Diamond Platinumz ataja siku ya harusi

Diamond platinumz amefichua siku anayo pania kumuoa mpenziiwe Tanasha.

Akizungumza na waandishi wa habari wa lebo yake ya Wasafi, katika wasafi festivals kule mjini Dar – es- salaam jana, Diamond alisema huenda siku ya harusi yake na Tanasha ni tarehe 7 Julai mwaka huu.

Diamond alitoa habari hio akijibu swali la mwanahabari mmoja aliyemuliza siku anayaopanga kumvisha pingu za maisha binti huyu wa kikenya.

Majibu yake yalikuwa ya kupendeza sana kwani alitaja kuwa atatoza watu fedha za kuingia kwenye harusi yake.

“Itakuwa sherehe ya kufana sana kwani kutakuwa na meza kumi huku 5 za kwanza zikilipiwa 200,000 ilihali zilizobaki zikilipwa shillingi 80,000 kila moja. Nathani mnafaa kuhifadhi hizo meza zote kwani kila mmoja atakumbuka tarehe 7 mwezi julai mwaka huu.”

Diamond Platnumz with Tanasha

Staa huyu wa kibao cha kanyanga na African Beauty, alisema kuwa sababu ya kupeleka harusi yake mbele kutoka tarehe 14 mwezi Februali mwaka huu ni kuwa hawakuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya hafla hio ya kiheshima ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa wengi wa nguvu ulimwenguni.

 

Diamond Platnumz holding Tanasha
Diamond Platnumz holding Tanasha
Hata hivyo, Diamond ameamua kuwa na meza 10 pekee. Je, hilo litawezekana aje? Na Je, huenda sababu ya ndoa hii ni uja uzito wake Tanasha? sote natungoje tumwone Diamond atakalo fanya.

 

PATANISHO: Alinichapa na kuniumiza mbavu na kichwa

Paul mwenye miaka 32 aliomba kupatanishwa na Martha mwenye miaka 28. Wawili hawa wamekua kwenye ndoa kwa miaka tisa lakini Paul akamchapa na kumuumiza Martha, ambaye aliondoka.

PAul alieleza kwamba;

“Mke wangu alienda, nilikua nimemfungulia kazi ya kuuza viazi. Nilikua nimetoka mazishi nikapata amekasirika akidhani nimetoka kwa wanawake, akaenda sokoni akaniachia mtoto, nikachukua mtoto nikapelekea mwanamke mwingine ambaye ni Cousin yangu.

Nikiwa nakunywa pombe, bibi akaniambia mtoto hajakula. Nikiongea na mwanamme mwingine, akadhani nilikua namuongelea, akanitusi, nikamtandika makofi. Nilikua nimekasirika na kulewa. Mimi ndio nilikua na makosa.Martha naomba unisamehe.”

PATANISHO: Nime move on na maisha na haturudiani!

Martha alimjibu Paul;

“Alinipiga na kunifanya madharao, akanikanyaga, mbavu na kichwa akaniumiza kabisa hata sasa hivi sijapona.Pole yako mimi sitaki ulinishapa na haukuwahinisaidia hata hospitali. Sitaki nimekataa. Nitakupatia miaka tano ujirekebishe.Nimechoka na kulia na kuchapwa kila siku.Mimi nishatosheka kuolewa”

Sikiza mawasiliano yote kati ya Paul na Martha kwenye link ifuatayo;

‘Vijana chipukizi wanaopendana,’ Mama Diamond asifia Tanasha

Mama ya Mwanamziki Diamond Platnumz amemsifia Tanasha Donna ambaye ni mpenzi wa mtoto wake. Mama Diamond ambaye anajulikana kwenye mitandao ya kijamii kama Mama Dangote alitoa sifa hizo kwenye Instagram na kuandika kwamba;

“Vijana Chipukizi, wanaopendana, wanyenyekevu tena wanaopendeza ❤❤❤”

tanasha.donna.diamond

Diamond alitangaza kwamba atafunga ndoa mwisho wa mwaka huu na mwanamitindo huyo wa Kenya huku akiisihi serikali ifanye siku hiyo sikukuu ya kitaifa.

Tanasha anadaiwa kuwa na mimba ya Diamond ila wawili hao hawajaweka wazi fununu hizo, lakini iwapo Tanasha ana Mimba, huyo atakua mtoto wa nne wa Diamond.

Diamond ana watoto wawili na aliyekua mpenzi wake Zari Hassan. Pia ana mtoto mmoja na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Diamond alipokua kwenye mahusiano na Zari, mamake alimsifia sana lakini sasa hivi, inaonekana kwamba Tanasha ndiye kipenzi cha mama mkwe.

