Mwanamme mmoja apatikana ameaga kwenye kambi la polisi huko Busia

Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 20 amepatikana ameaga dunia kwenye chumba kimoja katika kambi la polisi wa utawala ya Malambisia eneo bunge la Butula kaunti ya Busia kwa njia ya kutatanisha.

Inadaiwa mwanaume huyo alikamatwa na maafisa wa polisi wakati wa usiku kwa tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja katika eneo hilo, na wananchi wanadai alipigwa na maafisa hao kabla ya kufunga nguo shingoni na kudai kuwa alijitia kitanzi.

Kwingineko

Kinara wa ANC musalia Mudavadi amewataka wakenya kuunga mkono usajili wa huduma namba akisema hatua ya viongozi wa upinzani kuunga mkono zoezi hili ina maana kuwa sio swala la serikali bali ni la manufaa kwa wakenya

Akiongea mjini Kakamega, Mudavadi amesema usajili wa huduma namba utahakikisha kila eneo linapata mgao sawa kulingana na idadi.

Kwingineko

Washika dau katika sekta ya mazingira wameelezea wasi wasi wa kaunti ya Taita Taveta kuendela kukabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya anga kufuatia hatua ya kuendelea kuchomwa kwa misitu mikuu eneo hilo, kukatwa miti kiholela na uharibifu wa chemchemi za maji.

Mwanamazingira Esther Mwanyumba anasema kwa mda wa juma moja sasa misitu kadha imechomwa, hali ambayo anasema iwapo haitathibitiw, huenda eneo hilo likakuwa jangwa hivi karibuni.

Ameitaka jamii ya Taita Taveta kutupilia mbali dhana potofu kuwa uchomaji misitu kunavutia Mvua.

Click here for more

Serikali yatenga shilingi millioni 650 kukabili changamoto ya maji katika kaunti 23

Serikali imetenga shilingi milioni mia sita hamsini kukabili changamoto ya maji katika kaunti ishirini na tatu ambazo zimeathirika pakubwa

Waziri wa maji, Simon Chelugui amesema fedha hizo zinatumika kuhakikisha maji yanafikia mashinani kwenye kaunti zilizoathirika

Waziri huyo alitaka baraza la magavana kuona kwamba magavana wanakomesha uhasama wa umiliki wa vyanzo vya maji akisema ni raslimali ambayo haina mipaka

Chelgui amesema uwepo wa raslimali ya maji hauzingatii mipaka ya ki maeneo

Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya ametaja uwepo wa idara nyingi zinazohusika na usimamizi wa maji kuwa sababu ya gharama ghali ya maji.

Oparanya anaitaka serikali ya kitaifa kuona kwamba inaondoa mzigo kwa mwananchi aweze kupata maji kwa bei nafuu.

Kwingineko

Imebainika kuwa idadi ya vijana wanaochukua mikopo kutoka kwa hazina ya vijana nchini ni ya chini mno ikilinganishwa na kaunti zingine.

Afisa mkuu mtendaji wa hazina hiyo Josiah Moriasi anasema vijana pia hukuosa kulipa mikopo yao huku akisisitiza haja ya serikali za kaunti kuwapa zabuni makundi ya vijana ili kujiendeleza.
Hazina hiyo imetoa takribani milioni 35 pekee za mkopo kwa vijana kaunti hiyo kwa kipindi Cha miaka 12.

Read here for more

Mwanamume mmoja aua mkewe katika kijiji cha mahiakalo, Kakamega

Mwanamume mmoja amemuua mkewe katika kijiji cha mahiakalo kaunti ya kakamega na kisha kutorokea katika msitu wa Kakamega akitishia kijutia kitanzi

Juhudi za jamaa yake kumpata hazijafua dafu.

