Serikali haitalegeza sheria kuhusu michezo ya kamari asema waziri Matiang’i

Serikali haina mpango wa kuyelgeza sheria kuhusu michezo ya kubashiri amesema waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i. Kuanzishwa kwa sheria hizo kali kulifanya kampuni nyingi za  michezo ya kubashiri kufungwa nchini na kulikuwa  matumaini kwamba huenda zikarejelea oparesheni baada ya kulegezwa  kwa baadhi ya sheria hizo .

Ni Kubaya!KQ yawatuma wafanyikazi kwa likizo ya bila malipo kabla ya awamu nyingine ya kuwachisha kazi

Matiang’I aliyekuwa akizungumza katika taasisi ya KICD katika mkutano na viongozi kutoka Murang’a  amesema  amekuwa akipokea simu kutoka kwa viongozi wa kidini wanaohofia kwamba huenda michezo hiyo ya kubashiri ikirejea tena na kuwateka vijana baada ya sheria kulegezwa ili  kuruhusu kampuni hizo  ziendelee na oparesheni yazo nchini

“ Hatutabadilisha sheria hizo kwa sababu tunataka unadhifu enya .michezo ya kamari nusura iiharibu Kenya .wahalifu na watu  wanatakatisha fedha  walikuwa wakinawiri na wengine walikuwa wmetoka mashariki mwa Uropa.walikuwa wakifanya mambo ambao hawangeyafanya katika mataifa yao’ amesema Matiang’i

Waziri huyo  amesema  kwamba serikali inaheshimu uamuzi wa bunge kuhusu suala hilo  huku akiongeza  kwamba hakuna leseni iliyotolewa kwa kampuni ya michezo ya kubashiri mwaka huu wa kifedha  kwa sababu wanangoja idhini ya wizara ya afya  kwa ajili ya janga la corona .

Uhuru ahamia Jumba la Harambee kutoka Ikulu kwa ajili ya COVID 19

Dr Matiang’I Pia amesema  serikali  hivi karibuni itaanzisha awamu ya pili ya msako dhidi ya  pombe haramu na  dawa za kulevya katika kaunti za Murang’a na Kiambu .

 

 

Ni Kubaya!KQ yawatuma wafanyikazi kwa likizo ya bila malipo kabla ya awamu nyingine ya kuwachisha kazi

Shirika la safari za ndege  nchini Kenya Airways  limewataka wafanyikazi wake  ambao huduma zao hazihitajiki linaporejelea oparesheni zake kuchukua likizo ya  bila malipo .

Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo  Allan Kilavuka amesema  maelekezo hayo yanaanza kutekelezwa julai tarehe 6 .

Kupitia taarifa kwa wafanyikazi wake KQ imewataka wale ambao huduma zao hazitahitajika kwa sababu hapatakuwa na shughuli  nyingi za usafiri kuchukua  likizo hiyo ya bila malipo kuanzia julai tarehe sita .

Uhuru ahamia Jumba la Harambee kutoka Ikulu kwa ajili ya COVID 19

Amesema uamuzi huo umechukuliwa ili kuwapa fursa ya kuzungumza na washirika pamoja na wadau wengine kuamua hatua bora zaidi kwa wafanyikazi wa shirika hilo na kampuni nzima .

“ Ingawaje sote tumeweka juhudi kabambe za kuhakikisha kwamba tunaendelea na biashara yetu ,hali imekuwa ngumu na changamoto zilizopo ni nyingi kuendelea na  oparesheni zetu’ amesema afisa huyo mkuu

Matiang’i: Kenya iko tayari kurejelea usafiri ndani na nje ya nchi

Amesema tathmini yao imeeleza kwamba itawalazimu kupunguza idadi ya wafanyikazi  hata wanapoanza kurejelea oparesheni baada ya sekta nzima ya usafiri wa angani kuvurusgwa pakubwa na  janga la corona .

Kilavuka amesema kwa ajili ya uhaba wa watu wanaosafiri ndege zao nyingi zitasalia bila shughuli na hivo basi wafanyikazi wengi hawatahitajika .

