Harambee Stars wajikakamua na kutoka sare na wenyeji Misri

Harambee Stars jana walitoka sare ya 1-1 na wenyeji Misri katika mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2021.

Kenya walijipata nyuma ya the Pharaohs kufikia muda wa mapumziko kufuatia bao la Mahmoud Abdel-Moneim. Bao la kusawazisha la Kenya lilifungwa katika dakika ya 67 na Michael Olunga.

Mechi inayofuata ya Stars itakua dhidi ya Togo jumatatu uwanjani Kasarani.

Huenda Lionel Messi akachezea Argentina katika mechi ya kirafiki na Brazil nchini Saudi Arabia hii leo. Mahasimu hao wa Amerika Kusini watakutana jijini Riyadh huku Messi akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa tangu Julai.

Kiungo huyo wa Barcelona alipigwa marufuku ya miezi mitatu kwa kusema kuwa ligi ya Copa America ina ufisadi. Neymar hatacheza kutokana na jeraha la mguu lakini Gabriel Jesus yuko kwenye kikosi.

Uingereza walifuzu kwa Uro mwaka 2020 kwa kucharaza Montenegro mabao 7-0 ugani Wembley. Nahodha Harry Kane alifunga mabao matatu na kupanda hadi katika nafasi ya tano katika orodha ya wafungaji mabao mengi, Uingereza, akiwa amefunga magoli 31 huku Alex Oxlade-Chamberlain, Marcus Rashford na Alexandar Sofranac wakifunga mabao hayo mengine.

Mshambulizi wa Chelsea Olivier Giroud alifunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti mabingwa wa dunia Ufaransa walipotoka nyuma na kuwanyuka Moldova 2-1 katika mechi yao ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 na kupanda hadi kileleni mwa kundi H.

Kufuzu kwa Ufaransa kulijiri kabla ya mechi hio kuanza kutokana na Uturuki kutoka sare na Iceland. Vadim Rata walifungia Moldova dakika tisa baada ya mechi kuanza kabla ya Raphael Varane kusawazisha na Giroud kufanya mambo kuwa 2-1.

Cristiano Ronaldo sasa amesalia na mabao mawili awe na jumla ya mabao100 katika mechi za kimataifa baada ya kufunga mabao matatu jana dhidi ya Lithuania katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2020.

Ureno ilishinda mechi hiyo mabao 6-0. Kiungo huyo wa Juventus mwenye umri wa miaka 34 huenda akawa mchezaji wa pili kufikisha mabao 100 ya kimataifa iwapo atafunga mabao mawili dhidi ya Luxembourg jumapili.

Manchester United ina nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Norway Erling Haaland kinda wa miaka 19, ambaye alifunzwa na Ole Gunnar Solskjaer akiwa Molde. Wakati huo huo United inatarajia kuafikiana na Juventus kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic mwenye umri wa miaka 33, kufanya mazoezi na klabu hiyo mwezi ujao kabla ya uhamisho wa Januari.

Kiungo wa AFC Leopards Moses Mburu ameeleza kufurahishwa na kuregelea mazoezi na timu yake baada ya kukaa nje kwa takriban mwaka mmoja akiuguza jeraha.

Mlinzi huyo alifanyiwa upasuaji mwezi Septemba mwaka uliopita na kuregelea mazoezi miezi minne baadae kabla ya kupata jereha la mguu. AFC Leopards iko katika nafasi ya saba katika ligi ya KPL wakiwa na alama 15 baada ya mechi 9. Wtakabana na Bandari mjini Mombasa alhamisi wiki ijayo.

Kocha wa Chemelil Sugar Francis Baraza ameteuliwa kama kocha mkuu wa timu ya Tanzania Biashara United Mara. Baraza ameondoka Chemelil Sugar, ambao wako katika nafasi ya mwisho katika jedwali la KPL na hawajashinda mechi hata moja tangua kuanza kwa maimu mpya.

Alijiunga na timu hiyo Mei mwaka 2018 na ameshawahi pia kufunza Muhoroni Youth, Sony Sugar na Western Stima.

