EACC yamchunguza Oparanya

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi inamchunguza gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuhusiana na madai ya kununua hoteli moja mjini Kisumu kwa kima cha shilingi milioni 250.

Oparanya
Oparanya

Ripoti ya EACC iliofikia the Star inaonyesha kwamba EACC inachunguza madai kuwa Oparanya alinunua St John Manor Hotel akitumia pesa za umma zinazoaminika kufujwa kutoka hazina ya kaunti ya Kakamega.
Hoteli ya St John’s Manor ni ya kiwango cha three-star katika barabara ya Nerhu mjini Kisumu.

 
Inapakana na hifadhi ya wanyama ya Impala na Kisumu Yatch Club.
Hoteli hiyo hutumika sana kwa mikutano ya magavana kutoka eneo la Magharibi kila wanapokuwa na mikutano mjini Kisumu na hugharimu kati ya shilingi 6000 – 9000 kwa usiku mmoja.

Wycliffe Oparanya
Wycliffe Oparanya

Hata hivyo Oparanya ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la Magavana, siku ya Jumapili alitaja uchunguzi huo kama kupoteza muda na kushikilia kwamba hamiliki hoteli hiyo na kwamba hana hata nia ya kuinunua.

 
“Si miliki hoteli hiyo na sijawahi kuimiliki. Wakitaka kuchunguza,wacha wafanye hivyo,” Oparanya aliambia The Star kwa simu.

 
Aliendelea kusema: “Hakuna kosa mimi kumiliki hoteli. Hata kama ningemiliki, ningefurahia kusema. Nini mbaya na kumiliki hoteli?”

 
Oparanya amepongezwa sana kwa kuimarisha maendeleo katika kaunti ya Kakamega na huenda uchunguzi wa EACC rekodi yake nzuri.

Ruto akutana na rafikiye baada ya miaka 35!

Naibu rais William Ruto hangeficvha furaha yake baada ya kukutana na jamaa waliokuwa wakisoma naye, Sospeter Ojwang.

 

Maraifiki hao wawili, walikutaona tena katika eneo la Lwanda siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza tangu walipofanya mtihani wa kidato cha nne katika shule ya Wareng.

 

Delighted to meet and reunite with Sospeter Ojuwang, a former schoolmate at Wareng High School, Eldoret during my visit to Luanda, Vihiga County,” Ruto aliandika kwenye twitter.

 

Ruto amabye alionekana mwenye furaha afanya mazungumzo ya kufana na rafiki huyo wake wa zamani na amabi alingana naye kwa jukwaa kuu.

image_of_dp_william_ruto_enjoying_a_hearty_conversation_with_former_schoolmate_sospeter_ojuwang_august_23_2019_0
Naibu rais William Ruto akutana na jamaa waliyesoma naye miaka 35 iliopita.

“Tulikumbushana matukio ya siku zetu za ujana, tulicheka pamoja na kumtakia heri njema,” Ruto alisema.

Wakenya walichangia kupitia mitandao ya kijamii baada ya picha za wawili hao kuchipuka. Kulingana na oicha Ruto alionekana barubaru huku rafiki yake akionekana mzee sana.

 

Pesa ni lotion my friends, spot the difference, loosely translating to, money is like fine body lotion my friends, spot the difference,” Frank Kiptoo aliandika kwenye twitter.

Baadhi ya wananchi nao walimtaka Ruto kumsaidia rafikiye kwa kumtafutia kazi.

 

Read here for more

Uhuru afanya mabadiliko katika serikali

Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika wizara za serikali kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.

Uhuru 2
Katika agizo la rais siku ya Ijumaa, Uhuru aliunganisha idara ya usalama wa ndani na ile ya uhamiaji.
Idara ya kitaifa ya mambo ya ndani na ile ya huduma kwa wananchi sasa zote zitakuwa chini ya wizara mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya kitaifa.