Diamond akiri kumfuatilia Zari na mpenziwe katika mitandao ya kijamii

‘Sidaiwi kodi,’ Hamisa Mobetto akanusha fununu

Hamisa Mobetto ambaye ni mwanamitindo kutoka Tanzania amekanusha madai kwamba anadaiwa kodi. Akiongea na SnS, Mobetto, ambaye pia ni mwanamziki amesema kwamba hajawahifeli kulipa kodi ya nyumba.

“Mimi sidaiwi kodi na sijawahi kudaiwa kodi. Kila baada  ya miezi miwili huwaga wanaziongelea, kila siku nikiamka kuna habari mpya kunihusu. Mimi niko palepale na ikitokea siku ambayo nataka kuhamia sehemu nyingine, nitahama.”

hamisa.mobetto.1

Mobetto ni mama wa watoto wawili. Alitamba mitandaoni alipokua kwenye uhusiano na Diamond Platnumz ambaye ni mzazi mwenza.

Hivi sasa, Mobetto anasema kwamba hayuko kwenye uhusiano wowote kwa kuwa anajishughulisha na muziki na bisahara yake ya nguo.

hamisa mobetto

Sina mimba ya Diamond, nikomeni! Hamisa shuts down rumours

Willy Paul anataka mwanamke, sio mke

Willy Paul ameweka wazi kwamba anataka mwanamke ambaye atakuwa mwandani wake ila hatamuoa. Amesema anawezakuwa katika mahusiano zaidi ya miaka thelathini bila kuoa.

“Kwanini nioe? Nataka mwanamke lakini sio mke” Mwanamziki huyo aliongea katika njia ya simu na ripota wetu.

Aliendelea kusema kwamba yeye hayuko katika Uhusiano ijapokua anaimba nyimbo ambazo ni za mapenzi.

“Siko kwenye uhusiano wowote, wanawake ni watu wagumu sana. Nimejifunza kwa maisha na siyaamini mapenzi”

Willy Paul
Willy Paul

Hata hivyo, Mali Queen, ambaye ni mzazi mwenza wa Willy Paul,aliambia wasichana wakae mbali na mumewe.

“Wasichana, Willy Paul amechukuliwa na hivi karibuni tutafunga ndoa. Mimi ni mama wa mtoto wake #KingDamian..Wasichana kaeni mbali, msimletee majaribu.”

Lakini je! Willy Paul na Mali Queen wako katika mahusiano?

willypaulnewlook

Willy Paul amtafutia kazi Mcee mkubwa nchini

 

Vanessa Mdee aachana na mpenzi wake Juma Jux

Mwanamziki Vanessa Mdee ametangaza rasmi kwamba ameachana na aliyekua mpenzi wake Juma Jux. Wawili hao kutokea nchi jirani ya Tanzania wamekua kwenye mahusiano kwa mda mrefu.

Kwenye mtandao wake wa Instagram, Vanessa Mdee aliulizwa na shabiki mmoja kama ameachana na Juma.

Mdee alijibu “Ndio, lakini sisi ni marafiki wazuri na daima, tutakua familia”

Vanessa Mdee

Siku kadhaa zilizopita, dada ya Vanessa kwa jina Mimi Mars aliweka wazi kwamba wawili hao walikua wameachana, japokua Vanessa na Juma walikua wamekataa kuongea kuhusu jambo hilo.

“In Tanzania, to enter a corporate building your skirt must pass your knees,” – Vanessa Mdee

Sasa ni wazi kwamba Vanessa hayupo katika mahusiano.

Vanessa Mdee na JUma Jux

Mpenzi Wa DK Kwenye Beat amuenzi siku yake ya kuzaliwa

Mwanamziki wa nyimbo za injili DK Kwenye beat anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Mchumba wake Shanice Wangeci amemuenzi kwenye mtandao wa Instagram akimshukuru kwa kuwa mtu ambaye anamsikiliza wakati wote.

“Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu. Asante sana kwa kuwa rafiki yangu, mwendani wangu na kunisikiliza ninapotaka mtu wa kunisikiliza. Asante kwa kunipa sababu za kuangaza. Wewe ni kila kitu na ninatumai siku hii ni mojawapo wa siku nzuri maishani mwako.”

DK Kwenye Beat

DK atamba mitandaoni miezi kadhaa iliyoisha baada ya kuhusika kwenye mahusiano ya ngono na mwanafunzi wa chuo kikuu.

HopeKid : Nilifukuzwa kanisani kisa skendo yangu na DK kwenye Beat

Baadaye mpenzi wake, Shanice, alifuta picha zote katika mtandao wake wa Intagram lakini kwa sasa hivi amerudi na inaonekana kwamba mapenzi ya wawili hawa yanazidi kutamba.