 

Soma jinsi serikali ya Misri ilivyowaokoa Harambee Stars mjini Cairo

Serikali ya Misri iliwaokoa Harambee Stars waliokua nusura wafurushwe kutoka kwa hoteli yao jijini Cairo kutokana na kutolipwa kwa ada.

Stars wako jijini humo kwa mechi yao ya kufuzu kwa AFCON ya kundi G dhidi ya the Pharaohs leo usiku. Rais wa FKF Nick Mwendwa ameilaumu serikali kwa hali hio ambayo anasema inatishia kusambaratisha mechi yao dhidi ya Misri.

Serikali hata hivyo kupitia kwa katibu wa michezo Kirimi Kaberia ilirushia lawama FKF huku Kaberia akisema hawakuipa serikali taarifa muhimu na kuwa walitaka kupewa pesa taslim.

Harambee Starlets wamewasili salama nchini Tanzania kabla ya kipute cha ubingwa wa kinadada cha CECAFA mwaka 2019 kinachopangiwa kuanza jumamosi.

Hii ni siku moja tu baada ya kinadada hao kuwasili nchini kutoka Zambia ambapo walibanduliwa nje ya michuano ya kufuzu kwa olimpiki ya bara mwaka 2020 na She Polopolo.

Starlets wanatumai kushinda taji hilo ambalo limekua likiwaponyoka katika miaka ya hivi majuzi, watakapoanza kampeni yao dhidi ya Ethiopia jumapili tarehe 17.

Meneja wa Uingereza Gareth Southgate anasema hatasita kumchagua kiungo Raheem Sterling kwa mechi ya jumapili ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 huko Kosovo.

Sterling alichujwa kutoka kwa mechi ya leo baada ya kulumbana na mwenzake Joe Gomez. Uingereza inahitaji alama moja tu dhidi ya Montenegro ili kufuzu. Sterling anayechezea Manchester City Sterling atacheza mechi ya jumapili huko Kosovo.

Wing’a wa Chelsea Callum Hudson-Odoi anasema aliongea na meneja Frank Lampard kumshawishi asalie Stamford Bridge. Kinda huyo wa miaka 19 aliwasilisha ombi la kutaka kuhama mwezi Januari baada ya Chelsea kukataa ofa ya pauni milioni 35 kutoka kwa Bayern Munich.

Hata hivyo Odoi amemfurahisha Lampard aliyechukua uskani msimu wa joto. Odoi atakosa mechi za msimu huu baada ya kupata jeraha la mguu alipokua akicheza katika mechi yao dhidi ya Burnley mwezi Aprili.

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaregea katika ulingo wa soka baada ya kukubali kuwa mkuu wa ukuzaji soka duniani wa FIFA. Hatua hii inamaliza uvumi uliomhusisha mfaransa huyo na kurudi kama meneja wa Bayern Munich.

Wenger aliondoka Gunners Mei mwaka 2018, baada ya miaka 22 mamlakani. Wadhfa wake mpya utasaidia kukuza soka ya kinadada na wanaume na vilevile masuala ya kiufundi.

 

Serikali kulipa marupurupu ya Kenya 7s, kinadada wawachwa nyuma?

Serikali imejitolea kuwalipa timu ya raga nchini marupurupu yao ya michuano ya kufuzu kwa Olimpiki iliyochezwa wikendi iliyopita. Wizara ya michezo imeomba taarifa za benki za wachezaji wote ili kuweza kuwalipa, baada ya timu hiyo kuinyuka Uganda 31-0 na kufuzu kwa michuano hiyo.

Hata hivyo hakukua na taarifa zozote kuhusu marupurupu ya timu ya kinadada ambao pia walifuzu kwa Olimpiki. Hii ni licha ya kinadada hao kumrai waziri Amina Mohammed kuingilia kati.

