe ili niweze kukidhi mahitaji yangu. Niliachia masomo baada ya kumaliza shule ya msingi ila dadangu alilipiwa karo hadi akamiliza kidato cha nne. Hata hivyo,ndoa yangu haikukawia sana kwani ilivunjika na nilipozungumza na mama aliniambia nisimpelekee mtoto kwake.”

Kwa sasa Doreen ni anaishi hapa mjini Nairobi na jambo kubwa yeye hushirikiana na mamaye mzazi ni salamu pekee kwani hadi leo hii mamaye hampendi kamwe.

 

John De Mathew aaga dunia kutokana na ajali ya barabarani

John Demathew aliaga dunia baada ya kupata ajali ya barabarani katika eneo la Bleu Post thika asubuhi ya kuamkia jumatatu. De mathew alikuwa mwanamziki wa nyimbo za lugha ya kikuyu na anajulikana kwa wimbo wake, ‘Njata yakwa’ uliomhusisha mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Murang’a Sabina Chege.

th

Wakenya wamezidi kuomboleza kifo chake Demathew huku wengi wakituma risala za rambirambi kwa familia yake.

 

For this world wasn’t our home shine on your on your way home where we all belong #RIPDemathew #RIPJohnDeMathew

Phillipe Coutinho akamilisha uhamisho kwenda Bayern Munich ya Ujerumani

Phillipe Coutinho ameamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani akitokea Barcelona ya Uhispania kwa msimu mmoja.

Bayern inatarajiwa kulipa dhamani ya millioni nane kwa msimu huu huku pia kukiwa na uwezekano wa kumnunua Coutinho kwa ada ya millioni mia moja na ishirini msimu ujao.

Philippe Coutinho
Philipe

Siendi ng’o!: Alexis Sanchez akiri hataondoka Man United

 Phill Coutinho alijiunga na Barcelona mwezi januari mwaka 2018 akitokea klabu ya Liverpool kwa ada ya millioni mia moja na arubaini na mbili.
Ndani ya mwaka mmoja na nusu ugani Camp Nou,Coutinho alicheka na wavu mara 21 ndani ya mechi 75. Ujio wake Antoine Griezmann umekuwa sababu kuu kwa uhamisho wake Coutinho.
 Mario-Balotelli_3266736 (1)
Kwingineko ni kuwa aliyekuwa mshambulizi wa AC Milan na Manchester City, Mario Balotelli amejiunga na klabu ya Brescia kwa mkataba wa miaka miwili.
Balotelli mwenye umri wa miaka 28 anatarajiwa kuisaidia klabu hio kufanya vyema msimu ujao kwenye ligi kuu nchini italia.
Soma mengi hapa

 

Mashabiki wa AFC Leopards wazidi kumwoboleza Felix Shitsama

Kakamega fraternity of AFC Leopards is mourning the death of former club vice chairman Felix Shitsama who perished in a road accident on Friday.

Felix Shitsama, Right: car wreckage

Wakaazi wa kakamega na mashabiki wa klabu ya AFC Leopards wanaendelea kumwomboleza aliyekuwa naibu rais wa klabu hio, Felix Shitsama aliyeiaga dunia siku ya Ijumaa baada ya kupata ajali ya barabara katika eneo la Timboroa. Felix alikuwa anaelekea mjini Malava  akiwa na maarafiki zake kwa ajili ya matanga ya mmoja wa wanafamilia wake.

Mwanamke amuua mumewe kwa kumdunga kisu Eldoret

 “Nipigo kubwa sana kwetu sisi kama klabu na familia ya AFC Leopards. Felix alikuwa kijana aliyejitolea sana na kila jambo alilohusika nalo. Shitsama atabaki kuwa kwenye viyabu vya kumbukumbu vya klabu ya  Leopards uaminifu wake kwetu sisi,” mwenyekiti wa Leopards, Dan shikanda alisema.

Shitsama alichaguliwa na kama naibu wa rais wa klabu ya AFC Leopards mwaka wa 2016 chini ya uongozi wake Dan Mule. Shitsama anakubukwa kwa kufadhilisha dili baina ya klabu ya AFC Leopards na kampuni ya Umbro inayotengeza jezi zao kwa sasa.

“Wakati mwingine, Felix alikuwa anawatia motisha wachezaji akiwa peke yake pamoja na kuwaleta wachezaji wapya wanaoisaidia Leopards kwa sasa.”

Juzi jumapili,Klabu ya AFC Leopards iliita mashabiki wote ili wamwelekezee Mola matatizo yao. Kulingana naye Dan Shikanda, klabu hio iliamua kumwomba mwenyezi mungu usaidizi ili iweze kujikomboa na majinamzi yanayo iadama kwa sasa.

SOMA MENGI HAPA

Susumila ajibu madai kuwa majini hayaandiki nyimbo

Susumila amerejea na kuwajibu wanaomkashifu kwa madai kuwa yeye anatumia ushirikina ili kufadhilisha muziki wake pamoja na biashara zake.Susumila ambaye kwa sasa anataba na kibao, “Warembo” amekanusha madai yote yanayo muhusisha na utumizi wa Majini kwa kusema kuwa majini hayawezi andika nyimbo.

ytekdgz5pknajipeni57c92f324b6e1

Joyce Omondi na Waihiga wafichua mbona uhusiano wao ulikuwa siri kuu

“Nimelisikia hilo kwa muda mrefu sasa ila ningependa watu wajue kuwa majini ama nguvu za ushirikina huwa haziandiki mishororo ya mashairi au nyimbo.”

“Wimbo wangu mpya una hisia tamu hasa ukisikiliza mishororo yenyewe kwa udani. Madai hayo yote najua yanatolewa na maadui wangu wanaopania kunikwaza kila wakati na katika kila jambo nifanyalo maishani mwangu.”

Susumila hata hivyo aliwahimiza wanaoeneza uvumi kumuhusu waendelee tu kwani yeye hatowajali na atazidi kuimarisha maisha yake.” Najua pia watasema kuwa nimeedelea kimaisha kwa sababu gavana wa Mombasa, Hassan Joho alinisaidia ila mimi nasema kuwa ni sawa tu kwani lazima mambo kama haya yatokee.”

SOMA MENGI HAPA

Patanisho: Aliambiwa kuwa mimi navuta bangi kisha akenda kwao

Bwana Jared aliomba apatanishwe na mkewe Grace baada ya ndoa ya wawili hao kuvunjika mwezi Mwachi mwaka huu wakati Mama Ariet alipofunganya virago vyake na kurejea kwao kufuatia madai kuwa Jared alikuwa mlaguzi wa bangi.

story za ghost

“Nilikuwa nalewa na kurudi nyumbani saa mbili usiku. Nilikuwa naingia kazini saa kumi na mbili asubuhi na kutoka saa mbili usiku jambo lilofanya nikose wakati wa kushiriki na mke wangu. Mama Ariet nilimwoa akiwa na mtoto na ndoa yetu ilidumu kwa muda wa miezi sita pekee. Hata hivyo, aliambiwa kuwa mimi nilikuwa navuta bangi na marafiki zake na akakubali kisha akenda kwao.”

Mama Ariet ambaye aliolewa akiwa na mtoto mmoja alisema kuwa mumewe alikuwa na mazoea ya kulewa sana hivyo yeye aliamua kumwacha aendele na pombe yake.

PATANISHO: Nimemwambia nampenda kwani ni wimbo!

“Najua kuwa alikuwa anatumia mihadarati.Na mimi nilimwonya akakataa kuniskia sasa nikamwacha. Alikuja kwetu akambiwa na wazazi wangu ila akasema yeye atazidi kukunywa busaa.”

Mama Ariet alikataa kumrudia baba ariet na kusema kuwa ameendelea na maisha yake.

“Mimi nimerudi kwa bwanagu wa kwanza na hivo nimeshaolewa. Jared endelea na mambo yako kwa sababu mimi nimekusahau kwa sasa.”

“Haya ni magumu ila ningependa ufikirie tena kwa sababu mimi bado nakupenda sana na hata miaka kumi ijayo bado ntakuwa nakupenda,” Jared alisema baada ya mama Ariet kusema kuwa hawezi kurudi kwake na tena kuongeza kuwa alikuwa amerudiana na babaye Ariet tena.

SOMA MENGI HAPA

Siendi ng’o!: Alexis Sanchez akiri hataondoka Man United

Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, amekataa uhamisho wa kuelekea Roma, licha ya klabu hiyo ya Old Traford kukubali kulipa kitita kikubwa cha mshahara wake wa £560k kwa wiki.{Mirror)

Hatahivyo Sanchez huenda akaelekea katika ligi ya serie A baada ya Man United kumruhusu kufanya mazungumzo na Inter Milan, ambapo huenda akakubali kupunguza mshahara wake. (Mail)

Liverpool huenda ikafaidika na £18m iwapo mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo na raia wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ataelekea Bayern Munich kwa mkopo. (Mail).

