Chelsea kumenyana na Man U wikendi ya kwanza ya EPL 2019/2020

Ratiba ya michuano ya mwaka 2019/20 ya Ligi ya Uingereza metolewa leo asubuhi.

Miongoni mwa mechi ambazo zimeleta furaha chungu nzima dhidi ya mashabiki ni mechi kati ya Manchester United na Chelsea.

Mechi hiyo ya kukata na shoka itachezwa jumapili ya kwanza ya msimu, tarehe 11, Agosti kuanzia mida ya 6:30. Isitoshe, Chelsea watakuwa wamemenyana na Liverpool katika shindano la Super Cup ambalo hung'ang'aniwa na washindi wa Europa pamoja na washindi wa kombe la mabingwa wa ulaya.

Usisahau kuwa staa wa Chelsea, Eden Hazard tayari amehamia wababe wa ligi kuu ya uhispania, Real Madrid.

Washindi wa ligi msimu ulioisha, Manchester City wataanza safari ya kutetea taji lao kwa mara ya pili Jumamosi saa nane wakiwa ugenini kwa West Ham.

Liverpool ambao walimaliza katika nafasi ya pili, ndio watakaoanzisha msimu huu mpya dhidi ya Norwich, ambao walipandishwa ngazi. Mechi hiyo itakuwa siku ya Ijumaa tarehe 9, mida ya saa nne usiku.

Timu ya Arsenal ambayo haikufuzu katika nne bora, itafungua msimu wao dhidi ya Newcastle, kikosi chake Rafa Benitez katika uwanja wa St. James Park siku ya Jumapili, tarehe 11 saa kumi jioni.

Timu yake nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama, Tottenham Hotspur watawakaribisha Aston Villa katika uwanja wao mpya wa White Hart Lane, Jumamosi, tarehe 10, saa moja unusu.

Msimu huo mpya unamepangiwa kuanza Agosti tarehe 10 na utaendelea hadi Mei tarehe 17 mwaka ujao.

Kwa mara ya kwanza ligi hio itachukua mapumziko ya msimu wa baridi huku tarehe zikitarajiwa kutangazwa baadae. EPL pia itaanza kutumia marefa wa VAR msimu huu.

Tazama jedwali ambalo lina ratiba ya mechi za wiki ya kwanza.