PATANISHO: Nimebaki nikichekwa na Jamaa aliyeninyang’anya mke

Hayo yakijiri, Tottenham wanatarajia kumchukua mshambuliaji wa kati wa timu ya Roma ya Italia Lorenzo Pellegrini, mwenye umri wa miaka 23, kama mtu anayeweza kuchukua nafasi ya Christian Eriksen. Kwingineko Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United, ikiwezekana mwezi Januari, huku kiungo huyo wa kati Mserbia mwenye umri wa miaka 31 akitarajiwa kwenda Italia.

Miamba wa soka Uhispania Real Madrid wanatathmini kitita cha Uro milioni 400 kumsajili nyota mshambulizi wa PSG Kylian Mbappe. Raia huyo wa Ufaransa alihusishwa na uhamisho hadi Los Blancos wakati alipokua akichezea timu ya Ligue 1 AS Monaco lakini akahamia PSG kwa kitita cha Uro milioni 135.

Mbappe mwenye umri wa miaka 20 awali alihusishwa na uhamisho wa mabingwa hao wa Uropa lakini kwa mujibu wa ripoti za hivi punde Madrid wanamtaka sana mshambulizi huyo na wako tayari kutoa kitita hicho.

Familia ya watu sita waliofariki katika ajali ya barabara, yazika wapendwa wao

Manchester United hawana uhakika atakaporegea Scott McTominay baada ya kupata jeraha la mguu. Kiungo huyo wa kati alijiondoa kutoka kwa kikosi cha Scotland baada ya kufanyiwa uchunguzi jumatatu akiwa na tatizo hilo tangu alhamisi iliyopita waliposhinda mechi yao ya ligi ya Uropa dhidi ya Partizan Belgrade.

McTominay, ambaye ameibuka kuwa mmoja wa wacheza anaowategemea Ole Gunnar Solskjaer msimu huu, alianza katika ushindi wao dhidi Brighton wikendi lakini akalazimika kuondoka mwishoni mwa mechi hio kwani alionekana kuwa na uchungu mno.

 

Mwanariadha Abraham Kiptum apigwa marufuku ya miaka minne

Harambee Starlets hawatoshiriki katika michuano ya Olimpiki 2020

Harambee Starlets hawatashiriki Olimpiki ya mwaka 2020 baada ya kubanduliwa nje ya raundi ya nne ya michuano ya kufuzu na Zambia kwa 1-0 na jumla ya mabao 3-2 ugani Nkoloma, Lusaka jana.

Starlets walihitaji ushindi ili kufuzu kwa raundi ya mwisho ya michuano hio ambapo wangechuana na aisha Ivory Coast au Cameroon.

PATANISHO: Nilikuwa nalala na kisu kitandani kwa raha zangu

Bodi ya uchaguzi ya FKF imetangaza vituo vya kaunti vya uchaguzi utakaoandaliwa katika kaunti 18 nchini. Uchaguzi huo utapelekea wajumbe kutoka kwa vilabu kwenye kaunti hizo kuwachagua wagombea 6 kwa kila tawi kuongoza ajenda yao ya kuendeleza soka.

Uchaguzi huo utafanyika wikendi ijayo. Bodi hio kwa sasa inathibitisha wapiga kura kufuatia kuchapishwa kwa orodha yao wiki iliyopita.

Bingwa wa mbio za Marathon Eliud Kipchoge yuko katika orodha ya mwisho ya wanariadha watano watakaotuzwa katika tuzo za wanariadha duniani huko Monaco.

Hata hivyo mwenzake Timothy Cheruiyot alibanduliwa nje ya orodha hiyo iliyotangazwa jana na IAAF. Wanariadha hao wengine ni mganda Joshua Cheptegei, Mwamerika Sam Kendricks, mwenzake Noah Lyles na raia wa Norway Karsten Warholm.

Mutyambai achukuwa hatua dhidi ya polisi waliompiga kinyama mwanafunzi wa JKUAT Jumatatu

Unai Emery amepewa uungwaji mkono na usimamizi wa Arsenal lakini akaonywa kuwa lazima matokeo yaimarike. Kocha huyo mkuu amekua chini ya shinikizo kali kufuatia msururu wa matokeo mabaya na rekodi ya ushindi wa mechi mbili tu katika mechi kumi za ligi ya Primia.

