'You changed my life.' Harmonize na mkewe washerehekea miaka minne katika ndoa

Msanii wa nyimbo za bongo Harmonize na mkewe Sarah Michelotti wanasherehekea miaka minne katika ndoa. Wawili hao walioana mwaka jana katika harusi ya siri.

Kulingana na sarah, walianza kuchumbiana na Harmonize mwaka wa 2016.

“HAPPY ANNIVERSAY ❤️🤴🏾… 11/05/2016🔥🔥 the day that changed my life.. ‘WE LOVED WITH A LOVE THAT WAS MORE THAN LOVE’. 👸” Aliandika Sarah.

Harmonize hakunyamaza alimjibu,

“LOVE YOU 4 EVER." Harmonize Alijibu.

Baadae Harmonize kupitia mitandao ya kijamii aliandika;

“HAPPY ANNIVERSARY LOVE OF MY LIFE 🌹”

Haya basi kizungumkuti kiko hapa, kama vile alisema kuwa walikuwa kitu kimoja na Harmonize wakati huo msanii huyo alikuwa mchumba wa Wolper.

Awali Wolper alidai kuwa Sarah alimnyanganya msanii Harmonize na kisha wakaanza safari yao rasmi ya kuwa wapenzi.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO