Kagia ameninyima nafasi ya kuwaona watoto wangu – JB Masanduku

JB Masanduku amedai kuwa amenyimwa nafasi ya kuwaona watoto wake na aliyekuwa mkewe Tina Kagia. Kagia na Masanduku walifunga ndoa mwaka wa 2014 kwenye chemba ya Jaji.

Masanduku amesema kuwa penzi hilo lilimwadhiri hadi kwenye taaluma yake ya Muziki.

masanduku (2)

“Hii ndio sababu niliacha kufanya tasnia ya ucheshi kwani nilikosa sababu ya kuwafurahisha wengine ilihali mimi mwenyewe sina furaha.” Masanduku alisema.

“Tulipeana talaka kwa amani tu na mimi namshukuru mungu kwa kuwa alikuwa na utu uzima kwenye wakati huo wote. Hata hivyo, Talaka ni jambo mbaya sana.”

Hayawi hayawi huwa: Majesty Bahati azaliwa

“Tangu tuachane sijawahi pewa ruhusa ya kuwaona watoto wangu hata mara moja ila bado mimi nawapa usaidizi wa baba. Jambo hili limenidhuru na ndio sababu nimekuwa sifanyi shoo ila nashukuru mungu kwa kuwa yeye yu mwema.” Jambo hilo anasema kuwa limemwadhiri kimawazo sana  kwani hata Kagia mwenyewe hapendi kumwongelesha.

JB Masanduku amewapa ujumbe wazazi wanao wanyima waenzao nafasi ya kuwaona wanao.” Mtoto atazidi kukua na akifikisha umri wa miaka 18 atakuwa na dai la kutaka kumwona babaye na hivyo atajua tu kuwa ni mamaye alimyima hio nafasi na hilo jambo sio jambo nzuri.”

Pamoja na hayo, Masandukuhakutaja sababu inayomfanya Kagia kumyima nafasi ya kuwaona wanawe wawili.

Soma mengi hapa

 

Timu tano za kuangazia msimu ujao ligi kuu Uhispania

Laliga Santander inatarajiwa kung’oa nang’a hii leo huku mechi ya kwanza ikiwa baina ya bingwa mtetezi Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao.

Kwa muda sasa klabu ya Barcelona imekuwa ikitawala ligi hio huku Lionel Messi akiwakosesha usingizi mabeki pamoja na walinda lango wa timu pinzani. Hata hivyo, Vilabu vingine vimekuwa na biashara za kufana sana na huenda vikaletea mabingwa hao wakati mgumu msimu huu.

Atletico Madrid

atletico.madrid

Ronaldo kuwania tuzo la mchezaji bora dhidi ya Messi na Van Dijk

Bingwa wa mwaka 2014, Atletico Madrid ilimsajili kinda wa miaka kumi na tisa, Joao Felix kutoka klabu ya Benfica na sasa kinda huyu anatarajiwa kuendeleza ukali wake nchini Uhispania.
Pamoja naye, klabu hio ya uhispania ilinunua wachezaji saba wapya huku Kocha wao Diego Simeone akisema kuwa anataka kubadilisha aina ya mchezo wake. Atletico huenda ikarejelea makali yake ya msimu wa 2013/2014 ilipotwaa taji la Laliga.

Real Madrid

real.madrid

Zinedine Zidane amemsajili kiungo mshambulizi wa Chelsea, Eden Hazard ili aweze kumsaidia kungangania taji la ligi kuu nchini Uhispania.

Hazard anatarajiwa kurudisha furaha mioyoni mwa wapenzi wa klabu ya Real Madrid msimu huu haswa baada ya kukosekanana mfungaji wa kutegemewa msimu uliopita.

Zidane amefanya sajili nne kufikia sasa na huenda akamsajili Neymar kabla dirisha la Uhamisho halijakamilika.

Villareal

villareal\

Mastaa waliovunja uhusiano wao na klabu zao kimabavu

Santiago Carzola amerejea na raundi hii anakiwasha kama moto. Msimu uliopita kiungo huyu alianza akiwa majeruhi ila baada ya kurejea mwezi Januari kiungo huyu alipika magoli sita huku akicheka na wavu mara nne.
Villareal huenda ikaletea uchangamfu mwingi msimu ujao baada ya kuonyesha makali mwishoni mwa msimu uliopita.

Barcelona

valencia-cf-v-fc-barcelona-la-liga

Mkurugezi mkuu wa Barcelona Josep Martina aliweka wazi matamanio ya kuona klabu yake ikimaliza msimu kama haijapoteza mchezo hata mmoja.

Barcelona imemsajili Antoinne Griezmann pamoja na Frankie De Jong kuongeza kwenye kikosi cha Barcelona. Msimu uliopita Barcelona ilipoteza michuano mitatu pekee na sasa wanaazimia kuimarisha rekodi hio. Je wataweza?

Sevilla

sevilla

Sevilla imemleta aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania, Julen Lopetegui na sasa anatarajiwa kuleta ushindani mkali msimu ikizingatiwa kwamba alifukuzwa kazi msimu uliopita na klabu ya Real Madrid.

Hata hivyo, Usajili wake Rony Lopez, Luuke De Jong pamoja na Olivier Torres inatarajiwa kuongeza ushindani kwenye ligi kuu Uhispania msimu ujao.

Soma Mengi Hapa

 

Ghost na Arocho wapanga kukuza vijana kupitia kadanda

Watangazaji wa Radio Jambo, Fred Arocho na Jacob ‘Ghost’ Mulee ni miongoni mwa watangazaji ambao taaluma zao za uanahabari zimejengwa kwa msingi wa kadanda.

Kwa mfano, Afrika mzima, yajua kuwa Ghost Mulee ni mmoja wa makocha maahiri na humu nchini anatambulika kama gwiji kwa ujuzi na mafanikio aliyoletea nchi hii.

PICHA: Mwanawe Arocho asafiri hadi China kwa mafunzo ya soka

Arocho ama ukipenda ‘Twiga’ pia anaheshimika nchini kwa mchango wake kama mchezaji, enzi zile na hata pia ndani na nje ya uwanja na studioni, ambapo anatetea maswala ya wachezaji.

Pamoja, wawili hao wameshirikiana ili kukuza talanta na isitoshe, ni mpango wao kuonesha fahari yao kwa Nairobi na haswa Eastlands, mtaa ambao walilelewa.

Moja wapo ya mipango wao ni kuandaa shindano la kadanda la wachezaji 11 kila upande, shindano ambalo litaleta pamoja timu nane kutoka mitaa tofauti ya Nairobi.

Shindano hili ambalo limedhaminiwa na OdiBets, ni la siku moja, linafanyika hii leo katika uga wa Camp Toyoyo, Jericho.

Isitoshe, wawili hao wameshirikiana na ajenti kadhaa kutoka Sweden wakiwemo; Patrick Murk na Johan Sandohl na pia Jamal Ibrahim, ambao watakuwa wakitafuta talanta ambazo watakuza.

Story za Ghost: Jamaa atoroka hotelini alipomuona DCI Kinoti

“Ghost Mulee nami tulileta vichwa vyetu pamoja kama watu walioanzia Eastlands, watu ambao walipata fursa ya kucheza kadanda na kufika tulipo. Sasa tunataka kupatia wengine fursa kama ile ili wajikuze.” Alisema Arocho.

Aliongeza,

Tumechukua timu nane kutoka Nairobi kote ambazo ndio timu bora kabisa Nairobi ili waoneshe talanta zao. Na wakibahatika watajipata bara Uropa. Shindano lile litaanzia robo fainali, kisha nusu fainali hadi fainali.”

Shindano hilo liitwalo ‘Champions of champions’ tayari limeanza na litakamilika saa kumi na moja jioni.

Washindi watazawadiwa kitita cha elfu 50,000 huku watakaopoteza katika fainali watapokea elfu 20,000.

 

Kizaazaa baada ya meno bandia kukwama katika koo la mgonjwa

Mgonjwa mmoja amepatikana meno bandia yaliokwama kwenye koo lake siku nane baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

Mtu huyo wa miaka 72 alilalamika kuwa na tatizo la kumeza chochote na kwamba anakohoa damu kabla ya madaktari kugundua amemeza meno bandia.

Alirudi hospitali mara kadhaa, kufanyiwa upasuaji mwingine na hata kuongezewa damu ili kurekebisha hitilafu hiyo ya kimatibabu.

Pombe inawapotezea muda na pesa zenu; Frasha awambia walevi

Hospitali ya Chuo Kikuu cha Paget mjini Norfolk, nchini Uingereza wamesema kuwa wamefanyia marekebisho utaratibu wa kumkagua mgonjwa kabla ya kufanyiwa upasuaji.

Kisa cha mwanamume huyo kimechapishwa katika ripoti ya jarida la BMJ, ambayo waandishi wake wamependekeza mgonjwa atolewe meno bandia kabla ya kudungwa sindano ya kufisha ganzi mwili mzima.

Siku sita baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe tumboni mwake, mtu huyo alirudi katika hospitali hiyo kuwafahamisha madaktari alikuwa na tatizo la kumeza chakula.

Picha ya Xray ya koo

Nina uhakika Ozil na Kolasinac wako tayari kucheza – Unai Emery

Madaktari katika hospitali ya Gorleston nchini Uingereza wanaamini ilikuwa maabukizi ya mfumo wa kupumua kutokana na athari ya kuwekewa mipira kooni wakati wa kufanyiwa upasuaji, na kumuandikia dawa aina ya antibaiotiki na steroids.

Lakini mwanamume huyo aliporudi tena siku mbili baadae, wahudumu wa afya walichunguza koo yake na mfumo wa kutoa sauti- na ni hapo walipogungua kuna kitu chenye muundo wa duara nusu ambacho kimeziba sehemu ya koo lake.

Baadae aliwaambia amepoteza meno yake bandia – meno matatu na sehemu ya juu ya ndani ya mdomo – wakati alipokuwa amelazwa hospitali hapo kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Baada ya upasuaji mwingine wa kuondoa meno hayo bandia aliruhusiwa kwenda nyumbani alkini alirudi tena mara nne hospitali akiwa na tatizo la kutokwa na damu.

Wakati wataalamu walipogundua damu hiyo inatoka kuuni mwake alikuwa amepoteza damu nyingi kiasa cha kuhitaji kuongezewa damu.

Mtayarishi wa ripoti hiyo amesema visa vingine kama hivyo vimewahi kushuhudiwa ambapo watu wamewahi kumeza meno bandia baada ya kudungwa sindano ya kufisha ganzi.

Kawaida mgonjwa huulizwa kama ana kiungo chochote bandia kama meno mwilini mwake na meno hayo hutolewa kabla ya mgonjwa kufanyiwa upasuaji, waliongeza.

Mkurugunzi wa Hazel Stuart, katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget, amesema hatua hiyo ilikuwa imefanywa.

“Kutokana na kisa hiki, mchakato huo umechunguzwa upya, na kufanyiwa marekebisho, na wafanyikazi kuhusishwa vilivyo katika utaratibu huo,” alisema.

-BBC

Pombe inawapotezea muda na pesa zenu; Frasha awambia walevi

Kiongozi wa chama cha Maendeleo Chap Chap, Frasha amesema kuwa ameachana na pombe kabisa na sasa anataka vijana waachane na ulevi kabisa kama yeye.

Frasha ambaye hivi karibuni amekuwa akiwarai vijana waache pombe hivi karibuni amekuwa mlevi kwa zaidi ya miaka kumi na mitano sasa.

download (3)

“Nilijipa changamoto ya kususia pombe kwa siku 40 sasa kila mwaka na sasa nimegundua umuhimu wa kuachana na ulevi,” Frasha alieleza Word Is siku ya Jumanne. Frasha anasema kuwa upo wakati alitumia hela zaidi ya elfu mia tano chini ya mwezi mmoja.

“Jinsi mtu anavyozidi kukua ndivyo ajuavyo kuwa vitu vingine havina umuhimu wowote maishani mwako kwani vinaharibu wakati wako, pesa yako pamoja na kukupotea fahamu bure.”

Vanessa Mdee afichua kwamba anamatatizo ya macho

Frasha alisema kuwa anajutia kuhusu pesa alizotumia kwenye ununuzi wa pombe,” Hakuna jambo nzuri kuhusiana na pombe. Kazi kubwa ni kukuharibia wakati, inakuumiza mwili wako bure pamoja na kukupotezea mambo ya maana.”

Frasha amewapa changamoto kwa kuwaambia wafikirie mahali watakuwa miaka miwili ijayo na wajue mahali watataka kua miaka miwili ijayo kuanzia sasa,”Nimegundua kuwa pombe ipo kila siku na itaishi kuwako licha ya jambo lipi liyokee.Mke wangu haniamini na hivyo ameniambia nimpe mude kwai bado anafikiria mimi ni mlevi.”

Frasha kwa sasa anaendelesha chama chake cha Frasha HIV Foundation ambacho kinawasaidia na kuwashauria watu wanaougua ugonjwa wa ukimwi.

SOMA MENGI HAPA

Nina uhakika Ozil na Kolasinac wako tayari kucheza – Unai Emery

Kocha wa Arsenal Unai Emery ana uhakika asilimia mia moja kuwa wachezaji wake Mesut Ozil na Sead Kolasinac wako tayari kurejea katika kikosi chake, baada ya kuwachwa nje ya mechi ya kwanza ya ligi ya EPL dhidi ya Newcastle kutokana na usalama wao.