Everton imetoa ofa ya kumsaini winga wa Ufaransa Franck Ribery, 36, ambaye yupo huru baada ya kuondoka Bayern Munich baada ya kuhudumu kwa miaka 12 katika klabu hiyo ambayo ndio mabingwa wa ligi ya Bundesliga . (90Min)

Kwengineko, Kiungo wa kati wa Portugal Renato Sanches, 21, anataka kuondoka Bayern kwa kukosa muda wa kucheza katika klabu hiyo. (Sport1 – in German).

Mesut Ozil

Mesut Ozil, 30, huenda akaondoka Arsenal na kujiunga na klabu ya DC United iwapo klabu hiyo ya ligi ya MLS inaweza kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumani kuhamia Washington. (Star)

Beki wa kulia wa Ivory Coast Serge Aurier, 26, huenda akaondoka Tottenham na kuelekea AC Milan iwapo beki wa timu hiyo Andrea Conti, 25, ataondoka ligi ya Serie A kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la Ulaya. (Calciomercato)

Na mchezaji wa Everton Yannick Bolasie, 30, yuko tayari kurudi katika uwanja wa Goodison Park, huku klabu za Uturuki Besiktas na Trabzonspor zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Congo . (Sun)

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli, 29, anakaribia kujiunga na klabu ya Serie A Brescia. (Sun via La Gazzetta)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, hakuorodheshwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Rennes kutokana na jeraha na sio kwamba raia huyo wa Brazil anataka kurudi Barcelona. (AS – in Spanish)

Mshambuliaji wa Barcelona Kevin-Prince Boateng, 32, amefichua ni kwa nini Sir Alex Ferguson hakumsajili kujiunga na Manchester United mapema wakati wa kipindi chake cha mchezo. (Goal)

-bbc

Mwanamke amuua mumewe kwa kumdunga kisu Eldoret

Polisi mjini Eldoret wamemkamata mwanamke aliyemdunga mumewe kwa kisu na kumuua jana usiku katika mtaa wa Shauri Estate, mjini Eldoret.

Marehemu alikuwa dereva wa teksi na alifika nyumbani usiku wa manane alipotoka kazini, baadaye wawili hao walianza ugomvi kuhusu ujumbe aliopokea na hapo vita vikaibuka dhidi yao wawili.

Jirani yao, bi Pauline Kibe alisema kuwa waliskia ugomvi na mayowe ndani kutoka kwa nyumba hiyo lakini juhudi za kumuokoa jamaa huyo hazikufua dafu kwani alifariki papo hapo baada ya kudungwa kisu kifuani.

Polisi waliofika eneo hilo la tukio walianzisha uchunguzi na wakaupeleka mwili katika chumba cha kuhifadhia mauti cha hospitali ya Moi.

Hayo yakijiri,

Wizara ya afya katika kaunti ya Taita Taveta itawapa ajira za kudumu zaidi ya wahudumu wa afya 200 wanaohudumu kwa kandarasi ili kukabili changamoto ya uhaba wa wahudumu. 

Waziri wa afya kaunti hiyo Daniel Makoko anasema huduma ya afya ina upungufu wa wahudumu 400 huku akilitaja swala hilo kama changamoto kubwa katika kutoa huduma kwa wakazi.

Anasema wahudumu wengi wa afya wanashawishika kuhamia kaunti zinazotokana ajira ya kudumu na jivyo kusababisha uhaba katika kaunti hiyo.

TANZIA: Mlipuko wa bomu waua watu 63 harusini

Bomu limelipuka katika ukumbi wa harusi katika mji mkuu wa Afghanistan , Kabul na kuwaua takriban watu 63 na kuwajeruhi zaidi ya 180.

Walioshuhudia waliambia BBC kwamba mlipuaji wa kujitolea muhanga alijilipua wakati wa sherehe hiyo ya harusi.

Mlipuko huo ulitokea mwendo wa saa nne na dakika 40 saa za Afghanistan katika eneo lililopo magharibi mwa mji ulio na rai wengi Waislamu wa dhehebu la Kishia.

Kundi la Taliban limekana kwamba ndilo lililohusika na shambulio hilo. Hakuna kundi jingine lolote lililokiri kutekeleza shambulio hilo.

Wapiganaji wa Kiislamu kutoka Dhehebu la Sunni , ikiwemo Taliban na kundi la wapiganaji wa Islamic State mara kwa mara wamekuwa wakiwalenga Waislamu wa Hazara wa dhehebu la Shia walio wachache nchini Afghanistan na Pakistan.

