Chagua chagua utajipata single forever!Podcast kuhusu kinachokuzuia kupata mtu(Part 1)

Katika podi yangu  maalum ya  kila siku  tuliangazia baadhi ya mambo ambayo huenda yanakuzuia kupata mtu wa kuanza maisha naye. Wakati mwingine tunajibana katika vijikanuni tunavyojiwekea.

Katika hali nyingine ni kwa sababu ya kutojiamini au kuogopa kuvunjwa moyo. Sikiza podi nzima ujue tatizo huenda liko wapi na pia kuna ilani , hili halimaanishi kwamba lazima uwe katika mahusiano kwa sababu wakati mwingine unanawiri hata zaidi na kuwa na furaha ukiwa single –mahusiano au ndoa sio mafanikio kama inavyoweza kukupa presha jamii.

Watu  hawaishi vituko na katika sehemu ya Pili ya Podi hii, mwenzangu  Mutala Mukosia atakusimulia jinsi ni kibarua kikubwa kwa wanawake kuweza kutosheleza matakwa ya kijamii kabla ya kuonekana kuwa tayari kwa ndoa.