Emery aliteuliwa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger Mei mwaka wa 2018 na msimu wake wa kwanza uliishia na kushindwa mabao 4-1 na Chelsea katika fainali ya ligi ya Uropa.

 

Utumizi wa teknolojia ya VAR katika ligi ya Primia umepewa alama 7 kati ya 10 na wasimamizi wake licha ya kukashifiwa sana. Neil Swarbrick anasema VAR itaboreka na akawataka mashabiki kuwa na subira baada ya wiki nyingine ya utata.

VAR ilianza kutumika katika ligi ya Primia msimu huu baada ya kujaribiwa katika kombe la Carabao na FA, lakini imewakasirisha mashabiki wanaosema muda unaochukua kufanya maamuzi humaliza morali wa mechi.

Inaaminika kuwa usahihi wa maamuzi muhimu kama vile magoli, kadi nyekundu na penalti umeongezeka kutoka asilimia 82 msimu uliopita hadi asilimia 90 msimu huu.

Wajua mapato ya Messi ni maradufu ya Ronaldo? Orodha ya Mishahara ya Wanasoka 10 Bora Duniani

Raheem Sterling hatacheza mechi ya Uingereza ya kufuzu kwa Uropa dhidi ya Montenegro Alhamisi kufuatia patashika lililozuka St George’s Park. Meneja wa Uingereza Gareth Southgate anasema Sterling alilumbana na Joe Gomez kufikia mwishoni mwa mechi ya Liverpool waliyoshinda 3-1 dhidi ya Man City jumapili. Inaarifiwa kuwa wawili hao walilumbana tena walipokutana jana kwa mazoezi ya Uingereza na kumpelekea Sterling kujiondoa kutoka kwa kikosi hicho.

 

Wajua mapato ya Messi ni maradufu ya Ronaldo? Orodha ya Mishahara ya Wanasoka 10 Bora Duniani

Ni wazi  kwamba watu wengi sana huthamini soka kwa kuwa unavutia donge noo  sana, ila baadhi ya mashabiki hawajui ni kwamba  mapato ya kila  mwanasoka hutofautiana sana kulingana na ubora wake  na ustadi wake kwa timu anayochezea.

Katika ulingo wa soka, Messi yupo kileleni kwa  wale wanaotiia kikapuni  mpunga mkubwa sana ambayo ni maradufu zaidi ya kile mshindani wake Ronaldo anapata kila mwezi.

Kulingana na ripoti iliyochapishwa na  L’Equipe,  nyota wa Barcelona Lionel Messi anaongoza  kutokana na kiasi kukubwa cha mshahara anayolipwa.

Mwajentina huyu  ambaye hucheza kama kiungo wa mbele ,  hutia mfukoni  kima cha  pauni milioni 8.3, hii ni takribani  shilingi milioni  957,874,833.95 kila mwezi.

Naye nyota wa Ureno, ambaye aligura Real madrid na kujiunga na Juventus analipwa kima cha pauni milioni 4.7 kila mwezi ambayo ni shilingi milioni  542,445,183.36.

Ronaldo ndiye mwanasoka wa pekee anayecheza kule Italiano ambaye amerodhoshwa kwenye 10 bora.

Timu ya AS Roma yazindua ukurasa rasmi wa Kiswahili

Hata hivyo, Hispania  inaongoza katika orodha hiyo wakiongoza huku watano kati yao wakichezea ligi ya La Liga.