 
Idara ya kunyunyizia mashamba sasa imewekwa chini ya wizara ya maji kutoka wizara ya kilimo
Wizara hiyo sasa itajulikana kama wizara ya maji,usafi na unyunyiziaji. Wizara ya kilimo pia imebadilishwa jina na sasa itajulikana kama wizara ya Kilimo,mifugo na uvuvi.

 
Kitengo cha rais cha kuimarisha huduma kwa wananchi (The President’s Delivery Unit) kimehamishiwa katika wizara ya mambo ya ndani.

 

 

Mabadiliko haya yanaanza kutekelezwa mara moja.

Tabitha Karanja na mumewe waachiliwa kwa dhamana

Wakurugenzi wa kampuni ya Keroche Tabitha Karanja na mumuwe Joseph Karanja wameachiliwa kwa dhamana baada ya kufikishwa katika mahakama ya Milimani kujibu mashtaka ya ufisadi siku ya Ijumaa.

TABITHA.1 (1)

 

Tabitha Karanja aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 15 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au shilling milioni 10 pesa taslim. Mumewe Joseph Karanja aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au shilingi milioni mbili pesa taslim.

Ufisadi! Wakurugenzi wa Keroche wafikishwa kizimbani

Hakumu mkuu Francis Andayi hata hivyo amewapa siku saba kuwasilisha dhamana zao mahakamani. Mahakama hata hivyo imewaagiza wasalimishe paspoti zao. Wawili hao ambao walikamatwa Alhamisi baada ya kulala katika majengo ya kampuni hiyo walikanusha mashtaka yote kumi dhidi.

 

 

Tabitha alikesha katika korokoro ya polisi baada ya kuandikisha taarifa katika idara ya DCI, mumuwe Joseph Karanja hata hivyo aliachiliwa kwa dhamana ya polisi kutokana na hali yake ya kiafya.
Wakurugenzi wa Keroche wanadaiwa kukwepa kulipa ushuru wa takriban shilingi bilioni 14 pesa za Kenya.

 

 

Katika taarifa siku ya Jumatano, Karanja alisema kampuni yake haijashiriki ukwepaji wowote wa ushuru na kuongeza kwamba haikua haki kwa kampuni ya Keroche “kuhujumiwa na kudhalilishwa”

Aliyekuwa mshambulizi wa Ghana aiaga Dunia

Aliyekuwa mshambulizi wa Nottingham forest na timu ya taifa ya Ghana, Junior Agogo ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 40 kutokana na ugonjwa wa  Kiharusi.

 

AGOGO

Agogo alichezea taifa la ghana mara 27 kwenye mechi za kimataifa huku akicheka na wavu mara 11 maishani mwake. Alianzia soka yake na klabu cha Shefield United kabla ya kwenda nchini Marekani. Baadaye alirejea nchini Uingereza na kuchezea Brentford pamoja na Nottigham Forest.

Jesse Were arudishwa kwenye kikosi cha Harambee stars

Agogo alitetemesha ulimwengu wa soka akichezea klabu cha Bristol City. Vilabu alivyochezea vimesikitikia kifo chake na kutumia familia yake risala za rambi rambi.

Amekuwa akiugua maradhi ya kiharusi tangia mwaka wa 2015.

AGOGO 2

Soma Mengi hapa

Patanisho: Alitoka nyumbani bila sababu mwaka 2017

 

Bi. Emily alipiga simu akitaka kupatanishwa na mumewe,Fredrick aliyemwacha mwaka wa 2017. Wawili hawa wana mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na nusu.

gidi na ghost

Patanisho: Mke wangu alitoroka nyumbani na amekataa kurejea

 “Tulikuwa tumeishi vizuri na mume wangu lakini mwaka wa 2017 nilianza kuona tabia za kiajabu kutoka kwakee. Alianza kuja nyumbani kama amechelewa sana kitu saa nane usiku na akifika anasema ameshiba. Siku moja nilimwambia  kimchezo kama amechoka na mimi achukue virago vyake na aende zake. La kustaajabisha alichukua vitu na akaenda na hadi wa leo hajawahi kurudi.”