Ni nini tunachojua?

Waziri wa maswala ndani nchini Afghanistan amethibitisha vifo hivyo saa chache baada ya bomu hilo kulipuka .

Picha zilizosambazwa katika mitamndao ya kijamii zilionyesha miili ikiwa imetapakaa huku viti na meza zikiwa zimependukia.

Harusi za Afghanistan huruhusu mamia ya wageni ambao hukongamana katika kumbi kubwa ambapo wanaume hutengwa na wanawake na watoto.

Mgeni mmoja kwa jina Mohammad Farhag alisema kwamba alikuwa katika eneo la wanawake wakati aliposikia mlipuko mkubwa katika eneo la wanaume .

”Kila mtu alikimbia nje akipiga kelele na kulia”, aliambia chombo cha habari cha AFP.

”Kwa takriban dakika 20 ukumbi huo ulikuwa umejaa moshi . Karibu kila mtu katika eneo la wanaume ni aidha wamekufa au kujeruhiwa. Sasa saa mbili baada ya mlipuko , wanaendelea kutoa miili ndani ya ukumbi huo”.

Muhudumu mmoja wa chakula , Sayed Agha Shah alisema kwamba kila mtu alikuwa akikimbia baada ya mlipuko huo.

”Wahudumu wetu kadhaa walifariki ama kujeruhiwa”, aliongezea. Msemaji wa Taliban alisema kuwa kundi hilo linashutumu shambulio hilo.

”Hakuna haki ya shambulio la kusudi kama hilo na mauaji ya kiholela yaliowalenga wanawake na watoto”, Zabiullah Mujaheed alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Nini kilichotokea awali?

Mlipuko huo unajiri siku 10 baada ya bomu kubwa kulipuka nje ya kituo cha polisi cha Kabul na kuwaua watu 14 huku 150 wakijeruhiwa.

Kundi la Taliban limesema kuwa lilitekeleza shambulio hilo.

Siku ya Ijumaa ndugu mmoja wa kiongozi wa Taliban Hibatullah Akhundzada aliuawa kutokana na bomu lililotegwa ndani ya msikiti karibu na mji wa Pakistan wa Quetta.

Hakuna kundi lolote kufikia sasa lililokiri kutekeleza shambulio hilo.

Duru za kijasusi kutoka Afghanistan zinadaiwa kukaribia kutangaza makubaliano ya amani.

-bbc

KISUMU: Meneja wa hoteli amuua mwanaume kwa kumpiga risasi

Mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa mjini Kisumu siku ya Jumamosi.

Peter Otieno Ogallo alipigwa risasi tatu kifuani na Daniel Yona Jaoko, meneja wa hoteli ya Ray Green mjini Nyamasaria.

Otieno ambaye ni meneja wa Coast Bus tawi la Kisumu, alipigwa risasi mbele ya familia yake na akakimbizwa katika hospitali ya Avenue ambapo alifariki.

Jaoko alikuwa tu amemfikisha mpenziwe Vivian Achieng Meresa ambaye anaishi mtaa moja na marehemu wakati wa kisa hicho cha saa kumi na moja asubuhi katika  eneo la Polyview.

Kamishna wa polisi wa kaunti ya Kisumu Benson Maweu alisema kuwa Jaoko na Vivian wametiwa mbaroni kuhusiana na mauaji hayo.

Maweu alisema kuwa marehemu alipigwa risasi akijaribu kuondoa gari lake la Nissan matatu la usajili KCU 552X ambapo lilikuwa limeegezwa.

Gari la Otieno lilikuwa limezibwa na gari lingine la aina ya Jeep la usajili KCC 422T. “Alipomkaribia Jaoko kumpisha apite ili aondoe gari lake, lakini badala atoe gari alitoa bastola na kumpiga risasi.” Alisema Maweu.

Maweu aliambia The Star kupitia simu kuwa risasi mbili ziliingia katika upande wa kushoto wa kifua cha Otieno na kuharibu mapafu yake.

Washukiwa hao wamezuiwa katika kituo cha polisi cha Kondele. Mkuu wapolisi alisema kuwa swala hilo bado linachunguzwa.

“Tutawafikisha kortini pindi tu uchunguzi utakapo kamilika.” Aliongeza.

Maweu alisema kuwa walipata bunduki aina ya Ceska lenye risasi 15 walipo wakamata washukiwa hao wawili huku risasi zingine 42 zikipatikana nyumbani kwake Jaoko.