 

 

 

No apologies !Anita Nderu asimama kidete na uamuzi wake wa kuwaleta mashoga katika kipindi chake

Mtangazaji Anita Nderu amesimama kidete na uamuzi wake wa kuwaleta mashoga katika kipindi chake cha upishi Instagram. Akizungumza na Massawe Japanni   katika kipindi chake cha Ilikuaje kwa njia ya simu ,Nderu amesema ingawaje anaheshimu maoni ya watu na misimamo yao kuhusu ushoga ,katu hataomba radhi kwa uamzi wa kuwaleta rafiki zake hao  ambao ni wapenzi wa jinsia moja

Hot Soup: Anita Nderu apondwa mtandaoni kwa kuwashirikisha wanaume shoga katika kipidi chake cha upishi

Nderu alizua mhemko mtandaoni baada ya kurushiwa cheche za shutuma  na watu wengi kwa kuwaleta wapenzi wa jinsia moja katika kipindi hicho ambapo walionekana wakipika na kufanya densi densi mtandaoni . baadaye   watu wengi walianza kumtumia jumbe za kumkashifu kwa upotofu wa maadili  wakimtaka aiondoe video hiyo mtandaoni lakini hajatikisika .

Alipoulizwa na Massawe iwapo naye pia ni shoga amesema hilo ni jambo la kibinafsi na atajitokeza endapo itahitajika au  wakati ufaao ingawaje kwa sasa amebainisha wazi kwamba anaunga mkono wa  jamii ya LGBTQ.

Abomination! Mwanamke avua nguo na kusalia uchi mbele ya mwanawe akisherehekea birthday yake,ni sawa?

Ameongeza kwamba  hatosita kuwaleta tena watu  wa jinsia moja katika makala yajayo ya kipindi chake instagram kwani  kila mtu anafaa kuheshimu maoni ya wengine .

‘Nakataa kuomba msamaha kwa kuwaruhusu rafiki zangu kuwa jinsi walivyo,nakataa kuomba msamaha kwa kupeperuha episode hiyo kwa sababu ni yangu ,ingawaje naheshimu uamuzi wa wale ambao hawajapendezwa na kipindi hicho’

 

 

 

Mhudumu wa boda boda Uganda ajiteketeza baada ya ‘kuitishwa hongo’

Mhudumu mmoja wa boda boda nchii Uganda aliye na umri wa miaka 29 ameaga dunia baada ya kujitia moto  ndani ya kituo cha polisi .

Pikipiki ya Hussein Walugembe ilinaswa na polisi katika wilaya ya masaka siku ya jumatatu  na  akatakiwa kulipa rushwa ya takriban shilingi elfu 4  ili arejeshewe lakini hilo halikumfurahisha .idara nzima ya trafiki katika eneo hilo sasa ipo chini ya uchunguzi kwa mujibu wa  msemaji mmoja wa polisi .

Polisi wa Lamu afungwa jela maisha kwa ubakaji wa mwanamke

Pia inaripotiwa kwamba  Walugembe  alikuwa akiishi katika makaazi ya polisi na alikuwa akiwazuia maafisa hao chakula . Nchini Uganda usafiri wa boda boda umepigwa marufuku  katika baadhi ya nyakati  ili kuzuia  maambukizi ya virusi vya corona na mara kwa mara polisi hufanya msako wa kuwakamata wahudumu wanaokaidi marufuku hiyo .

Wahudumu hao wanaruhusiwa kufanya kazi zao kuanzia saa kumi na mbili alfajiri na  hadi saa kumi na moja jioni na  wanaweza tu kusafirisha mizigo .

Hot Soup: Anita Nderu apondwa mtandaoni kwa kuwashirikisha wanaume shoga katika kipidi chake cha upishi

Polisi wanasema  Walugembe  alikuwa amempa rafiki yake pikipiki yake aliyepatikana akimsafirisha abiria hatua iliyosababisha kunaswa kwa pikipiki hiyo . Baadaye alifadhaishwa na kutibuka kwa  juhudi zake kutaka pikipiki yake iachiliwe  ndiposa akaamua kujifungia katika chumba kimoja ndani ya kituo cha polisi na kujiteketeza kutumia  mafuta petrol aliokuwa ameficha kweye chupa .

 

Polisi wa Lamu afungwa jela maisha kwa ubakaji wa mwanamke

Afisa mmoja wa polisi aliyekuwa akihudumu huko Lamu amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke mmoja  aliyekuwa amekwenda kupiga ripoti katika kituo cha polisi .

Rodgers Ouma,  mwenye umri wa miaka 28  pia atahudumia kifungo cha miaka 10 jela  kwa kutumia vibaya maamlaka yake  na  kulipa shilingi laki nne kwa  mwathiriwa kama fidia .

Mwanamme aliyeachwa na jeneza la mkewe Meru kuishtaki serikali

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma amesema  upande wa mashtaka umethibitisha kesi yao dhidi ya mtuhumiwa bila shauku  kwamba Ouma alimhadaa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26 hadi katika nyumba yake disemba  mwaka wa 2019 na kumfanyia unyamahuo .