Emily amekua akizungumza na mumewe hata ikafikia kuwa mumewe anamtumia pesa kila wakati akimwitisha licha ya kwamba mumewe huyo amekataa kurudi nyumbani.

Tulipompigia bwana Fredrick simu alikataa kuzungumza nasi kwani alisema kuwa atampigia mkewe simu baadaye.

SOMA MENGI HAPA

Ufisadi! Wakurugenzi wa Keroche wafikishwa kizimbani.

Wakurugenzi wa kampuni ya Keroche Tabitha Karanja na mumuwe Joseph Karanja wamefikishwa katika mahakama ya Milimani kujibu mashtaka ya ufisadi.

TABITHA.1 (1)

 
Wawili hao ambao walikamatwa Alhamisi baada ya kulala katika majengo ya kampuni hiyo hata hivyo walikanusha mashtaka yote kumi dhidi yao mbele ya hakimu mkuu Francis Andayi.

Tabitha Karanja wa Keroche atiwa mbaroni

Tabitha alikesha katika korokoro ya polisi baada ya kuandikisha taarifa katika idara ya DCI, mumuwe Joseph Karanja hata hivyo aliachiliwa kwa dhamana ya polisi kutokana na hali yake ya kiafya.

 
Wakurugenzi wa Keroche wanadaiwa kukwepa kulipa ushuru wa takriban shilingi bilioni 14 pesa za Kenya.

Katika taarifa siku ya Jumatano, Karanja alisema kampuni yake haijashiriki ukwepaji wowote wa ushuru na kuongeza kwamba haikua haki kwa kampuni ya Keroche “kuhujumiwa na kudhalilishwa”

TABITHA
Walisafirishwa kutoka Naivasha hadi makao makuu ya DCI mjini Nairobi kwa mahojiano zaidi punde tu baada ya kukamatwa.

Wanawakilishwa na wakili James Orengo.

Matiang’i aonya wanasiasa wanaochochea umma dhidi ya Sensa

Waziri wa usalama Fred Matiang’i ametoa onyo kali kwa wanasiasa dhidi ya kuchochea wananchi kususia zoezi la kuhesabu watu kuanzia siku ya Jumamosi.

Matiang.i
Matiang’i alisema zoezi hilo halitahusisha mambo mengi na kwa hivyo halifai kuingizwa siasa.
Waziri alisema Kenya ni nchi ya kisasa na zoezi la kuhesabu watu la mwaka 2019 linafaa kufanyika kwa utaratibu mwafaka.

Matiang’i aamrisha mabaa yote yafungwe tarehe 24 na 25

Sudan: Abdalla Hamdok ateuliwa waziri mkuu

“Na wahimiza viongozi, hasa wanasiasa, kuunga mkono zoezi la kuhesabu watu. Hili ni zoezi la moja kwa moja na tuachie swala hilo hapo. Wacha tuliendeshe kwa adabu,” Matiang’i alisema.

 
Matiang’i alizungumza siku ya Alhamisi baada ya mkutano wa mwisho wa jopo la mawaziri linaloendesha zoezi la kuhesabu watu la mwaka huu. Alisema serikali inafahamu na inaendelea kupiga msasa shughuli za wanasiasa ikiwemo mikutano ambayo huenda ikatumiwa kuchochea wananchi.

 
“Tuna tathmini shughuli zao. Tunajua mikutano iliofanyika jana usiku. Mwishowe utakabiliwa kisheria.Tujiepushe na njama kama hizi,” Alisema.

 
Waziri alikuwa ameandamana na mawaziri wengine Ukur Yatani (Fedha), Joe Mucheru (ICT) na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya takwimu nchini (KNBS) Zachary Chege. Serikali ilithibitisha kuwa mipango ya zoezi la kuhesabu watu imekamilika.