Wawili hao walikua wamehusika na jaribio la kuibiwa na watu wawili ambao walitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka. Emery pia anadai wawili hao wako katika hali nzuri ya kimawazo na watafanya vyema.

Wanafunzi waliopatikana na dawa za kulevya waachiliwa kwa dhamana

Mtandao wa kijamii wa Twitter umekubali kujadili ubaguzi wa rangi na kundi moja linalopambana na ubaguzi huo katika soka Kick It Out kwa mara ya kwanza.

Haya yanajiri wakati mshambulizi wa Chelsea Tammy Abraham alipolengwa mitandaoni kwa kukosa mkwaju wa penalty wakati walipopoteza 5-4 kwa Liverpool katika fainali ya Super Cup jumatano usiku. Kick It Out imekuwa ikishinikiza jukwaa za mitandaoni kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi huo.

Hayo yakijiri, kocha wa mchezo wa table tennis wa timu ya taifa Fahd Daim anasema kuwa ana imani kikosi chake kitafika katika awamu ya medali katika michuano ya All African games nchini Morocco.

Fahd amekua akifanya mazoezi na timu yake katika ukumbi wa  Kasarani kwa mwezi mmoja kabla ya kuondoka jana kabla ya kuelekea Rabat, Morocco.

Baba amuumiza mwanawe kwa kuchimba na kupika viazi

Kikosi hicho chenye wachezaji 10 kitaongozwa na Josiah Wandera, Brian Mutua, na  Ken Kojal upande wa wanaume huku Doreen Juma, Nelly Mutuma, na Pamela Glory wakiongoza kikosi cha kinadada.

Timu ya soka ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 15 itaanza kampeni yake katika mchuano wa CECAFA dhidi ya Somalia kesho mjini Asmara, Eritrea. Kenya ambao wako katika kundi A pamoja na wenyeji Eritrea, Sudan na  Burundi watakuwa wanawania ushindi ili kuimarisha nafasi zao za kufuzu kwa awamu ya robo fainali. Kocha msaidizi Elvis Nandwa anadai wako katika hali nzuri na watakua wanatafuta ushindi.

Mabingwa wa zamani wa KPL AFC Leopards waliwalaza Polisi wa utawala mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jana katika uwanja wa KTTC. Ingwe ilipata mabao yake kupitia Austin Ochieng na Hansel Ochieng, huku wakiziba ngome lao na kuhakikisha wapinzani hawakufunga goli lolote.  Ingwe walimaliza katika nafasi ya 11 na watakua wanawania kushinda ligi msimu huu baada ya zaidi ya miaka 20.

 

PATANISHO: Nilimtusi mke wangu kuwa tunda lake sio tamu

Joshua kutoka maeneo ya Kilifi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bibi yake bi Anette akiomba ndoa yake iokolewe kwani yazama.

“Mimi na yeye tumeoana kwa miaka mitatu na alipofika nyumbani sijui ni kama hakupendelea maeneo yale kwani kitambo tulikuwa twaishi Malindi.

Tuliporudi Kilifi ni kama hakufurahia na tulichokosana zaidi ni kuwa alikuwa anateteshana na mamangu na mimi kidogo nikaegemea upande wa mama.” Alieleza Joshua.

Tazama mitaa Sonko wa Redio Jambo atafungia zoezi la kugawa hela nchini

Licha ya yale yote mkewe bado yuko lakini anasema kuna wakati alimtusi na kumwambia tunda lake la ndoa sio tamu. Hata baada ya kuzungumza bado anahisi mkewe hayuko sawa.

“Halafu unajua amepata kazi maeneo ya Tana River na nahofia nitawachwa, huo ndio wasiwasi wangu hata nakonda.” Aliongeza.

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Isitoshe Joshua alisema kuwa mkewe itabidi adjust time table ya Mombasa raha kwani hatosheki lakini mkewe anasema hana shida na tendo la ndoa.

Unachotakiwa kufanya ili ushinde elfu 5 na elfu 1 kutoka Redio Jambo

Tazama mitaa Sonko wa Redio Jambo atafungia zoezi la kugawa hela nchini

Zoezi la kuwatunuku hela mashabiki wa kituo hiki linatazamiwa kufika tamati Agosti 30 msimu huu. Ikumbukwe kuwa mchakato huu wa kuwapa zawadi mashabiki zawadi hufanyika kila mwaka. Sonko wa Redio hii atakuwa anafunga ziara za kuzunguka miji mbalimbali baada ya kuzuru viunga vya jiji la Nairobi wiki ijayo.