Hii hapa ni orodha ya wachezaji 10 wa soka wanaolipwa donge nono kila mwezi kabla ya kutozwa ushuru:

 

1. Lionel Messi (€8.3 Million)

2. Cristiano Ronaldo (€4.7 Million)

3. Antoine Griezmann (€3.3 Million)

4. Neymar (€3.06 Million)

5. Luis Suarez (€2.9 Million)

6. Gareth Bale (€2.5 Million)

7. Philippe Coutinho (€2.3 Million)

8. Alexis Sanchez (€2.28 Million)

9. Kylian Mbappe (€1.73 Million)

10. Mesut Ozil (€1.6 Million).

Sofapaka wapata afueni baada ya kupata ufadhili wa milioni 35

Hongera! Kenya 7s yafuzu kwa michuano ya Olimpiki Japan 2020

Timu ya raga ya wachezaji saba kila upande ilifuzu kwa mchuano ya Olimpiki Japan mwaka ujao, baada a kuilaza Uganda 31-0 katika fainali za Africa 7s jana, mjini in Jo Berg, Afrika kusini.

Oscar Dennis alifunga mara mbili huku , nahodha Andrew Amonde, Daniel Taabu, na Jeff Oluoch pia wakifunga. Shujaa wanarejea kwa mara ya pili baada ya kuwakilisha Afrika katika awamu ya Rio 2016.

Timu hio itarejea nyumbani kesho huku wakianza mazoezi ya mkondo kwanza wa IRB sevens, itakayochezwa Dubai mwezi ujao.

Hayo yakijiri, mabingwa KCB walilaza Top Fry Nakuru alama 50-13 huku Homeboyz, wakiwanyuka Menengai Oilers 25-20 katika michuano ya ligi ya raga ya Kenya cup.

Kabras nao waliwagwaruza Impala 25 -3 na kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa baada ya mechi ya tatu, sawia na KCB na Homeboyz. Kwingineko Mwamba waliwagwaruza Kisumu 65- 22, nao Nondes wakiwalima Blakblad 38- 23.

Tukielekea ulaya, Leicester ilipanda hadi nafasi ya pili kwenye jedwali ya EPL baada ya kuinyuka Arsenali 2-0. The foxes walipachika mabao yao kupitia mfungaji bora Jamie Vardy na James Maddison katika kipindi cha pili na kuhakikisha Arsenali wameshuka hadi nafasi ya sita.

kwingineko, Chelsea ililaza Crystal Palace 2-0 kupitia mabao ya Tammy Abraham na Christian Pulisic na kupanda hadi nafasi ya tatu. huku Sheffield United ikipanda hadi nafasi ya tano bada ya sare ya 1-1 na Tottenham.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ”hakuna nafasi kabisa ” ya klabu hiyo kumsajili Kylian Mbappe, ingawa kumekuwa na kampeni za mitandao ya kijamii kuhusu tetesi za kuwa mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain ,20 atatua kwenye klabu hiyo.

Barcelona walirejea kileleni mwa ligi ya Uhispania baada ya kuilaza Celta Vigo mabao 4-1, huku nahodha Lionel Messi akifunga magoli matatu naye Sergio Busquets akiongeza la nne.

Lucas Olaza alifungia Celta goli la kufuta machozi. Ushindi huo ulihakikisha Barca wamejizolea alama 25 sawia na mahasidi Real Madrid huku wakiwa na magoli mengi.

Real Madrid nao wailiwaadhibu Eibar 4-0 huku Karim Benzema akifunga mawili nao Sergio Ramos na Federico Valverde ’wakiongeza moja kila mmoja.

Katika ligi ya Ujerumani, mabingwa Bayern Munich waliwapiga Bourssia Dortmund 4-0, chini ya mkufunzi wa muda Hansi Flick.

Robert Lewandowski alifunga magoli mawili huku Serge Gnabry akiongeza la tatu naye mlinzi Matts Hummels akijifunga mwenyewe. Bayern walipanda hadi nafasi ya tatu na alama 21, alama moja nyuma ya Borussia Mönchengladbach ambao hawajacheza mechi moja.

Ligi ya Uingereza: ushindani wa kumaliza katika nne bora

Ligi ya Uingereza itakuwa inachezwa wikendi hii huku klabu mbali mbali zikiwa na matarajio ya kumaliza katika orodha ya nne bora katika msimu huu wa mwaka 2019/2020.

