Nigeria na Senegal tayari zimefuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya kombe la afcon na leo tutafahamu zitachuana na timu gani. Makabiliano makali yananukia leo kati ya Ivory coast na Algeria ,miamba wazito wa soka barani ambapo wengi wanatabiri huenda matuta ya penalty ndio yatakayoamua mshindi .
Mechi hiyo itaanza saa moja jioni na itapeperushwa mubashara hapa radio Jambo .Baadaye mwendo wa saa nne usiku Vijana wapya katika kipute hicho Madagascar wanajipima maarifa dhidi ya vigogo Tunisia huezi kujua matokeo yatakuwa yepi.
Tayari timu nzito na zenye wachezaji tajika kama vile wenyeji Misri ,Mali ,Ghana Morocco na Cameroun zimeonyesha mlango kutoka mashindano hayo .Je unafikiri timu gani mbili zitatamba leo kati ya Ivory Coast dhidi ya Algeria na Madagascar dhidi ya Tunisia?