Cha kusikitisha! Mapacha waaga baada ya mashua kuzama wakivua samaki

capsize
capsize
Kilichotakiwa kuwa uvuvi wa kawaida kiligeuka ghafla na kuwa janga la kuwakereketa wengi maini baada ya mapacha kuzama bahari hindi mtaa wa ufuo wa bahari wa Watamu, kaunti ya Kilifi.
Pacha hawa, pamoja na wavuvi wawili walikuwa wamefunga safari kuenda  kati ya bahari hindi kuvua kisha mashua waliyokuwa ndani ikatikiswa na upepo mkali na kuwafanya watoto hawa wazame.
Wavuvi hawa waliogelea vizuri na kuokoa maisha yao.

Hata hivyo, mmoja wa pacha hawa aliokolewa baada ya masaa mawili na kupelekwa katika hospitali ya Malindi lakini kwa bahati mbaya akafariki akiendelea kupewa matibabu.
Mwili wa pacha mwingine ulipatikana saa kumi na moja jioni.
Kwa sasa, mipango ya mazishi ndiyo yanayoendelea.
Kwa kuthibitisha kisa hiki, mkubwa wa polisi wa kaunti ya Malindi bwana Philip Wambugu alisema kuwa,wavuvi wanafaa kufanya utafiti na kujua mawimbi baharini yako vipi kabla ya kuenda kuvua.

Vilevile alisema kuwa, hata kama wavuvi wengi wamezoea  maisha ya bahari, hawafai kuchukulia onyo wanayopewa kama mzaha.

“Many fisherman have been in fishing for long and they should not take precautions for granted because they have experience,”Philip Wambugu alisema.