Uchaguzi wa Amerika; Joe Biden amtaja seneta Kamala Harris kuwa mgombea mwenza

Mgombeaji wa urais kwa tiketi ya chama cha Democtratic Joe Biden siku ya Jumanne alimteua seneta Kamala Harris kuwa mgombea mwenza wake, na kumfanya mwanamke wa kwanza wa asili ya Afrika kuwa kwenye tiketi ya urais kwa chama kikuu katika historia ya Marekani.

Soma mhabari zaidi;

Seneti kwa mara ya nane yashindwa kukwamua utata wa mfumo wa ugavi wa mapato

 

Harris atapiga jeki kampeni za Biden dhidi ya rais Donald Trump wa Republican  huku kukiwa na uhasama  wa kijamii kuhusu unyanyasaji wa raia kwa misingi ya rangi na dhulma za polisi dhidi ya wananchi wenye asili ya kiafrika nchini humo.

Biden amekuwa na shinikizo kuchagua mwanamke mwenye asili ya kiafrika kuwa mgombea mwenza wake. Biden na Harris watafanya mkutano wao kwanza pamoja wakiwa kwa tiketi moja ya urais leo Jumatano nyumbani kwake Biden mjini Wilmington, Delaware.

kamala 1

“Ni heshima kubwa sana kumchagua @KamalaHarris — mpiganaji jasiri wa mtu mdogo, na moja wapo wa watumishi bora wa umma – kama mgombea mwenza wangu ,” Biden alisema kwa  Twitter.

Harris ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kuchaguliwa seneta alipochaguliwa mwaka 2016, atategemewa sana kushawishi kura za watu wenye asili ya kiafrika – ambao wengi wao ni wafuasi wa chama cha Democratic.

Miaka minne iliyopita hatua ya kutopata uungwaji mkono kutoka kwa watu wa asili ya kiafrika kulipelekea mgombeaji wa Democratic Hillary Clinton kubwagwa na Donald Trump.

 

Soma mhabari zaidi;

Toto saafi! Picha za muigizaji Maria akiwa amejipodoa zawazuzua wakenya

Biden ambaye campaign zake za mchujo wa chama cha Democratic ziliokolewa na wapiga kura weusi katika jimbo la South Carolina mwezi Februari, anahitaji sana uungwaji mkono thabiti kutoka kwa wapiga kura weusi dhidi ya Trump. Kivumbi kitatifuliwa katika majimbo kama vile Michigan, Pennsylvania na Wisconsin ambamo Trump alishinda kwa pengo dogo mwaka 2016. Kura za maoni sasa zaonyesha kwamba biden anaongoza katika maeneo hayo.

 

Siogopi ‘system au deep State’ Ruto afoka

Naibu rais William Ruto kwa mara nyingine tena amesema kamba haogopi kile wapinzani wake wanaita ‘deep state’ au ‘system’ ambayo anasema juhudi zake ni kusambaratisha azma yake ya urais.

Ruto alisema kwamba ikiwa agekuwa muoga, yeye na rais Uhuru Kenyatta hawangeunda serikali ya sasa.

Soma habari zaidi;

Mwanafunzi wa chuo kikuu ashtakiwa kwa kumbaka mpenzi wake wa zamani

“Kama rais Uhuru na mimi tungekuwa waoga, hatungeunda serikali chini ya JP. Tulitishwa na madai mengi, ikiwemo kesi zetu za ICC wakati huo, ambazo zilikuwa uongo,” Ruto alisema.

Naibu rais alizungumza siku ya Jumanne nyumbani kwake mtaani Karen Nairobi alipokuwa mwenyeji wa viongozi wa jamii kutoka eneo bunge la Kajiado Kusini, wakiongozwa na mbunge Katoo Ole Metito na Seneta Mary Seneta.

https://youtu.be/Ejli_IHMcDY?t=94

Matamshi ya Ruto pia yanajiri baada ya naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe kuwaambia wakenya kujiandaa kwa uongozi wa Raila mwaka 2022.

Murathe alikuwa amesema kwamba Raila amepigania nchi hii sana na anastahili kuzawadiwa.

murathe1

Ruto alisema kwamba matokeo ya uchaguzi wa 2022 yataamuliwa na wapiga kura, na kupuuzilia mbali ushawishi wa ‘deep state au system’.

