CENSUS: Bungoma yajitokeza asilimia 100 kuhesabiwa

Wakaazi wa kaunti ya Bungoma wamepongezwa kwa kujitokeza kwa asimilia mia moja kuhesabiwa katika zoezi la census.

Akiongea alipozuru kaunti hio kutazama jinsi zoezi hilo linatekelezwa Head of public service Wanyama Musiambo amesema kwamba sehemu za mlima Elgon ambazo zilidhaniwa kuwa zitawapa maafisa wanaotekeleza zoezi hilo ugumu zimekuwa miongoni mwa sehemu ambazo zoezi hilo limetekelezwa vyema.

Kamishina wa Bungoma Stephen Kihara amewataka wakaazi ambao bado hawajahesabiwa kufanyiwa hivi kabla ya zoezi hilo kukamilika.

Idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi katika kaunti ya Taita Taveta imeongezeka katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na kufikia asilimia 25.

Kulingana na  ripoti iliyotolewa na mashirika ya kijamii kaunti hiyo, wanawake wamepiga hatua katika swala la umiliki wa mashamba huku wakitoa wito kwa serikali ya kaunti kubuni sheria zitakazosaidia wanawake kumiliki ardhi zaidi.