Cheche zaibuka baina ya mirengo inayoshabikia upande wa Ruto na Gideon Moi

55ft1JC2.jfif
55ft1JC2.jfif
Ubabe wa uongozi haswa katika jamii ya Kalenjin nchini unatazamiwa kuchukuwa mkondo mwengine baada ya viongozi wanaoshabikia upande wa Ruto na Gedion Moi kuanza kukabiliana kwa maneno makali baada ya Ruto kuzuru wazee wa Talai wiki jana.

Viongozi wanaoegemea upande wa seneta wa Baringo Gedion Moi,wamekashifu hatua ya Ruto kujiwasilisha katika eneo kuombewa na wazee hao wakisema walikuwa wanapania kumuombea Gedion kama kiongozi wao.

Akiwa kwa mazungumzo na jarida moja la humu nchini,katibu mkuu wa chama cha KANU Nick Salat amesema ni wazi kuwa Ruto ni kiongozi ambaye anajitakia makuu bila ya kulijali taifa ama jamii yake ya Kalenjin.

Salat alisema baadhi ya viongozi wa wazee hao walikuwa wanapania kumuombea Moi na kuwa kiongozi wao wa kisiasa.

"He has been blasting others for visiting shrines but what happened is a sign of desperation and wants the community to sympathise with him,"amesema Salat.

Salat ameongezea kuwa hakuna mtu yeyote kutoka Rift Valley anayemuonea huruma Ruto kwa yale anayopitia baada ya kuamua kulemaza utendakazi wa rais Kenyatta.

"The Friday meeting had no impact on us at all,amesema Salat.

Aidha wazee hao wa Talai walisema kuwa hakna njama fiche katika maombi yao kwani walikuwa wanamuombe tu Ruto.