Wanaume msilale na chupi! Pia badilisheni na sio kuvalia moja kila siku

Wanaume wameshauriwa kulala bila chupi au kuvalia zinazolegea.

Mwanajinakolojia Allan Ikol anasema kuvalia chupi za kubana ni jambo linaloathiri kiwango cha mbegu zako za kiume na hata ubora wake.

Je,ni kipi kinafaa kutolewa bure? Kondomu au kisodo?

Ikol anasema uzalishaji wa mbegu huregemea kiwango fulani cha joto na sehemu iliyojibana huwa na joto jingi. Joto hilo ndilo linaloathiri uzalishaji wa mbegu za kiume. Anaongeza kwamba wengi hufanya kosa la kulala usiku wakiwa na nguo za ndani zinazowabana sana bila kufahamu madhara yake.

 

Pia kuna   hili tatizo la wanaume kuwa na tabia ya kuvalia chupi moja zaidi ya mara moja .  wengi hufikiri hatua hiyo haina madhara lakini    Dkt .Ikol anasema ,unajitia katika hatari ya kupata maambukizi  katika sehemu zako za  uume endapo utarejelea  chupi yako kila mara .Anasema  harufu  ,msuguo wa ngozi na jasho   ni mchanganyiko  unaoweza kusababisha ukuaji  bakteria hatari  inayoweza kukudhuru .

Ikol anasema sio ajabu kumwona mwanamme aliyejikwatua kwa suti nadhifu sana lakini  ndani ,Chupi ina matundu kama kichungi !

Je, ni kweli kwamba  wanaume  hawatalii maanani usafi wa chupi zao?

Kauli ya Siku Ijumaa 31 Mei 2019

Mume wa Janet Mbugua aziweka wazi picha za mtoto wao wa pili

Mtangazaji maarufu Janet Mbugua alijifungua mtoto wa kiume, Mali, mwezi wa September na hatujapata fursa ya kuona uso wake tangu kuzaliwa.

Eddie Ndichu mumewe Janet, alipiga picha na wanao wawili wa kiume wakiwa katika hafla ya familia na kuziweka kwenye mitandao za kijamii.

Ni hakika Mali anafanana na mama yake kama shilingi kwa ya pili lakini kwa hakika macho ni ya baba yake.

Nominated Senator Millicent Omanga shows off lavish mansion – photos

janet mbugua (1)

Janet amekua akiwaweka wana wao mbali na mitandao za kijamii kama wanavyo fanya kina mama wengi ambao ni mastar hapa Kenya.

Mwaka uliopita, Sharon Mundia alikuwa amemueka mtoto wake mbali na mitandao ya kijamii kama tu vile Janet ila bwana yake akiziweka picha hizo wazi kwa umati.

Mtazame mtoto Mali:

Natural ways to keep your body warm during this cold weather

 

Read more

‘Kifo cha babangu kiliniuma sana’ Msanii Wyre afunguka

Msanii mashuhuri Wyre amesema kwamba kifo cha babake mzazi ndicho kitu kilicho muuma sana maishani kwani alikua mwandani wake.

Akiongea kwenye mahojiano na radio jambo Wyre alisema

wakati wa mwisho mimi kulia ni baada ya kumpoteza babangu.

WYRE
wyre

Couple goals! A list of the Best dressed celebrity couples

Babake Wyre aliaga dunia mwaka wa elfu mbili kumi na tano (2015) kabla Wyre atoe album yake ya ‘Wanilinda’.

Wyre aliweza kusema kwamba hakuweza kuupigia debe wimbo wake ilivyostahili kwani alikua bado anaomboleza.

Aliongeza kwamba kitu atakachomkumbuka babake nacho ni kwamba alikuwa anampa motisha wa kuendelea na muziki.

Wakati nilipojiingiza kwenye muziki, babangu aliniunga mkono na alifanya kila juhudi kuwa mwelekezi wangu.

Alitupa moyo kwa kutuhimiza tumwimbie tulipokuwa nyumbani.

Ngoma festival

Memes of that photo of President Uhuru showing off his photography skills

Hivi majuzi Wyre alisema kwamba kuoa mke wake wa miaka kumi mara ya pili ni kwa sababu ndoa ni kitu anachokidhamini kwa dhati.

Nashukuru mungu sana ya kwamba nina ndoa imara.

Kitu ambacho kimefanya ndoa yangu isimame kwa miaka kumi ni kwamba mimi na mke wangu tuna ongelelea maswala kwenye ndoa muda tu yanapojitokeza.

Wyre ambaye ni baba wa mtoto mmoja alisema sababu kuu ya kuweka familia yake mbali na mitandao ya kijamii ni kwa sababu hataki wadhulumiwe kwa hali yoyote ile.

Read more