Vijana wake Pep Guardiola waliweza kumaliza kileleni katika msimu uliopita baada ya ushindani mkali kushuhudiwa kati yao na Liverpool.

Mariga akubali kubwagwa, amualika Imran chakula cha mchana – Video

 Kwa sasa  klabu ya Liverpool inaongoza kwenye ligi hiyo ikiwa na pointi 31, wakifuatiwa na Manchester City ambayo wameweza kupata pointi 25, huku Leicester na Chelsea wakifunga orodha ya nne bora kila mmoja akiandikisha pointi 23.

Michuano ambayo itachezwa wikendi hii itachangia pakubwa kuthibitisha klabu ambazo huenda ikamaliza katika nafasi ya nne bora msimu huu.

‘Mungu anayesababisha mwanamke “tasa” kuimba,’ Kambua apeana sababu za kusifu

 Manchester United, Tottenham, na Arsenal pia ni miongoni mwa klabu ambazo zinatarajiwa kuleta ushindani mkubwa.

Mechi kubwa wikendi hii itakuwa baina ya Liverpool na Mancity ambao wanashikilia nafasi ya kwanza na pili mtawalia.

Mechi zingine ni;

Chelsea vs Crystal Palace

chelsea

Tottenham vs Sheffield Utd

dele

Leicester vs Arsenal

auba

Man United vs Brighton

pogba

 

Baab kubwa! Mechi 10 za kutazamiwa mwezi huu wa Novemba

Mwezi mpya wa Novemba upo nasi na kwa wanaopenda kadanda mwajua vyema kuwa hili lamaanisha mwezi mwingine mwenye mechi kadhaa baab kubwa!

Baada ya ligi kuu ya Uingereza kung’oa nanga mwezi wa Agosti, tayari tumeshuhudia mechi za kufana baina ya timu kuu kuu na pia timu zinazovuta mkia zikijikakamua dhidi ya mababe wa ligi.

Leicester City hivi majuzi waliandikisha historia baada ya kuvunja rekodi ya Manchester United walipowanyuka Southampton 0-9 ugani St Mary’s.

Vijana hao wa Brendan Rodgers wamewashtua wengi kwani sasa wamepanda jedwali na wanashikilia nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool na Manchester City.

Hata hivyo, usisahau kuna mechi za ligi kuu za Uhispania, Ujerumani, Italia na hata pia ligi ya mabingwa ulaya.

Radio Jambo tumekuandalia orodha ya mechi 10 ambazo hufai kukosa mwezi huu wa Disemba.

  1. Borussia Dortmund vs Inter Milan (Novemba 5, 2019)

inter

2. Chelsea vs Ajax (Novemba 5, 2019)

chelsea (1)

3. Real Madrid vs PSG (26, Novemba, 2019)

psg (1)

4. Juventus vs Atletico Madrid (26 Novemba, 2019)

juve

5. Juventus vs AC Milan (10 Novemba, 2019)

juvee

6. Liverpool vs Man City (10 Novemba, 2019)

liv (1)

7. Leicester City vs Arsenal (9 Novemba, 2019)

lei

8. Man City vs Chelsea (23 Novemba, 2019)

chel (1)

9. Real Madrid vs Real Sociedad (23 Novemba, 2019)

Real Madrid vs Real Sociedad

 

10. Liverpool vs Napoli (27 Novemba, 2019)

napoli

Man United waandikishwa ushindi wao mkubwa zaidi tangu Agosti

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kikosi chake kilikua na mpango wa jinsi wangecheza msimu huu waliwapowanyuka Partizan Belgrade na kufuzu kwa 32 bora katika ligi ya Uropa.

Mabao ya kipindi cha kwanza ya Mason Greenwood na Anthony Martial yalifuatiwa na la Marcus Rashford baada ya mapumziko na kutamatisha ushindi mkubwa zaidi wa United tangu Agosti. Ushindi huo unakiweka kikosi cha Solskjaer kileleni mwa kundi L.

Aaron Ramsey amekiri kua alimwomba radhi Cristiano Ronaldo kwa kukatiza na kumnyima rekodi nyingine ya ligi ya mabingwa.