Pata uhondo:

Unachotakiwa kufanya ili ushinde elfu 5 na elfu 1 kutoka Redio Jambo

Kituo hiki kinatazamiwa kuwatembelea mashabiki katikati mwa jiji la Nairobi jumatatu wiki ijayo. Sonko atafagia kabisa University Way, Odeon, Ambassador, Railways, Ngong, Kiserian na baadaye Rongai.

Siku ya pili sonko atavamia Industrial Area, South B na South C. Siku ya tatu sonko atachana kabisa mitaa ya Thika, Juja, Githurai, Kasarani, Mwiki, Babadogo na baadaye Dandora.

Sonko atapumzika baada ya kutinga ziara za mwezi mzima Embakasi, Syokimau,Mlolongo , Kitengela na Kajiado.

Sonko wa Redio Jambo azuru miji ya Kibwezi,Voi na Taveta

Maswali atakayokwenda kuuliza mashabiki sonko huyu ni rahisi sana. Sonko anahitaji kujua iwapo wasikilizaji wanaelewa kabisa maneno machache yanayolipa pesa “The Phrase That Pays”. Iwapo shabiki ataweza kung’amua Redio Jambo Ongea Usikike, sonko huwatuza shilingi 1,000. Aidha, mashabiki wanaozidisha ubunifu na kuyaandika maneno hayo katika bango hutunukiwa shilingi 5,000 pesa taslimu.

Unachotakiwa kufanya ili ushinde elfu 5 na elfu 1 kutoka Redio Jambo

Kituo chako mahabubu cha Jambo kwa mwezi mzima sasa kimejikita katika mchakato wa kuwatunuku wasikilizaji na hela lukuki. Zoezi hii ilianza tarehe 15 Julai na linatarajiwa kufungwa tarehe 30 Agosti mwaka huu.

Soma hapa:

Sonko wa Redio Jambo azuru miji ya Kibwezi,Voi na Taveta

Cha msingi sonko huyu anahitaji kujua ni iwapo wasikilizaji wanaelewa kabisa maneno machache yanayolipa pesa “The Phrase That Pays”. Iwapo shabiki ataweza kung’amua Redio Jambo Ongea Usikike, sonko huwatuza shilingi 1,000. Aidha, mashabiki wanaozidisha ubunifu na kuyaandika maneno hayo katika bango hutunukiwa shilingi 5,000 pesa taslimu.

Juma lijalo sonko huyu atazamia mji mkuu wa Nairobi kuwazawadi mashabiki. Sonko wa masonko atatembea viunga vya Nairobi kwa mara nyingine kwa udi na uvumba kumsaka atakayeng’amua The Phrase that Pays ambayo ni Redio Jambo Ongea Usikike.

Soma hapa:

Redio Jambo yatua miji ya Nyeri na Mwea kuzawadi mashabiki

Mapokezi makubwa hii leo yameshuhudiwa Voi, Taveta na Kibwezi huku wasikilizaji wakipata zawadi kemkem kutoka kituo hiki.

 

Sonko wa Redio Jambo azuru miji ya Kibwezi,Voi na Taveta

Sonko wa kituo cha Jambo hii leo amezuru miji iliyopo katika barabara kuu ya Nairobi kwenda Mombasa na kuwatuza mashabiki na hela kibao. Sonko huyu alianza ziara mjini Kibwezi na baadaye kuzamia Voi na kufunga ziara nzima mjini Taveta

Kituo cha Jambo kwa sasa kimemaliza mwezi mmoja katika mitaa kote nchini kikihusika katika zoezi la kuwatunuku wasikilizaji kwa ushabiki mkubwa. Kituo hiki kinawatuza mashabiki sugu wanaofahamu The Phrase That Pays Redio Jambo Ongea Usikike. Sonko wa kituo hiki alianzia juhudi hizi za mchwa viungani mwa jiji la Nairobi na baadaye akatoka jiji kuu na kuzamia miji midogo nchini.

Soma hapa:

Patanisho: Alitoka na ugali nilipoenda kumtembelea

Juma lijalo sonko huyu atazamia mji mkuu Nairobi kuwazawadi mashabiki. Sonko wa masonko atatembea viunga vya Nairobi kwa mara nyingine kwa udi na uvumba kumsaka atakayeng’amua The Phrase that Pays ambayo ni Redio Jambo Ongea Usikike.

Pata uhondo hapa:

Otile hakuninunulia gari! Jovial amwambia Massawe Jappani