Sudan: Abdalla Hamdok ateuliwa waziri mkuu

BBC

Sudan imemteua Waziri Mkuu mpya ikiwa nchi hiyo ikiwa kwenye utawala wa mpito wa miaka mitatu chini ya uongozi wa jeshi.

Abdalla Hamdok

Waziri Mkuu Abdalla Hamdok anasema kuwa kipaumbele chake ni upatikanaji wa amani na kutatua changamoto ya kiuchumi .  Uteuzi wake umekuja wakati ambapo Luteni Abdel Fattah Abdelrahman Burhan alichaguliwa kuwa kiongozi mpya wa baraza huru.

 

 

Serikali mpya itaongoza taifa hilo mpaka kipindi cha uchaguzi. Kumekuwa na vurugu kwa miezi kadhaa ambayo imesababisha vifo vya waandamani wengi.  Upande wa upinzani una matumaini kuwa uteuzi mpya utaweza kusaidia kumaliza utawala wa kijeshi. Migogoro nchini Sudan ilianza kwa waandamanaji mwishoni mwa mwaka jana wakati ambapo Omar al- Bashir alipoondolewa madarakani baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 30.

 

Bwana Hamdok ameapishwa kama waziri mkuu wa mpito alipowasili kutoka Ethiopia, eneo alilokuwa akifanyia kazi kama mtaalamu wa uchumi wa umoja wa mataifa(UN) tangu mwaka 2011 kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka jana.

 

 

“Vipaumbele vya kwanza vya serikali ni kusitisha vita, kuimarisha usalama, kuuza uchumi na kujenga uhusiano mzuri na sera za mataifa ya kigeni,” aliwaambia waandishi wa habari.

 

Mwaka jana, Hamdok alichaguliwa na Bashir kushika nafasi ya waziri wa fedha lakini alikataa, shirika la habari la AFP.

 

Kuapishwa kwa Hamdok na uwepo wa baraza huru inaonyesha utofauti kwa mara ya kwanza tangu Sudan ikiwa haipo chini ya utawala wa kijeshi tangu Bashir aingie madarakani mwaka 1989 . Baraza huru inachukua nafasi ya utawala wa mpito wa majeshi wakati ambapo utawala wa kiislamu ulipoondolewa baada ya maandamano makubwa.

 

 

Gen Burhan atawaongoza viongozi sita wa kiraia na wengine wanne wa kijeshi kama mpango wa wa muda mrefu wa miezi 39 kuelekea kwenye demokrasia.

BBC

Tabitha Karanja wa Keroche atiwa mbaroni

Aifisa mkuu mtendaji wa Keroche Tabitha Karanja ametiwa mbaroni na makachero wa DCI katika afisi za kampuni yake eneo la Naivasha.

TABITHA
Maafisa wa KRA na wachunguzi wa DCI walikuwa wamepiga kambi katika majengo ya kampuni hiyo kuanzia Alhamisi asubuhi kufuatia kutolewa kwa agizo la kukamatwa kwake na mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji.

 

Mahakama yakosoa DCI kwa kumkamata bwenyenye, Humphrey Kariuki

Tabitha alikamatwa pamoja na mumewe Joseph Karanja kwa madai ya ukwepaji wa ushuru wa takriban shilingi bilioni 14.

 
Katika taarifa siku ya Jumatano, Karanja alisema kampuni yake haijashiriki ukwepaji wowote wa ushuru na kuongeza kwamba haikua haki kwa kampuni ya Keroche “kuhujumiwa na kudhalilishwa”

Kitany amvua nguo seneta Linturi, hakamani

Walisafirishwa kutoka Naivasha hadi makao makuu ya DCI mjini Nairobi kwa mahojiano zaidi.
Kampuni hiyo inadaiwa kukosa kulipa ushuru wa mhuri wa thamani ya bidhaa (VAT) kwa kima cha shilingi bilioni 12.34 , (milioni 329.4),kwa kinywaji cha Crescent Vodka (milioni 135.4 ) miongoni mwa bidhaa zingine.