Kwingineko

Serikali imewatahadharisha wananchi dhidi ya kupotoshwa kuhusu mpangilio wa serikali wa kuwasajili wakenya kwa nambari maalum

Justus Mukoshi kutoka idara ya utawala kaunti ya kakamega amewasuta baadhi ya watu wanaowapotosha wananchi kuwa serikali ina nia tofauti ya kuwasajili katika nambari hiyo yakiwemo mambo ya kura ya maoni

Kwingineko

Makundi ya kijamii na idara za elimu na mahakama katika kaunti ya Taita Taveta zimetakiwa kushirikiana ili kukomesha ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia dhidi ya watoto katika eneo hilo.

Macrina Mwamburi kutoka sauti ya wanawake anasema visa hivyo bado vinaendelea kuripotiwa kwa wingi hususan maeneo ya mashinani huku washukiwa wakikosa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Anasema kuna haja ya jamii kupewa hamasa kuhusu athari za uovu huo.

Click here for more stories

Wakulima kutoka Taita Taveta wazusha kuhusu uvamizi wa ndovu mashambani yao

Mamia ya wakulima kutoka Sagala kaunti ya Taita Taveta hatimaye wameandikisha taarifa katika kituo Cha polisi Cha Voi kuhusu hasara wanayopata kufuatia uvamizi wa ndovu.

Wakulima hao ambao wanakadiria hasara kubwa sasa wanaitaka serikali kuwafidia mimea na mali yao iliyoharibiwa na ndovu ambao wamevamia maeneo ya Sagalla, Kirumbi na Kasighau tangu mwezi jana.

Kwingineko, vijana katika kaunti ya Taita Taveta watanufaika na masomo ya kibiashara pamoja na ufadhili wa kifedha kutoka kwa hazina ya maendeleo kwa vijana.(Youth Enterprise Development Fund) kupitia kwa mpango wa Youth Plus Mashinani.

Moris Murimi kutoka hazina hiyo anasema mpango huo utakaofanyiwa majaribio katika kaunti tatu unalenga kuwawezesha vijana kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu ubunifu wa biashara kupitia kwa kozi fupi za miezi sita.
Kwingineko, familia moja kutoka mjini Nambale kaunti ya Busia inaishi kwa hofu baada ya jamaa wao kutoweka nyumbani kwa njia isioeleweka.

Ziporah Wafula anasema mwanawe Daniel Abakar mwenye umri wa miaka 24 alitoka nyumbani tarehe 26/12/2018 na hadi leo hajawahi kuonekana huku juhudi zao za kumtafuta katika vituo vya polisi, hospitalini na hata kwenye vyumba vya wafu zikikosa kuzaa matunda.

Magavana wa Kaunti za Ukanda wa magharibi wakubaliana ishu ya ushuru

Magavana watano kutoka kaunti za ukanda wa magharibi kwa kauli moja wamekubaliana kuwa na (a common inter counties taxation) kwa minajili ya kushirikiana na kuruhusu wenyeji maeneo hayo kufanya biashara kwa uhuru.

Wakizungumza katika kaunti ya Bungoma baada ya kuwa na mkutano pamoja Magavana hao ambao ni Wycliffe Oparanya wa kaunti ya kakamega, Wilber Otichilo wa Vihiga , Sospeter Ojamong wa Busia , Khaemba Patrick wa Transnzoia naye Wickliff Wangamati wa Kaunti ya Bungoma wameelezea kuwa wana imani hatua hiyo ni mwanzo wa kuleta maendeleo katika maeneo hayo na nchi kwa ujumla.

Brian O. Ojama

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 46 auwawa Kaunti ya Bungoma

Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Makutano Eneo bunge la Kanduyi Kaunti ya Bungoma baada ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 46 kuuwawa na watu wasiojulikana kwa kudaiwa kudungwa dungwa mara kadhaa kwa kisu.

Tom Sifuna Mumewe marehemu anaarifu kuwa alipata habari kuwa wanawe walifika nyumbani kutoka shuleni majira ya jioni na kumpata mama yao kwa jina Irene Sifuna ameuwawa na alipofika nyumbani alimpata mkewe akiwa amelazwa kitandani akiwa uchi na majeraha ya kisu mgongoni huku kisu kilichokuwa na damu pamoja na kamba vikipatikana kando yake.