Haji kupitia kwa taarifa amesema   mwanamke huyo alikuwa amekwenda kuripoti kwamba mumewe alikuwa akimlazimisha kutumia tembe za kuavya mimba ilia to euja uzito aliokuwa nao .

Nipe Nikupe:Maseneta walimana makonde baada ya ushindi wa Ole Kina

Hakimu aliyeshughulikia kesi hiyo Allan Temba  amesema Ouma alitumia vibaya maamlaka yake kwa kuahidi mwanamke huyo kwamba angemsaidia na kesi aliokuwa amekwenda kuripoti .

 

 

 

 

Watu 247 wapatikana na virusi vya corona

Akitoa taarifa ya kila siku kuhusiana na virusi vya corona ,katibu msimamizi katika wizara ya afya Rashid Aman amesema watu 247 waoatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi nchini kuwa 7,188.

Watu 39 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 2,149 waliopona.

Wagonjwa wawili wamefariki na kufikisha watu 154 waliofariki kutokana na virusi hivyo.

Image

Kati ya visa hivyo vipya,wakenya ni 242 huku watu 5 wakiwa raia wa kigeni.

Wanaume ni 164 huku wanawake wakiwa 63,waathiriwa wakiwa kati ya miaka 1 na 100.

Nairobi imesajili visa 154 kati ya visa vipya vilivyosajili huku kaunti ya Mombasa ikiwa na watu 35.

Kaunti zingine zilizoathirika ni  Kajiado 15, Busia 12, Kiambu 12, Uasin Gishu 4, Machakos 4, Garissa 4, Murang’a 2, Nakuru 2, Siaya 2, Lamu 1, & Nyamira 1.

Wakati uo huo Aman amewataka wazazi kuwapeleka wasichana wa miaka 10 kupata chanjo ya HPV.

Visa vilivyosajiliwa katika kaunti ya Nairobi vimetokea maeneo, yafuatayo Kibra (35), Westlands (28), Dagoretti North (16), Kasarani (13), Embakasi East (12), Starehe (10), Langata (8), Makadara (6), Embakasi South (5), Embakasi West (4), Kamukunji (4), Roysambu (4), Dagoretti South (3), Ruaraka (3), & Embakasi Central (2).

Mungu hakupi vyote! Wema Sepetu afichua hofu yake

Mwanasosholaiti Wema Sepetu amefichua ukosefu  wa usalama wa miguu yake kupitia kwenye mitandao ya kijamii alieleza jinsi ilivyokuwa vigumu kwake kujikubali licha ya kuwa na miguu konde.

“TAHADHARI JAMANI NATOA… SIPENDI KUSEMWA MIGUU YANGU… MAANA MWENYEWE NAJIJUA MIGUU MIZURI SIKUBARIKIWA REASON HAMNIONI NIKIJI ASSOCIATE NA VITU VYA KUREVEAL MAMBO ZA HUKO CHINI…😂😂😂 NDO MAANA WANASEMA MUNGU HAKUPI VYOTE… BASI NIKIJIJUA MWENYEWE YATOSHA KWANI LAZIMA MNIAMBIE…”

Wema hakutia kikomo bali alikuwa na haya ya kunakili,

wema sepetu
wema sepetu

“WENGINE MNASEMA UKUTE MIGUU ZENU NI VITU MBAYA SANA PIA…🤦🏼‍♀️🤨 HAYA NDO MIGUU ZANGU HIZO APO MEZIONESHA… ENDELEENI KUSEMA SASA… 🤣🤣 NMEANDIKA HII CAPTION NACHEKA SANA KWAKWELI… SEMA KIUKWELI KWA MIGUU HAPANA.. SIO MAJAALIWA YANGU…🙈🙈🙈.” Alizungumza Wema.

Mapema mwaka huu aliwaacha wengi midomo wazi baada ya kupoteza kila 50.

Meneja wa Diamond Babu Tale kugombea kiti cha ubunge baada ya kifo cha mkewe

Meneja wa staa wa bongo Diamond Platnumz Babu take anawania kiti cha ubunge, hii ni baada ya WCB kutangaza habari hizo kwenye mitandao yao ya kijamii.

Kupitia kwenye mitandao hiyo lebo hiyo iliposti picha ya Babu na kuandika ‘chama cha mapinduzi CCM’.

Hili linajiri siku chache baada ya kumzika mkewe Shamsa.