Raia huyo wa Wales aliwaweka waItalia mbele baada ya dakika tatu tu za mechi yao waliowanyuka Lokomotiv Moscow 2-1 jumatano baada ya kuzuia mkwaju wa adhabu wa Ronaldo.

Ligi ya mabingwa Uropa: Man United watashinda?

Katika mchakato huo Ramsey alimnyima mreno huyo rekodi ya Champions League ya kufunga dhidi ya vilabu vingi zaidi lakini akakiri kuwa hisia zake ziliingilia kati ili kuhakikisha timu yake inafunga.

Mabao mawili ya kipindi cha pili yaliwapa Rangers ushindi dhidi ya Porto na kukaribia kufuzu kwa awamu ya mchujo ya mishuano ya ligi ya Uropa.

Vijana wa Steven Gerrard Alfredo Morelos na Steven Davis walifunga mabao ya Rangers. Matokeo haya yana maana kuwa Rangers wako kileleni mwa kundi G pamoja na Young Boys wa Uswizi wakiwa na mechi mbili zilizosalia, huku Porto na Feyenoord wakiwa alama tatu nyuma.

Orodha ya wagombea wa viti mbalimbali ambao hawakujipigia kura wakati wa uchaguzi

Kocha wa Harambee Starlets David Ouma ametoa wito kwa wakenya kujitokeza kuwashabikia kinadada hao katika mechi yao ya kufuzu kwa michuano ya Olimpiki dhidi ya Shepolopolo ya Zambia hii leo ugani Kasarani.

Hakuna ada ya kiingilio ya mchuano huo kwani FKF inataka mashabiki wengi zaidi kujitokeza kuwashabikia Starlets. Mechi ya marudio itachezwa Lusaka siku ya Jumatatu.

Arsene Wenger amekanusha fununu kuwa anajadiliana na Bayern Munich kuwa meneja wao mpya lakini amejiepusha kujiondoa kutoka kwa kinyang’anyiro hicho. Miamba hao wa Ujerumani wanamtafuta meneja mpya baada ya kumfuta kazi Niko Kovac, baada ya kunyukwa mabao 5-1 na Eintracht Frankfurt.

Wenger alishinda ligi ya Primia mara tatu na kombe la FA Cup mara saba katika tajriba yake ya miaka 22 North London kabla ya kuondoka mwaka wa 2017-18.

Aina mpya ya virusi vya HIV yagunduliwa na wanasayansi

 

Ligi ya mabingwa Uropa: Man United watashinda?

Klabu mbali mbali kutoka bara Uropa zinatarajiwa kuchuana leo usiku huku wakufunzi wakiwa na imani kuwa wachezaji wao wataweza kuandikisha ushindi ili waweze kufuzu katika ngazi utakaofuata.

Man United vs Partizan

Vijana wake Ole Gunnar Solsjaer watakuwa wanakaribisha klabu ya Partizan uwanjani Old Trafford.

Afisa wa CDF akamatwa kwa tuhuma za kuhonga wapiga kura Kibra

 Man United walipoteza mechi dhidi ya Bounermouth katika ligi ya Uingereza wikendi uliopita na mashabiki wao wanatarajia klabu hio itapata ushindi usiku wa leo.

Klabu ya Partizan kwa sasa wanashikilia nambari tatu wakiwa na pointi 4 katika kundi L, huku Man United wakiwa kileleni na pointi 7.

Utabiri wangu ni Man united watashinda mechi hiyo kwa mabao 3-1.

martial

Roma vs Monchengladbach

PICHA: Mamake Ken Okoth apiga kura katika uchaguzi mdogo Kibra

 Ni mchuano ambayo klabu ya Roma wanatarajiwa kupata ushindi mkubwa kwani wapo kileleni katika kundi J wakiwa na pointi 5 huku Monchengladbach wakiwa wa mwisho katika kundi hilo na pointi 2.

Utabiri wangu ni Roma itashinda mechi hiyo kwa mabao 4-2.

roooma