“Eti kuna watu fulani wameketi mahali ambao watafanya uamuzi.”

Soma habari zaidi;

‘Papa Shirandula alikasirika sana nilipopata ujauzito.’ Awinja Asimulia

 

Ruto aliongeza kuwa wapiga kura watakuwa na usemi wa mwisho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Naibu rais alitowa wito kwa viongozi waliochaguliwa kusimama wima dhidi ya nguvu zozote zinazolenga kuhujumu ahadi zao za uchaguzi.

 

 

Seneti kwa mara ya nane yashindwa kukwamua utata wa mfumo wa ugavi wa mapato

Seneti siku ya Jumanne kwa mara ya nane ilishindwa kupata suluhu kwa utata unaozingira mswada wa ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti.

Huku ikionekana kuwa maseneta walikuwa tayari wanaelekea kupiga kura, kiongozi wa wachache James Orengo aliingilia kati na kubadili mkondo wa mjadala.

Soma habari zaidi;

Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi ajiuzulu

Orengo alisema seneti haiwezi kupigia mswada huo kura na ilhali palikuwepo mabadiliko yaliyokuwa wamependekezwa na kamati ya seneti ya Fedha na Bajeti.

James Orengo
James Orengo

Mabadiliko hayo yanapendekezwa na seneta maalum Petronilla Were, Kimani Wamatangi (Kiambu), Ledama Olekina (Narok) na James Orengo wa Siaya.

Were anataka pendekezo la Tume ya ugavi wa mapato kukubaliwa kama mfumo wa tatu wa ugavi mapato.

Hata hivyo, seneta huyo anapendekeza kuwa mfumo wa sasa uendelee kutumika na kwamba mfumo wa tume ya CRA uanze kutumika wakati kiasi za mgao wa usawazishaji utakapopandishwa hadi shilingi bilioni 348 kutoka kiasi cha sasa cha bilioni 316.5.

Soma habari zaidi;

‘Mara nyingi hatukuwa tunazungumza tukiigiza,’ Wilbroda azungumzia uhusiano wake na Papa Shirandula

Hoja ya Orengo ilimlazimu Spika kuahirisha upigaji kura ili kuruhusu mjadala kuhusu mapendekezo hayo mapya.

Maseneta sasa watakuwa na kikao siku ya Alhamisi kujaribu kukwamua swala hilo hili.

Aliyekuwa mbunge wa Garsen Danson Mungatana akamatwa

 

Aliyekuwa mbunge wa Garsen Danson Mungatana siku ya Jumanne alikamatwa na maafisa wa DCI katika hoteli moja mjini Nairobi.

Munagatana alipelekwa katika makao makuu ya DCI kuhusiana na madai ya kupokea pesa kwa njia ya udanganyifu.

Soma habari zaidi;

Sasa unataka kulia?Murkomen wajibizana na Kang’ata

 

Mfanyibiashara aliyekuwa amempa pesa alishuku wakati alipoitishwa pesa zaidi  na kupiga ripoti kwa polisi.

Court-Gavel-Thumb
Court-Gavel-Thumb

 

Mkutano kisha ulipangwa katika hoteli moja mjini Nairobi ili wakutane na ni hapo ambapo Mungatana alitiwa mbaroni pamoja na mwanamume mwingine kwa jina Collins Waweru, aliyekuwa amesema ana uwezo kufanikisha makubaliano baina ya Mungatana na mfanyibiashara huyo.

Soma habari zaidi;

Covid 19 : Urusi yapata chanjo ya coronavirus Putin asema imeidhinishwa kwa matumizi

 

Mwaka jana mwezi Aprili, Mungatana alikuwa miongoni mwa washukiwa 26 walioshtakiwa katika mahakama ya Malindi kwa madai ya kupokea shilingi milioni 51 kwa njia ya ufisadi.

Maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi walimkaamata Mungatana baada ya kuvamia boma lake mjini Nairobi.