“CHANGAMOTO NI SEHEMU MOJA KATIKA MAISHA YETU WANADAMU HIVYO KWA CHANGAMOTO NA MITIHANI UNAYOPITIA ISIKUFANYE UKATE TAMAA, ISIKUFANYE URUDI NYUMA SISI TUNAIMANI NA WEWE NA TUNAAMINI UNAWEZA KWASABABU SIFA ZOTE ZA UONGOZI UNAZO.

25022390_526130901093081_7379466259408093184_n

KWA KIPINDI CHOTE TUMEFAHAMIANA UMEKUWA DEREVA MZURI KWETU NA KWA JAMII PIA NA HILI LIKO WAZI.”

Pia lebo hiyo ilisema kuwa atagombea kiti cha ubunge katika mji wa Morogoro.

“NI MUDA SASA WA KUWATUMIKIA WANANCHI WA MKOANI KWAKO MOROGORO VIJIJINI.

USHATIA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MOROGORO VIJIJINI HIVYO CHANGAMOTO NA MITIHANI ULIYONAYO ISIKUFANYE URUDI NYUMA INUKA PANGUSA VUMBI ANZA SAFARI NASI TUKO NYUMA YAKO BEGA KWA BEGA KUHAKIKISHA LENGO LAKO LINAFANIKIWA @BABUTALE MBUNGE MTARAJIWA MOROGORO VIJIJINI #GOTALE #NENDATALE #HAPAKAZITU #TANZANIAYASASA CC @IKULU_MAWASILIANO
@CCMTANZANIA.”

Baada ya kuwaongoza wasanii wa lebo hiyo sasa wakati umewadia wa kuwatumikia wananchi.

 

Uhuru ahamia Jumba la Harambee kutoka Ikulu kwa ajili ya COVID 19

  Rais Uhuru Kenyatta  amehamia jumba la Harambee baada ya ikulu kufungwa wafanyikazi wanne walipopatikana na virusi vya corona .

Rais Kenyata  amesema hajapatikana na virusi hivyo na amekuwa akifanya kaz katika jumba la Harambee  iliyotajwa kuwa salama .wafanyikazi wake pia wamehamia jengo hilo naye .

Rais Kenyatta amekuwa akifanyia kazi Ikulu ya Nairobi hadi  visa vya corona vilivporipotiwa Juni tarehe 15 katika makao hayo yake .mikutano yake yote sasa  imekuwa ikifanyika Harambee .

Kabla ya visa hivyo vya corona kuripotiwa Ikulu rais alikuwa akiandaa mikutano  yake  yote  ikiwemo na wabunge  na baadhi ya wanasiasa katika Ikulu .

Wazazi wangu waliachana nikiwa na miaka kumi-Mercy Kyallo

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Mercy Kyallo dada yake Betty Kyallo, uvumi umekuwa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wamekosana.

Betty alipokuwa akizindua saluni yake dada yake Mercy hakuhudhuria hafla hiyo kwa maana kuna ugomvi kati yao.

“Betty amechangia katika umaarufu wangu katika biashara yangu, nilipofutwa kazi nilikaa nyumbani miezi miwili nikiwa na mawazo chungu nzima

Wakati wa kufutwa kazi nilikuwa na mpenzi ambaye alinipa ushauri na kunitia moyo sana.” Alieleza Mercy.

106348428_130684815339860_9154683499459287266_n

Alipoulizwa kuhusu baba yake alikuwa na haya ya kueleza,

“Nakumbuka baba yangu alienda ulaya kutafuta kazi nikiwa na miaka kumi, hapo ndipo waliachana na mama yangu kusema ukweli tulisumbuka sana lakini namshukuru Mungu kwa maana ametuwezesha

Baba yangu yuko hai na huwa tunazungumza licha yake kuachana na mama yangu.”

Miezi michache iliyopita Mercy alikejeliwa sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumkashifu rafikiye aliyekuwa mume wake Betty Kyallo, hii ni baada ya mwanawe betty Ivanna kulazwa hospitali kwa muda.

Mercy Kyallo
Mercy Kyallo

“Kwa kweli sikuwa nimemkashifu Baba yake Ivanna bali alikuwa rafiki yake kwa kuingilia mambo ya familia sana, baada ya kukejeliwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii niliumia sana

Jambo ambalo liliniuma wakati huo ni mmoja wa mashabiki aliponiambia nipambane na hali yangu na niache ya wengine yaani ‘i should mind my own business.” Alizungumza Mercy.

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao yetu ya kijamii ya youtube.