Hata hivyo maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho huku wakimsaka mfanyakazi wa boma hilo ambaye anadaiwa kutoweka na kwenda mafichoni baada ya kisa hicho cha kutamausha.

Matumaini ya familia moja kumpata mwanao yameambulia patupu

Matumaini ya familia moja kumpata mwanao akiwa miongoni mwa manusura wa ajali iliyotokea hivi majuzi huko Kericho imeambulia patupu.
Familia hiyo iliyoko kijijini Gidimo katika kata ndogo ya Galona,Gisambai katika kaunti ndogo ya Hamisi imegubikwa na biwi la simanzi baada ya juhudi zao za kumsaka mwanao kwa siku tatu kugonga mwamba huku mwili wake ukigunduliwa leo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Russia mjini Kisumu.
Abrahm Madete na Nancy Minayo ni babu na shangaziye kijana huyo na wamekielezea kituo hiki kwamba mwanao alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Chuka na alikuwa akirejea nyumbani kuchukua bidhaa fulani za shughuli za masomo ndipo akapatana na mauti.
Insert-shangazi na babu
Hata hivyo familia hiyo inaomba msaada kutoka kwa serikali na wasamaria wema kuingilia kati na kuwanusuru katika hali hiyo ngumu ikizingatiwa kuwa aila hiyo ni ya pato la chini mno.

Collins Mmbulika

Wahadhiri 85 katika chuo cha teknologia cha Pwani wapinga vikali za serikali

Zaidi ya wahadhiri 85 katika chuo cha teknologia cha Pwani mjini Voi wamepinga vikali hatua ya serikali  ya kupunguza mishahara yao bila kutoa notisi.
 
Akizungumza chuoni humo mapema hii leo,katibu mkuu wa muungano wa KUPPET tawi la Taita Taveta Shedrack Mutungi amesema huendi jambo hilo limetokana na hatua ya serikali ya kuhamisha walimu hao kutoka kwa tume ya TSC hadi tume ya wafanyikazi wa umma(PSC).
 
Anasema hatua hiyo inakiuka agizo la mahakama linalozuia uhamisho wa walimu wa vyuo vya kadri (TVET) kote nchini hadi PSC na kuitaka serikali kuwalipa mishahara yao kikamilifu la sivyo wawasilishe kesi mahakamani.
 
Uhamisho huo umeathiri kiwango cha marupurupu yanayotolewa kwa walimu huku wengine wakikatwa kati ya shilingi elfu 12 na elfu 40.

Mwendeshaji wa pikipiki alikufa baada ya ajali na trella huko Mwatate

Mwendeshaji mmoja wa pikipiki mwenye umri wa makamo huko Mwatate kaunti ya Taita Taveta ameaga dunia papo hapo usiku wa kuamkia leo baaada ya kugonga trella kwa nyuma katika barabara ya Mwatate/Taveta.

Walioshuhudia wanasema mwendazake alikuwa anajaribu kuipita trella hiyo kabla ya kupunguza mwendo ili kukwepa kugongana ana kwa ana na gari jingine.

Mwili wake umepelekwa kuhifadhiwa katika hifadhi ya Moi mjini Voi.

Solomon Muingi Junior

Mbunge wa Matayos atishia kuishtaki serikali na inspecta mkuu wa polisi

Mbunge wa Matayos Kaunti ya Busia Geoffrey Odanga ametishia kuishtaki serikali na inspector mkuu wa polisi Joseph Boinet kutokana na visa vya maafisa wa polisi wa kituo cha kampuni ya miwa ya Busibwabu ya kuwavamia na kuwaumiza wananchi wasio kuwa na hatia kwa kizingizio cha kupiga vita pombe haramu.

Odanga amewataka maafisa hao kubadili tabia yao au waondolewe eneo hilo.