Sure Bet!! Tazama picha za mkewe Murkomen mwenye urembo wa kupindukia

Seneta Kipchumba Murkomen anafahamika sana katika sekta ya siasa, lakini hawakukosea katika kila mafanikio ya wanamume lazima kuwe na mwanamke yaani kwa kimombo( It’s said that behind every successful man there is a woman) na kwa kiongozi huyo methali hiyo imetimia kwa kumpata mkewe.

Akiwa kwenye mahojiano alisema kuwa mkewe alikuwa mwanamfunzi mwenzake, walikuwa wanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha Nairobi.

Walichumbiana kwa miaka kumi, kabla ya kufunga pingu za maisha na bado upendo wao unazidi kunoga. Wawili hao wamebarikiwa na watoto wanne na mkewe anafahamika kama Gladys Wanjiru,

Kwa kweli  ndoa si kitanda cha maua, wawili hao ni wakupigiwa mfano na ndoa yao kutamanika na wengi.

Hizi hapa baadhi ya picha zao;

senatormurkomen_90088655_2480052415641346_8923822421721249011_n-1

senatormurkomen_82117571_251987642459314_2032959499885017831_n-1-696x869

 

 

 

 

Sasa unataka kulia?Murkomen wajibizana na Kang’ata

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na kiranja wa wengi katika seneti Irungu Kang’ata Jumanne alizua cheche za maneno kwenye mitandao ya kijamii ya instagram mbele ya kikao cha seneti kuhusu fomula ya ugavi wa pesa.

‘Nilipoondolewa niliongea na rais mara moja,’ Murkomen afichua haya

Inadaiwa kuwa timu ya Murkomen inaunga mkono ugavi wa pesa hasa wale wananufaika kutokana naugavi wapesa katika kaunti.

Kanga’ata alimkejeli Murkomen huku akisema kuwa kaunti kama Nyeri na Mutang’a watapoteza fedha zao ilhali anaunga ugavi wa pesa mkono.

“Linturi na Murkomen ugavi wa pesa utaadhibu kaunti kama Nyeri kwanini? tumekukosea wapi?” Aliandika Kang’ata.

Irungu Kangata
Irungu Kangata

Murkomen naye alikuwa na haya ya kusema,

“Wacha kupagawa na mimi kwa sasa huko kwenye uongozi, heshimu msimamo wangu kama mtu wa nyuma na uongoze.”

Murkomen aapa kupinga mswada wa ugavi wa mapato ya taifa

Kang’ata naye alisema kuwa Murkomen amepinga pendekezo hilo ambapo kaunti 39 zitanufaika na ugavi wa pesa, huku kaunti 8 zikipoteza kutokana na ugavi huo.

Murkomen

“Sasa unataka kulia.” Murkomen alimuuliza.

Mjadala wa ugavi wa pesa unaendelea, huku wengi wakingoja kwa hamu nini kitakachotokea.

15 waaga dunia huku 497 wakipatikana na virusi vya corona

Watu 15 wameaga dunia kwa ajili ya virusi vya corona katika saa 24 zilizopita .

Katibu wa utawala wa wizara ya Afra Mercy Mwangangi  amesema hayo wakati akitangaza kwamba Kenya imesajili visa vipya 497 vya ugonjwa huo nchini  kutoka sampuli  4171 na kufikisha jumla ya visa hivyo  nchini kuwa 27425.  Kati ya waliopata ugonjwa huo 467 ni wakenya ilhali 30 ni  raia wa kigeni .

Wagonjwa  312 ni wanaume ilhali 185 ni wanawake . Mwangangi pia ametangaza kwamba 372 wamepona idadi inayofikisha jumla ya watu waliopona ugonjwa huo hadi sasa kuwa 13,867.

Covid 19 : Urusi yapata chanjo ya coronavirus Putin asema imeidhinishwa kwa matumizi

Kati ya watu 15 walioaga dunia ,11 walikuwa na matatizo ya awali ya kiafya na idadi hiyo sasa inafikisha 438 walioangamia kwa ajili ya virusi vya Covid 19 nchini .

Covid 19 : Urusi yapata chanjo ya coronavirus Putin asema imeidhinishwa kwa matumizi

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba chanjo iliyotengenezwa ndani ya Urusi kwa ajili ya ugonjwa wa Covid-19 imeidhinishwa kwa matumizi baada ya kufanyiwa majaribio kwa binadamu chini ya miezi miwili.

Bwana Putin amesema kwamba chanjo hiyo imepita vigezo vyote vilivyowekwa na kuongeza kwamba binti yake tayari amepatiwa.

Maafisa wamesema kuwa wanampango wa kuanza kutoa chanjo hiyo kwa umma kuanzia Oktoba.

Wataalamu wameonesha wasiwasi wao kuhusu kasi ya kazi ya Urusi na kusema kuwa watafiti huenda wametumia njia za mkato.

Huku wasiwasi ukiendelea kuhusu uwezekano wa usalama kuingiliwa wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitaka Urusi kufuata miongozo ya kimataifa ya kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Chanjo iliyotengenzwa na Urusi sio miongoni mwa orodha ya zile za WHO ambazo zimefika awamu ya tatu ya majaribio kunakohusisha majaribio kwa watu wengi zaidi.

 

Subiri urogwe! Zari Hassan amwambia Mama Dangote

Kwa Muda sasa Sandra yaani mama Dangote amekuwa akimposti mjukuu wake  Latiffah Dangote (Princess Tiffah) kwenye mitandao ya kijamii.

Katika moja wapo ya posti zake Zari Hassan alitoa maoni huku akimwambia mama ya staa wa bongo aweze kusubiri arogwe.

“Umezidi,subiri urogwe.” Aliandika Zari.

Unampeza Diamond,’Mashabiki wamwambia Zari baada ya kutoa maoni kwa ujumbe wa Diamond

Maoni yake hayakupokelewa vyema na mashabiki wake Hamisa Mobetto ambapo walisema kuwa alikuwa ana mkejeli na kumkosoa Hamisa.

tii

Wanamitandao walidai kuwa Zari alimaanisha kuwa Hamisa anaweza roga Mama Dangote ili hasimpende mjukuu wake vile anavyompenda.

Drama! Akothee aeleza kwa nini aliacha kumfuata Zari kwenye Instagram

Itasalia kwenye kumbukumbu za wanamitandao na watu wengi kuwa Diamond alijitokeza na kusema kuwa kuna wakati Hamisa alikuwa anataka kumroga.

Ilikuaje:Nilikataliwa na familia yangu kwa maana sikuwa na baba

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye country man, ambapo alilelewa bila baba na alikataliwa, na jamii sana baada ya kuachwa na mama yake akiwa na umri wa chini alianza kuuza majani chai.

“Nilikuwa naenda wiki mbili shuleni na wiki zingine mbili naenda kutafuta pesa, nilikuwa nalipwa shillingi mbili, nilitaani maisha ya watu wenye hawana mwelekeo

Nilianza wizi nikiwa darasa la nane, nilienda shule ya upili nilipokuwa naenda shule jamaa zangu walinifanyia matayarisho ya shillingi 21 nilipofika shulleni nilianza kuiba mpaka nikafukuzwa

Nilienda kuzurura Nakuru wakati mmoja kwa maana nilikuwa na machungu ya kukataliwa na familia yangu, tulimvamia mjomba wangu na hata kumnyang’anya pesa tukapelekwa polisi

Kesi yetu iliposikizwa nyanya yangu alinitetea na hata kunifukuza na kuniambia niende kabisa.” Alieleza Country Man.

Baada ya Muda Country Man alikuja Nairobu ambapao aliendelea na kazi yake ya wizi na hata kukamatwa na polisi na kupata kifungo cha miaka mitatu kwa kufanya uhalifu.

Alipotoka jela kwa mara ya kwanza alirudi tena baada ya kukata mtu mwingine bali hakupenda kufanya hayo kwa maana alikuwa na maumivu na machungu kwenye moyo wake kwa kuachwa.

Baada ya kutoka jela Country Man alianza kuchota maji huku akilipwa, licha yake ya kuchota maji alikuwa na chawa ambazo watu walikuwa wakiziona hata akianika nguo zake.

Baada ya muda Aliokoka na kuanza kubadilisha maisha ya vijana wengi.

Kwa mengi zaidi tembelea youtube yetu.